Naombeni ushauri! Nilimsamehe, lakini sasa hanijibu simu wala SMS, nifanyeje?

Blidi imekoma huyo, yupo kwa huyo mwenyewe namba inayoishia 32.

Alishataka kukuacha ila hakujua anakuachaje, kiherehere chako kwenye simu za watu kimempa sababu ya kukutoselea mbali.
 
Mbona swali linaeleweka kabisa Jamani, amerudi kwa mwenye namba inayoishia na 32.
 
Kosa ulilofanya ni kumsamehe yani hapo ashakuona rofa na huna jipya la kumfanya
 
Siku hizi ukinyamaziwa siku 2, ya tatu ikifika wiki ndo umeshaachwa!
Usiendelee kuuliza kosa lako, umia lia endelea na mambo mengine
 
Mwanamke msaliti huwa hasamehewi fukuza kama mbwa

Usije kurudia tena hilo kosa
 
Safi, huyu tutampa kadi mbili za uanachama anaonekana ameelewa sana somo la ijumaa… nashauri aendelee kukukaziaa hivyohivyo mpk uite press conference mkuu🙌🏻
 
Nina mpenzi wng ambae tulikuwa tunapendana sana,
Hapa tayari wewe mwenyewe unakiri mlikuwa. Sasa sio hivo, hampendi sana. SAWA

Sasa nilipokuwa kwake, kuna muda akaenda dukani akawa ameacha simu yake juu ya kochi( Mimi na yeye huwa hatufichani simu, kila mtu anajua password ya mwenzake),
Wewe msukuma sijui msukuma wa wapi unaniangusha kabisa.

Ameenda dukani, anajua unajua password ya simu, kuna sms, kaacha simu

Bado tu haujashtuka huo uliachiwa mtego, uone sms kisha ufanye maamuzi ya kumpiga chini!!!!!!

Alikuwa anashindwa tu kukwambia hakutaki, kakuachia simu usome sms uondoke mwenyewe. SASA NAKUAMBIA KIJANA WANGU HAUTAKIWI. HUYO MWENZIO MWENYE 32 NDIO MAHALI PAKE HAPO, ACHIA NGAZI.

Akaniamba msamaha sana akinipigia magoti huku akilia, mimi sikuongea tena kitu bali niliondoka hapo kwake nikiwa sipo sawa kabisa.
Ilikuwa kuomba msamaha wa kukuzuga tu akijua utakataa na kuondoka. Alijua akikwambia amerudiana na X wake utasusa. Nawe umezuzuka haujajiongeza.

Ila baada ya kumsamehe zikapita kama siku mbili nikimpigia simu hapokei, nikituma SMS hazijibiwi, ila WhatsApp anaview status zng vizuri tu, sasa hivi ni kama siku tatu
Kaona jamaa hujajiongeza kumpiga chini sasa ni bora kazi hiyo aifanye mwenyewe. UMEPIGWA CHINI NGOSHA.

Songa mbele na maisha, acha kuanzishia uzi mademu na K
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…