Naombeni ushauri! Nilimsamehe, lakini sasa hanijibu simu wala SMS, nifanyeje?

Nina mpenzi wng ambae tulikuwa tunapendana sana, ni mwanamke ambae amekuwa akinionyesha maana halisi ya upendo wa dhati, amekuwa akinipenda na kuniheshimu sana tu na hatujawahi kugombana tangu tuwe pamoja. Ila siku ya Jumatano iliyopita nilienda kwake, maana huwa kuna wakati anakuja kwangu na mimi naenda kwake.

Sasa nilipokuwa kwake, kuna muda akaenda dukani akawa ameacha simu yake juu ya kochi( Mimi na yeye huwa hatufichani simu, kila mtu anajua password ya mwenzake), basi nikachukua simu yake, huwezi amini katika kuangalia kwenye SMS nikaona kuna namba ambayo haijaseviwa inaishia 32 ilituma SMS inayosema Hivi unablid mwezi mzima?`, daahh nlipata mshtuko hatari maana nlimuamini sana mpenzi wng na sikutegemea kitu kama hicho kwake.

Sasa mpnz wng, aliporudi kutoka dukani, ilibidi tu nimwambie alishtuka sana na akaanza kulia akidai eti huyo mtu hamjui, basi nikamwambia kama unasema humjui basi piga hiyo namba saiv nihakikishe kama humjui, akawa anakwepakwepa bila sababu za msingi baadae akakataa kabisa, huwezi alinifanya nikasirike haswa ila ni kwamba niljizuia tu nisimfanye kitu kibaya.

Baada ya kumtishia na kumbana sana akasema huyo mtu anamfahamu na ni Ex wake alikuwa nae kabla ya kuwa na mimi. Akaniamba msamaha sana akinipigia magoti huku akilia, mimi sikuongea tena kitu bali niliondoka hapo kwake nikiwa sipo sawa kabisa.

Kwa jinsi nilivyokuwa nampenda na mambo mengi mazuri niliyokuwa nimepanga na yeye, na jinsi ambavyo analia kuniomba msamaha, nkafikiria tu kwamba sisi wote ni binadamu hatujakamilika kila mtu ana mapungufu yake., so nikaamua tu kumsamehe na tukaendelea kuwa pamoja huku akiniahidi kutorudia tena.

Ila baada ya kumsamehe zikapita kama siku mbili nikimpigia simu hapokei, nikituma SMS hazijibiwi, ila WhatsApp anaview status zng vizuri tu, sasa hivi ni kama siku tatu zimepita hatuna mawasiliano kabisa, na mimi sasa hivi nimeamua tu kuwa kimya. nashindwa kuelewa mimi nimemkosea nini sas, naombeni ushauri wakuu!!
Blidi imekoma huyo, yupo kwa huyo mwenyewe namba inayoishia 32.

Alishataka kukuacha ila hakujua anakuachaje, kiherehere chako kwenye simu za watu kimempa sababu ya kukutoselea mbali.
 
Mbona swali linaeleweka kabisa Jamani, amerudi kwa mwenye namba inayoishia na 32.
 
Kosa ulilofanya ni kumsamehe yani hapo ashakuona rofa na huna jipya la kumfanya
 
Siku hizi ukinyamaziwa siku 2, ya tatu ikifika wiki ndo umeshaachwa!
Usiendelee kuuliza kosa lako, umia lia endelea na mambo mengine
 
Mwanamke msaliti huwa hasamehewi fukuza kama mbwa

Usije kurudia tena hilo kosa
 
Safi, huyu tutampa kadi mbili za uanachama anaonekana ameelewa sana somo la ijumaa… nashauri aendelee kukukaziaa hivyohivyo mpk uite press conference mkuu🙌🏻
 
Nina mpenzi wng ambae tulikuwa tunapendana sana,
Hapa tayari wewe mwenyewe unakiri mlikuwa. Sasa sio hivo, hampendi sana. SAWA

Sasa nilipokuwa kwake, kuna muda akaenda dukani akawa ameacha simu yake juu ya kochi( Mimi na yeye huwa hatufichani simu, kila mtu anajua password ya mwenzake),
Wewe msukuma sijui msukuma wa wapi unaniangusha kabisa.

Ameenda dukani, anajua unajua password ya simu, kuna sms, kaacha simu

Bado tu haujashtuka huo uliachiwa mtego, uone sms kisha ufanye maamuzi ya kumpiga chini!!!!!!

Alikuwa anashindwa tu kukwambia hakutaki, kakuachia simu usome sms uondoke mwenyewe. SASA NAKUAMBIA KIJANA WANGU HAUTAKIWI. HUYO MWENZIO MWENYE 32 NDIO MAHALI PAKE HAPO, ACHIA NGAZI.

Akaniamba msamaha sana akinipigia magoti huku akilia, mimi sikuongea tena kitu bali niliondoka hapo kwake nikiwa sipo sawa kabisa.
Ilikuwa kuomba msamaha wa kukuzuga tu akijua utakataa na kuondoka. Alijua akikwambia amerudiana na X wake utasusa. Nawe umezuzuka haujajiongeza.

Ila baada ya kumsamehe zikapita kama siku mbili nikimpigia simu hapokei, nikituma SMS hazijibiwi, ila WhatsApp anaview status zng vizuri tu, sasa hivi ni kama siku tatu
Kaona jamaa hujajiongeza kumpiga chini sasa ni bora kazi hiyo aifanye mwenyewe. UMEPIGWA CHINI NGOSHA.

Songa mbele na maisha, acha kuanzishia uzi mademu na K
 
Back
Top Bottom