Hii ni business mkuu, jamaa anataka kutimiza lengo la kupata faida (profit) hata kama anasolve tatizo lililopo katika jamii. Katuni mjongeo kwa sasa zina market lakini ukiacha zlizotaget watoto kuelimisha kama fataki, ubongo kids kuna hizi za kuburudisha tu. Hizi ndo hizi za mpemba og na kuna kipindi bwakila alitoa hizi
Jamaa anataka aweke kazi yenye mtiririko kama ile vitabu ya marvel. Anataka kuurudisha kwa kina Dr. Tamba.. kutoa elimu kwa katuni labda watoto ndo uwatarget na hawa hawana uwezo wa kumiliki simu. So kuna namna hii plan inaweza kuwa threat sabab wanaokilim sim n watu wazima ambao wanawez kuangalia for fun tu. Mm naomba tujadili hapa apate kitu cha kumsaidia kwenye setup the way forwad
Anyway tufanye hivi mkuu,
.
Target Audience
Watoto mashuleni, Kama ulivyosema, mlengwa ni watoto kwa ajili ya kutoa elimu kama vile Dr. Tamba au Ubongo Kids. Changamoto ni kuwa watoto wengi hawana uwezo wa kumiliki simu. Njia nzuri inaweza kuwa kupitia TV, au kushirikiana na shule ili vipindi vipelekwe madarasani.
Kwa Watu Wazima kama Burudani, Watu wenye simu watafuatilia maudhui kama burudani. Kuchanganya ucheshi na utamaduni, kama vile "Mpemba OG" au "Bwakila" na wengineo.
.
Majukwaa na Upatikanaji wa
Vipindi vya TV, kama ulivyosema watoto wengi hawana simu, atengeneze mfululizo wa katuni zitakazoonyeshwa kwenye vituo vya TV, au majukwaa ya kidijitali yanayolenga familia.
Programu za Simu/application , app ya simu kwa ajili ya watu wazima wanaofurahia katuni kama burudani. Unaweza kujumuisha maudhui yenye elimu kidogo au vichekesho kwa watu wazima kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii (TikTok, Facebook na YouTube). Bila kusahau parental control.
Kuandaa Vitabu + ubia na shule husika, kuunda vitabu vya katuni au programu za kielimu zitakazotumika shuleni, hasa katika maeneo yenye upatikanaji mdogo wa simu.
.
Muendeleo wa Hadithi
Maudhui ya Mfululizo (Serialized Content), Kama ulivyotoa Mfano wa Marvel, inabidi kujenga hadithi za muda mrefu zenye matukio fulani yanayovutia watazamaji. Wahusika kama ( Dr. Tamba ), itakusaidia kuendeleza au kuleta mambo mbalimbali kama
afya, Lishe, historia, au utamaduni kadri mfululizo unavyoendelea.
Hapa ni kuchanganya hadithi za kitamaduni, lugha za asili, au marejeleo ya kitamaduni ili kuwavutia watazamaji wengi zaidi.
. Mfumo wa Mapato (Revenue Model)
Uuzaji wa Bidhaa, vitabu, au bidhaa za chapa zinazovutia watoto.( inahitaji uvumilivu kidogo mpaka uje kuaza kupata faida kwenye hii biashara)
Tafuta wadhamini, kushirikisha taasisi za elimu au mashirika yasiyo ya kiserikali ili kusaidia kudhamini katuni zinazofundisha masomo muhimu.
Mapato ya YouTube, Kwa katuni zinazowalenga watu wazima, unaweza kutumia YouTube, Facebook, Instagram na TikTok kupata faida kupitia matangazo au maudhui yanayodhaminiwa.
. Kukabiliana na Vitisho (Threat Mitigation)
Kuhusu matumizi ya Simu kwa Watoto, kukabiliana na changamoto ya watoto kukosa simu, jikite zaidi kwenye TV, mfululizo wa kwenye wavuti, au kwenye maeneo ya jamii kama shule, maktaba, au hata vituo vya jamii vyenye vifaa vya kuonyesha filamu.
PROJECT HII NI KUBWA SANA, mambo ya kuzingatia:-
. Mtaji ( ingawa Unaweza kuaza kidogo kidogo)
. Udini ( achana na masuala ya Udini, wengi sana huwa wanafeli sana kwenye hichi kipengele)
. Mawazo ya story ( story iwe ndefu isiyo pungukiwa utamu,)
. Vibali + usajili ( hili ni jambo la Kawaida)
. Bila kusahau majina mazuri yenye kuvutia kwenye hizo katuni ( hii Itasaidia watoto kukumbuka character wa hizo katuni), ikiwezekana zaidi usitumie kabisa majina ya kidini)