Naombeni ushauri: Nataka kumzuia mama yangu asiolewe tena baada ya baba kufariki

Naombeni ushauri: Nataka kumzuia mama yangu asiolewe tena baada ya baba kufariki

Habari ndugu zangu. Naombeni ushauri wenu juu ya mada tajwa.

Mzee wetu amefariki miezi 8 iliyopita baada ya maisha yake yote kuwa katika ndoa na mama yetu. Mama Sasa ana umri wa miaka 68. Kwa kipindi chote tangu sisi watoto wake tuanze kujitegemea tumekuwa tukijitahidi kuwawekea mazingira mazuri ya wazee wetu.

Pamoja na kuwajengea nyumba yenye hadhi na ya kisasa lakini tumehakikisha wazee wetu wanaishi maisha standard kuanzia chakula na mahitaji yote kiasi kwamba familia ya mzee wetu imetazamwa kama familia yenye nafuu pale kijijini.

Juzi ndugu zangu waliopo kijijni wamenitaarifu kwamba kajitokeza mzee anasema anataka kumuoa bi mkubwa. Nikauliza akishamuoa ataondokanae kwa maana bi mkubwa atahama mji tuliomjengea na mzee? Wakaniambia hapana inavyoonyesha huyu mzee kafuata maisha mseleleko.

Binafsi nimejiuliza je ni sahihi mama alete mwanaume kwenye kitanda alicholala na mzee wetu? Je ni kweli nyumba tuliowajengea wazee wetu mama atumie kuishi na mzee mwingine? Alifanyalo mama sio kutufedhehesha sisi watoto tunaohakikisha anapatiwa chochote akitakacho?

Uamuzi wangu nimepanga kuvuruga mpango wa bi mkubwa. Nataka nimwite nimuombe nije niishi nae mjini kwa maisha yake yote ili nizuie mipango yake na akikataa nimepanga sitomuhudumia chochote maana Mimi ndie mwanawe mpendwa.

Je, ndugu uamuzi wangu huu nitakuwa namkosea mama yangu? Au nimwachie tu ahangaike na maisha yake? Kinachoumiza mzee muoaji mwenyewe kachoka mno hata ndala anazovaa ukute zina matundu nusu anagusa ardhi nusu malapa.

Naona kama bi mkubwa atatuongezea mzigo wa kuangalia watu wawili kwa maana akibaki mwenyewe inakuwa rahisi hata kumchukua wakati wowote. Ushauri wenu
Vipi ulifanikiwa kumzuia bi mkubwa au Ndo mpo kwwnye vikao vya harus...
 
Kama mzee anajiweza, aondoke nae kwake na sio nyumbani kwa mama. Kuna mahitaji mengine ya lazima kwa mama ambayo watoto hamuwezi kumtimizia.
 
kuna wajinga wanasapoti huo upuuzi,wakagonganie huko ila siyo kwa baba yangu huyo bi mkubwa wa kuchapwa viboko kabisaaa
 
Back
Top Bottom