Habari ndugu zangu. Naombeni ushauri wenu juu ya mada tajwa.
Mzee wetu amefariki miezi 8 iliyopita baada ya maisha yake yote kuwa katika ndoa na mama yetu. Mama Sasa ana umri wa miaka 68. Kwa kipindi chote tangu sisi watoto wake tuanze kujitegemea tumekuwa tukijitahidi kuwawekea mazingira mazuri ya wazee wetu.
Pamoja na kuwajengea nyumba yenye hadhi na ya kisasa lakini tumehakikisha wazee wetu wanaishi maisha standard kuanzia chakula na mahitaji yote kiasi kwamba familia ya mzee wetu imetazamwa kama familia yenye nafuu pale kijijini.
Juzi ndugu zangu waliopo kijijni wamenitaarifu kwamba kajitokeza mzee anasema anataka kumuoa bi mkubwa. Nikauliza akishamuoa ataondokanae kwa maana bi mkubwa atahama mji tuliomjengea na mzee? Wakaniambia hapana inavyoonyesha huyu mzee kafuata maisha mseleleko.
Binafsi nimejiuliza je ni sahihi mama alete mwanaume kwenye kitanda alicholala na mzee wetu? Je ni kweli nyumba tuliowajengea wazee wetu mama atumie kuishi na mzee mwingine? Alifanyalo mama sio kutufedhehesha sisi watoto tunaohakikisha anapatiwa chochote akitakacho?
Uamuzi wangu nimepanga kuvuruga mpango wa bi mkubwa. Nataka nimwite nimuombe nije niishi nae mjini kwa maisha yake yote ili nizuie mipango yake na akikataa nimepanga sitomuhudumia chochote maana Mimi ndie mwanawe mpendwa.
Je, ndugu uamuzi wangu huu nitakuwa namkosea mama yangu? Au nimwachie tu ahangaike na maisha yake? Kinachoumiza mzee muoaji mwenyewe kachoka mno hata ndala anazovaa ukute zina matundu nusu anagusa ardhi nusu malapa.
Naona kama bi mkubwa atatuongezea mzigo wa kuangalia watu wawili kwa maana akibaki mwenyewe inakuwa rahisi hata kumchukua wakati wowote. Ushauri wenu
Mama yako hana heshima hata kidogo, mzee vile kweli? Mmewe hata hajaoza kashawaza kuolewa? Hapana usikubali hayo mambo kama anataka kuolewa aende kwa huyo mzee na sio mzee aje kwenu.
Baba yangu alifariki akiwa na miaka 30, alimuacha mama akiwa mbichi just miaka 25 trust me mama hakuolewa alitulea na kutusomesha mpaka sasa ni tumekuwa wazima hatukuwahi kumuona mwanaume ndani kwetu .
Mama alikuwa mdogo ana shape matata mrefu, miguu mizuri, yaani kwa ufupi alikuwa mwanamke haswaa lakini hayo yote ya tamaa aliweka chini akajiheshimu na anaheshimika pale nyumbani.
Nilimuuliza kwa nini mama hukuolewa na ulikuwa bado mdogo? Akaniambia baba yenu alinipa maisha mazuri, kuanzia kuvaa, kula kila kitu niliwazidi wanawake wa kijiji hiki.sikuona mwanaume wa kumlinganisha na baba yako.mali aliniachia, watoto aliniachia niolewe kutafuta nini?
Mpaka sasa mama yangu ana nmiaka 50 hatujawahi kuona dalili yeyote ya kuwa na mahusiano, na alitulea kila mara akitusema kuwa tusome na tumpe heshima maana alibaki kwa ajili yetu.
Kijijini kwetu kila mtu umtolea mama mfano linapotokea swala mme wa fulani kafa mke kaolewa ,utasikia wakisema hivi nyie hamumuoni mama luckyline?
Mkuu usikubali ongeoa na mama yako mwambie kama hataki kuja kwako mjini, basi aolewe aende kwa huyo mzee.
Mama yako atawaletea shida, kesho na kesho kutwa mungu kamchukua mama yenu huyo mzee atagomea kwenye hiyo nyumba, mtaanza kuangaika mahakamani, usiruhusu huo ujinga kutokea.