Naombeni ushauri namna ya kukabiliana na wateja wezi kwenye duka la nguo

Naombeni ushauri namna ya kukabiliana na wateja wezi kwenye duka la nguo

Yeah biashara ya nguo ni ngumu, pia apunguze kuruhusu kujaribishia nguo kama sio lazima, wanamuachia mijasho tu!
Sijawaza hilo la jasho 😜😀😀
Basi ni kazi ngumu sana na inataka uvumilivu haswa
 
Yeah biashara ya nguo ni ngumu, pia apunguze kuruhusu kujaribishia nguo kama sio lazima, wanamuachia mijasho tu!
Yaani kujaribu hapa ni kipengele kweli kweli na wengine ndio wanatumia mwanya huo kuiba
 
Kun
Kamera na wasaidizi ni mawazo yenye msaada.Ila,katika tabia zinazokera ni wizi na uongo.Hivi,akikamatwa mke wa mtu ameiba,mumewe atajisikiaje? Hatari sana.
Yaani tena ni wamama mmoja kaka nje mwingine ndio huyo kaingia ndani ndio kaondoka na nguo. Unatamani kuua mtu
a ma-specialist wa wizi wa maduka ya nguo. Mjomba wangu alikuwa na duka na kuna kipindi nilikuwa naenda kumsaidia na nilijifunza mengi.
Kuna mama mmoja yuko kama shome-shombe hivi anazungumza kama ana asili ya Zenji. Akiingia dukani mwako, anakuliza. Anakuja amevaa baibui, huku ameshika ''sample'' za vigauni, anataka kununua mzigo mkubwa. Anakubabaisha na kukusumbua kwa kusema ''hebu lete ile''. Ukigeuka tu, kwa kasi ya ajabu, anachukuwa gauni lolote lililo karibu, anatumbukiza ndani ya baibui lake (limeshonwa special kwa kuwekewa mifuko ya siri). Nakushauri ujaribu kuweka kijana mbele
 
Kuna ma-specialist wa wizi wa maduka ya nguo. Mjomba wangu alikuwa na duka na kuna kipindi nilikuwa naenda kumsaidia na nilijifunza mengi.
Kuna mama mmoja yuko kama shome-shombe hivi anazungumza kama ana asili ya Zenji. Akiingia dukani mwako, anakuliza. Anakuja amevaa baibui, huku ameshika ''sample'' za vigauni, anataka kununua mzigo mkubwa. Anakubabaisha na kukusumbua kwa kusema ''hebu lete ile''. Ukigeuka tu, kwa kasi ya ajabu, anachukuwa gauni lolote lililo karibu, anatumbukiza ndani ya baibui lake (limeshonwa special kwa kuwekewa mifuko ya siri). Nakushauri ujaribu kuweka kijana mbele ya duka. Wanapokuja wateja wengi yeye anaweka kiti mbele i.e. anageukia lilipo duka na wateja na kuangalia movement zote za wateja. Kingine, muuza duka awe mtu aliye shap, kuweza kuangalia na kugundua nyendo na kusoma saikolojia ya wateja. Ukichukuwa cheap labour hasa kutoka vijijini wasio na u-sharp wa mjini utapigwa sana.
Ni kweli mkuu na ni wamama.inaonyesha wako competent kuiba
 
Funga kamera zitakazokua zinaonekana wazi. Uwepo tu wa kamera utamfanya mtu aogope kwa kuhisi anaonekana
 
Tena wanaozibebaga vizuri ni hawa waliojaliwa miili mikubwa anachukua ata dera anajizungushia kwenye makebo akijidanganya anapima pima
 
Wengine wanatumia dawa kukuzubaisha muuzaji unakuta washaiba wenzio na wametoka.
 
Back
Top Bottom