Naombeni ushauri: Nataka kumzuia mama yangu asiolewe tena baada ya baba kufariki

Naombeni ushauri: Nataka kumzuia mama yangu asiolewe tena baada ya baba kufariki

Kuuliza si ujinga ndugu zangu. Endapo wakakubaliana Mama mtu aishi na huyo marioo wake wa uzeeni hapo kwake kwa bahati mbaya huyo Mama akafariki! Huyo Baba wa Kambo ndo atashikilia madaraka Kama Baba wa nyumba au?
 
Miaka 60+ huyo mama yako hana busara kwanini asikitulize kwani kinaoza? Embu mwambie mama yako atulie mmulee
 
Mi nadhani kaa na bi mkubwa,mkubalie aolewe ila wakaanze maisha yao upya mbali na nyumbani kwenu,over

Halafu kwa umri huo bado menstrual circle haijakwisha,bado anawashwa tu,anyway,fuata ushauri huo akigoma basi muachi Mola afanye anachotaka
 
Miaka 68....halafu only 8 month imepita...huyo alikua mchepuko wake..anatelezea hapo sorry to say that...maana km ni stranger mmh ana haraka gani..


Kama ana hamu sana kuolewa aolewe wakakae hukooo kwa mume...
Akija hapo manake mama yako ndo kaoa....
Akakae kwa mume mpya asiwape mzgo
 
Kuuliza si ujinga ndugu zangu. Endapo wakakubaliana Mama mtu aishi na huyo marioo wake wa uzeeni hapo kwake kwa bahati mbaya huyo Mama akafariki! Huyo Baba wa Kambo ndo atashikilia madaraka Kama Baba wa nyumba au?
Nalo neno[emoji16]...yani mzee baba atabaki humo anajitutumua si kwake bana.....


Aah haikubaliki...akakae hukooooo na huyo bwana ake km wanapendana sana
 
Umeongea mengi lakini hapo nilipobold pazingatie sana, kwani huna nafasi ya kumpangia mzee wako vipi Aishi. Vile vile kama mzee (baba) alifariki basi mama yako anao uwezo wa kuja kuishi na huyo mwanaume atakaemuoa kwenye boma lenu kwani hapo mama yako pia ni kwake labda kama apende kuondoka kwake.
Ni kwake alikokua anakaa na mume wake wa zamani...aliyemuoa...
Akiolewa tena akakae kwa mume mpya....
Huyo maza akifariki unataka dingi mpya arithi nyumba...ukoo mwingine kabsaaaa
 
Namshauri Mdau Kama imeshindikana Kumshauri Bi mkubwa asiolewe na huyo Marioo wake.... Fanya umpangishie Nyumba sehemu nyingine wakaishi na huyo Baba yenu mpya. Lipia kodi ya Mwaka mzima halaf mvae huyo Baba ukiwa mwenywe umwambie kodi zinazofuata atalipa mwenywe
 
Mwache aolewe Ila kwa sharti aende akaishi kwa mumewe na huduma zote apewe na mumewe.
 
Kinachomzuia mwanadamu sio umri kwani matamanio hayaishi isipokuwa isipokuwa busara na hekima.......

Moja ya sehemu ya kujitambua mwanadamu ni kuishi kwa kulingana na nyakati na kujitahidi kuyadhibiti matamanio yake...........

Kuna muda kimaumbile unawatamani mabinti lakini ukitazama nyakati na umri unapuuzia na kuhamisha fikra kwenye mambo mengine......

Wale wazee wasiojitambua na kushindwa kuyadhibiti matamanio yao ndio wanakuwa vituko na kichekesho kwenye jamii..........

NB;
Unaochokipigania ni sahihi lakini umekosa hoja ya msingi na yenye nguvu kusimamia maamuzi yako.........

Unaonekana unapingana na uchumi wa huyo muoaji na sio uamuzi wa mama kuolewa.....
 
Angalia huyo Mzee asije akamrubuni Mama na kumuandikishia mali zake kwa jina la huyo mzee,huyo mzee huenda ikawa anatumika tu ili kufanikisha mpango fulani,kuweni makini sana na mali za hapo Nyumbani hasa nyaraka za Nyumba,

Kama Mama ameridhika kuolewa muache tu aolewe ili nae apate mwenza,huenda ikawa anataka kuolewa ili tu ajifariji kwa msiba mzito uliomfika,anatamani nae awe na mtu wa kuongea nae na kumliwaza,

Chunga sana usije ukamkasirisha Mama yako hata kama unamhudumia kwani yeye alikuzaa na pia alikuhudumia,wema wake wa kukuzaa na kukulea huwezi kuulipa hata kama utamuhudumia kwa kiasi gani,jaribu kutumia wazee ili upate ufumbuzi ambao hautaumiza pande zote mbili,

Good luck Brother.
 
