Naombeni ushauri kuhusu mahusiano haya ya mama yangu na huyu mwanaume

Naombeni ushauri kuhusu mahusiano haya ya mama yangu na huyu mwanaume

watoto lazima tutambue kuwa kuna mambo tunaweza kuwashauri wazazi wetu....lakini kuna mambo yao mengine ni vigumu kuwashauri....kamwe huwezi kumshauri mzazi wako mambo ya mapenzi...kumbuka kuwa alie mpenda mama yako ndie baba yako...
 
Habari zenu,

Nimekuja na ID mpya ili kuficha utambulisho wangu wa awali ni kuomba msaada wa ushauri.

Naombeni ushauri na njia za kutatua tatizo hili.Ipo hivi kwenye tumbo la Mama yetu tulikuwa watoto 7 hadi Leo hii tupo 4. Katika watoto 7 tumezaliwa na Baba tofautitofauti 4. Katika hao baba zetu kuna moja wao ndio tumekuliwa kwake toka tukiwa wadogo badaye miaka 6 iliyopita Mama alitengana Nate.

Mama ni mtumishi wa umma, hivyo alinunua kiwanja na kujenga nyumba ambapo watoto wote 4 tuliongozana nae na kwenda kuishi nae, maana haikuwezekana kukaa tena kwa huyo baba mlezi sababu katika wathili.4 tuliobaki kati yetu 1 tu ndio mwanae kwahiyo ikabidi wote sisi sote tuongozane na mama. Ikumbuke kuwa katika sisi watoto 4, mtoto 1 hamjui baba yake wengine 2 Baba yao alifariki na mtoto 1 baba take ndio huyo aliyetulea.

Sisi sote miaka yetu ni 24+ na Mama yetu ni 52, jambo linalotusumbua ni kuwa Mama yetu ana mwanaume mwingine ambaye ni mume wa mtu. Jamaa huyu huwa anakuja na kulala hapa nyumbani karibu kila siku; huwa anasitisha kuja pale ambapo kaka yetu mkubwa akija nyumbani.

Ndugu na marafiki wamejaribu kumshauri mama kuwa tayari umri umekwenda na ana vijana wakubwa anatakiwa kuacha mambo hayo pasipo mafanikio, haelezeki wala haambiwi chochote. Kwa sasa tumefunga chuo sababu ya hii CORONA nipo hapa home naona aibu kijiji kizima kinatuzungumza.

Kaka yangu mkubwa alijaribu kuongea na huyo bwana mwaka jana; kwa kweli jamaa alisitisha kama miezi 2 hivi pasipo kuonekana, badaye ratiba ikaanza kama kawaida nimemjulisha kaka atafute siku 3 nyumbani tusaidiane kutatua tatizo hili. Pia, kila tukimsuhi Mama kuacha hiyo tabia majibu anayotupa ni kuwa huu mji ni wake na hamna aliyemsaidia kujenga hivyo anafanya chochote atakacho.

Ndugu zangu wana JF, naombeni msaada wa mawazo namna ya kutatua tatizo hili.
Kitu cha kwanza tambueni kuwa jinsi mnavyogombana naye ndivyo mbavyokaribisha pepo lake liwaingie na kuwatesa maishani.
Ukiwa mwanamke ogopa sana kuzalia nyumbani hiyo haifi na uzao wako watafanya hivyo.
Pambaneni na namna ya kuepuka tabia ya mama kuwa yenu.Ni wazi mama kashindwa kuishi na wanaume kwa tabia zake za ubabe.Tena nahisi kazi ya mama ni mwalimu ama nesi.
Ushauri wangu kwako achaneni naye kabisa mkishindwa shirikisheni ndugu nayo isiwe lazima kwa sababu tatizo la mama lipo ktk damu ambayo tayari imewaumba mnaishi nayo hivyo probability ya ninyi kuwa hivyo ni kubwa ingawa mwaweza kujiepusha.

Poleni kwa hayo yanayowasibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie mlitaka Mama awe analiwa na bodaboda wa kitaa?
 
Hamna tatizo hapo. Ona Ankali Shante anavolelewa kwa gharama ya kuzungusha kiuno.
 
Huyo mama anaonekana anaishi maisha ya usichana wakat abakaribia kuwa bb. Kwa nn asiende kuish kwa huyo mwanaume huko aliko huyo mwanaume. Kuketa mwanaume humo ndani anakuwa anajidharau sana
 
Hahahaha itakua wewe ni mmoja wa watoto wa huyo mama, poleni kwa mnayopitia.

Boost your Immune System to fight a Covid-19.

Huwa tunawatazama wazazi kama role models katika vitu vingi. Mama anavibehave hivyo, inakatisha tamaa, na inasonenesha sana. Na jamaa kazungumzia yeye ni mwanafunzi, bado anategemea msaada wa wazazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa tunawatazama wazazi kama role models katika vitu vingi. Mama anavibehave hivyo, inakatisha tamaa, na inasonenesha sana. Na jamaa kazungumzia yeye ni mwanafunzi, bado anategemea msaada wa wazazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mama ana behave vipi?
Yaan kwa kua ana watoto ndio asiwe na mpenzi? Mbona watu mnakua selfish sana, kwani yeye sio binaadam? Hana matamanio?
Angekua anabadilisha leo mwanaume huyu kesho yule hapo home hapo sawa lakini kampata mwenza wake kwanini asi enjoy?

Boost your Immune System to fight a Covid-19.
 
Bado tuu hamjamzoea mama yenu.kwa mujibu wa maelezo yenu mama yenu amewazaa kutoka kwa wababa tofauti .so ameshazoea huenda alikuwa hana mpango wa kuwapata nyinyi ilikuwa ni mimba za bahati mbaya wakati wa starehe zake.

maadamu hata munasomeshwa mpaka chuo ,nyie subirieni chuo kifunguliwe muende chuoni sasa hivi huyo jamaa endeleeni kuwita uncle.sababu huwezi jua labda ndiyo anayelipa ada zenu za chuo na mahitaji yote hapo home
 
Mama ana behave vipi?
Yaan kwa kua ana watoto ndio asiwe na mpenzi? Mbona watu mnakua selfish sana, kwani yeye sio binaadam? Hana matamanio?
Angekua anabadilisha leo mwanaume huyu kesho yule hapo home hapo sawa lakini kampata mwenza wake kwanini asi enjoy?

Boost your Immune System to fight a Covid-19.

Watoto saba, wanaume wanne. Na huyu wa tano. Mama ana shida huyo. Hata kina Wema Sepetu huzeeka ujue

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama ana behave vipi?
Yaan kwa kua ana watoto ndio asiwe na mpenzi? Mbona watu mnakua selfish sana, kwani yeye sio binaadam? Hana matamanio?
Angekua anabadilisha leo mwanaume huyu kesho yule hapo home hapo sawa lakini kampata mwenza wake kwanini asi enjoy?

Boost your Immune System to fight a Covid-19.
So far Mama hajavunja Sheria yoyote
 
Vipi maendeleo Huko? Ba Mdogo Hajaweka Mambo bado?
Mkuu umenichekesha sana..
Bwana mdogo alileta mada hakutegemea replies za kibazazi.😀😀😀

Everyday is Saturday........................... 😎
 
Back
Top Bottom