Naombeni ushauri, nataka nimuache na kumsahau huyu Mwanamke

Umekuwa naye kwa miezi 3 lakini ndani ya huo muda mfupi tayari mna magomvi na kutishiana kuachana...

Hapo hakuna chemistry, acha 'jini mkata kamba' apite tu muachane kwa amani msijefanyiana ubaya...
 
Au afanye biashara ya vyombo vya moto kama pikipiki,bajaji, hiace akiona simu ya dereva tu akili inarejea back to default settings.
Yeah! Ndio ivo mkuu anatakiwa apige kazi za stress tupu aache kuendeshwa na mapenzi ya mama wawili..
 
Ndo shida ya kuonja vya wakubwa.Anza na watoto wenzio,ukikua ndo anza kutubambia ...hutoona ngeni tena.Inayokwamakwama ina utamu wake pia hata kama umezoea KITUO KENDE.
 
Mkuu kuacha nako kunahitaji tukupe mbinu...

Huna msimamo inaonekana,, so hata ukishauriwa bado hutaweza kumuacha..
 
Mimi nakupa haya nilijifunza miaka mingi sana toka brother. Dismas Lyasa ni zaidi ya miaka 10 imepita lakini bado sija ya sahau; sharing is caring. Yachukue haya kama kweli unania thabiti ya kuachana nae:

1. FANYA KILA KITU UNACHOKIPENDA KWA MAZINGATIO, UMAKINI WA HALI YA JUU (ACTIVE FOLLOWS HOBBIES)
-Mfano kazi unayoifanya ifanye kwa umakini wa hali ya juu na tahadhari zote. Ina maana kwamba kama ni muajiriwa basi ukiwa kazini kuwa kazini kweli.

2. PANGA RATIBA ZA MAISHA YA KILA SIKU,
-Kila siku uwe unaorodhesha mambo unayotaka kuyafanya siku inayofuatia. Heshimu ratiba uliyojiwekea hata kama ilikuwa kuangalia mpira simba na mwadui au Yanga na Mlandege FC kuanzia saa kumi mpaka saa 12 jioni basi fanya hivyo. Weka ratiba mpaka ya kulala na kuamka. Kamwe usiingize jambo ambalo litaathiri ratiba yako ya siku nzima.

3. TAFUTA KAMPANI MPYA
-Usiwe mpweke tafuta marafiki wapya wenye nidhamu ya urafiki na wanaelewa nini maana ya urafiki omba akupe kampani kwa kipindi champito, akiwa mwanamke ni bora zaidi. Usisite kuwa muwazi kwamba unahitaji kampani ya kubadilisha mawazo kwa sababu unapitia kipindi kigumu.

4. KUWA MUWAZI KWA WALE UNAOWAAMINI KUHUSU MAAMUZI YAKO ILA USIOMBE USHAURI
-Weleze hisia zako kwa kuhusu huyu kidudu mtu unayetaka kuachana nae mazima na kila zuri ulilomfanyia lakini akashindwa kuelewa. Waombe wakupe sapoti ya faraja na matumaini mengine kwa sababu maisha yanatakiwa kuendelea haijalishi nini kimetokea. ...USIOMBE USHAURI KWA SABABU USHAAMUA KUACHANA NAE...Makinika kuna watu wanajifanya wao wanajua kuliko wewe ujuavyo, believe your intuition.

5. SIKILIZA NYIMBO UNAZOZIPENDA
Muziki ni hisia, na watu huimba kwa hisia. Na hata wasikilizaji pia husikiliza kwa hisia. Sikiliza muziki unaogusa hisia zako

....LEO NI SIKU NYINGINE, KAZI IENDELEE...
 
Aisee.
 
Hii story yako ni kama vile wewe sasa umekuwa ni mtoto wake wa tatu, huyo dada ana watoto watatu rasmi.
Usimuache
 
Misimamo ndio nguzo kila kunapokucha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…