Habari ndugu zangu. Naombeni ushauri wenu juu ya mada tajwa.

Mzee wetu amefariki miezi 8 iliyopita baada ya maisha yake yote kuwa katika ndoa na mama yetu. Mama Sasa ana umri wa miaka 68. Kwa kipindi chote tangu sisi watoto wake tuanze kujitegemea tumekuwa tukijitahidi kuwawekea mazingira mazuri ya wazee wetu.

Pamoja na kuwajengea nyumba yenye hadhi na ya kisasa lakini tumehakikisha wazee wetu wanaishi maisha standard kuanzia chakula na mahitaji yote kiasi kwamba familia ya mzee wetu imetazamwa kama familia yenye nafuu pale kijijini.

Juzi ndugu zangu waliopo kijijni wamenitaarifu kwamba kajitokeza mzee anasema anataka kumuoa bi mkubwa. Nikauliza akishamuoa ataondokanae kwa maana bi mkubwa atahama mji tuliomjengea na mzee? Wakaniambia hapana inavyoonyesha huyu mzee kafuata maisha mseleleko.

Binafsi nimejiuliza je ni sahihi mama alete mwanaume kwenye kitanda alicholala na mzee wetu? Je ni kweli nyumba tuliowajengea wazee wetu mama atumie kuishi na mzee mwingine? Alifanyalo mama sio kutufedhehesha sisi watoto tunaohakikisha anapatiwa chochote akitakacho?

Uamuzi wangu nimepanga kuvuruga mpango wa bi mkubwa. Nataka nimwite nimuombe nije niishi nae mjini kwa maisha yake yote ili nizuie mipango yake na akikataa nimepanga sitomuhudumia chochote maana Mimi ndie mwanawe mpendwa.

Je, ndugu uamuzi wangu huu nitakuwa namkosea mama yangu? Au nimwachie tu ahangaike na maisha yake? Kinachoumiza mzee muoaji mwenyewe kachoka mno hata ndala anazovaa ukute zina matundu nusu anagusa ardhi nusu malapa.

Naona kama bi mkubwa atatuongezea mzigo wa kuangalia watu wawili kwa maana akibaki mwenyewe inakuwa rahisi hata kumchukua wakati wowote. Ushauri wenu

Mwache mama aenjoy life ndo hili hili huyo mzee hawezi kugaiwa mali yoyote hapo sababu haimhusu sio mali waliyochuma pamoja..hata ukimchukua kuishi nae mjini hautampa kitu atachotaka..plus usikute huyo baba choka mbaya ndo alikua mpenzi wake enzi za usichana
 
Kinachomzuia mwanadamu sio umri kwani matamanio hayaishi isipokuwa isipokuwa busara na hekima.......

Moja ya sehemu ya kujitambua mwanadamu ni kuishi kwa kulingana na nyakati na kujitahidi kuyadhibiti matamanio yake...........

Kuna muda kimaumbile unawatamani mabinti lakini ukitazama nyakati na umri unapuuzia na kuhamisha fikra kwenye mambo mengine......

Wale wazee wasiojitambua na kushindwa kuyadhibiti matamanio yao ndio wanakuwa vituko na kichekesho kwenye jamii..........

NB;
Unaochokipigania ni sahihi lakini umekosa hoja ya msingi na yenye nguvu kusimamia maamuzi yako.........

Unaonekana unapingana na uchumi wa huyo muoaji na sio uamuzi wa mama kuolewa.....
Hapana uchumi si shida kama wataamua kuishi kwa muoaji. Tatizo naona kama fedheha kwa marehemu baba kama yule mwanaume atahamia pale. Nikiri kwamba kama wataondoka basi nitamuhudumia bila kinyongo. Hata baba zetu wadogo wanapinga boma la kaka yao kutwaliwa na huyo mtu.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo shamte wa mama diamond kamchukua mama diamond kwenye nyumba yake?

Au anaishi kwa mama diamond??

Mtoa maada akijibu hapa basi atapata majibu
Haya yapo inategemea na ustaarabu wa familia. Binafsi mzee katulea ktk maadili na hatukutegemea mazingira ya namna hii. Sijajua huyo Shamte ambae kwako ww ni kioo chako.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Bimkubwa bado anahitahi faraja, usiishie kufikiria kupigwa miti tu

Lakini pia kuna makabila hayakubali kuzeeka yan hadi miaka 80, bado anataka mikasi,
Lakin pia unawezekana utandawazi umemuharibu kwa kiasi chake

Fatalia jambo vizuri na kwa umakini sana


HUU UZI NTAKUJA KUUFUFUA
 
Back
Top Bottom