Naombeni ushauri nimemfumania shemeji yangu

Umeongea vyema mkuu shukrani nitajitahidi Sana kulea uovu nashindwa abadani[emoji17]
 
Binafsi huwa naona SI SAWA KUMWAMBIA MWENZA BAADA YA KUMFUMA MWINGINE.. Kama kweli unataka kujenga, mwambie huyu shemeji yako kuwa anayoyafanya siyo, na aache Mara moj...!! Najua huyo shemeji anaweza kukusingizia jambo kwa jamaa, wewe tunza ushahidi...!! Hasa kwamba unamtaka kimapenzi

Ila kwa upande mwingine, jiandae kuvunja urafiki wenu.
 

Chukua hizo evidence umtumie huyo shemeji yako (mwanamke) usiandike chochote zaidi ya evidence.

Alafu ukaushe kimya. Rafiki yako usimtumie kwanza. Mwanake atafunguka tu. Na wala usimwambie mwanamke kwamba hukusudii kumpa taarifa mumewe
 
Nitumie mimi hizo picha na video za shemeji yako kisha nicheki na namba ya rafiki yako ntakusaidia kufikisha ujumbe bila ya wewe kujulikana....hahaaaaa natania tu mkuu.

Mi nakushauri tafuta namna ya kumwambia huyo rafikiyo.Kukaa kimya baada ya kujua yote hayo ni usaliti kwa urafiki wenu.
 
Malaya malaya tu

Km rafiki yako aliuziwa madeni mbuzi kwenye gunia ujue hata reasoning yake ipo chini

Rafiki yako atapata ukimwi kwa ujinga wake wa kuokota wanawake hovyo

Tafuta line mpya mpe evidence zote ila asijue km ni wewe

Ukimpenda mtu unamlinda kwangu mimi ni bora nipewe ukweli nitajua rafiki ninaye kuliko nijue mwenyewe hlf uje kusema ulikuwa unajua.

Mi sijawahi kuogopa tatizo hlf sijawahi kupenda unafiki.

Kuna zile case za mtu amuacha mwanamke baada yakudumu nae miaka 40 ndoanihlf akagundua walipokuwa na miaka 15 ya ndoa mkewe alimsaliti basi haba tofauti na mimi.
 

Mwisho kabisa, kama kweli huyo ni rafiki yako, lazima umwambie ajue maana kusema amchunguze mkewe wakati una idea ya kinachoendelea bado hujamsaidia.

Rafiki yako mwambie ukweli ajue kinachoendelea. Usipomuambia akigundua kwamba taarifa ulikuwa nayo ila ulimbania ndo urafiki utaishia hapo kwasababu huna msaada kwake. Tell him
 
Waliposema ndoa iheshimiwe na watu wote hawakua na maana ndoa ya mwanamke mmoja na wanaume wawili , ndoa ilisha vunjika siku nyingi ambae hajui ni rafiki yako hivyo mtaarifu tu, mtumie hiyo video hata kwa mail mpya ya kutengeneza
 
Je nikimwambia kwa njia ya simu Ina Afya au nionane naye ana kwa ana....???
Maana kwa Sasa nipo mbali naye kwa Maana ya distance.

Wewe tumia muda mrefu mpigie simu kamanda muulize kwa mapana juu ya welfare yake na ndoa kiujumla, na muulize kwa upana maisha ya ndoa anayaonaje, nje na makwazo yale ya madeni ya mwanzo je kwa sasa yukoje? Ana changamoto zozote kwa sasa? Mpongeze kwa kuoa, kama hujaoa mwambie unatamani ndoa pia, mdodose kuhusu any joint projects kati yake na mkewe zilizopo na tarajiwa, uliza kwa kiasi gani mkewe ni mshirika na msiri wake wa karibu wa kimaendeleo taarifa za kibenki, mashamba, nyumba, viwanja, biashara etc.
Kisha namna nzuri kwa baadae ikihitajika taarifa na videos na picha usitoe wewe mtumie baharia mwingine kbsa.

Mpime kwenye mastori yenu kama mwamba ana kifua ama kaba ya kiume.

Kuchapiwa si sehemu ya kubebeana kwenye maisha ya ndoa.
 
Mambo ya ndoa humalizwa na wanandoa, usiingilie ndoa yao, utajiweka katikati ya migogoro bila sababu yoyote na mwisho wake kupoteza hata urafiki !
Acha ujinga wewe,mitaani kote wanawake wanapofanya ujinga wao pasipo wanaume zao kujua lakini badaye huja kugundua kupitia majirani na watu wa karibu.
Huyo Jamaa anatakiwa amwambie ni kitu kibaya sana mwanamke kuchepuka,kibaya zaidi ya kibaya.
 
utakapomtumia video au picha atasema hizo picha ni za zamani!!alipokuwa na x wake!

embu endelea kupata ushauri humu labda unaweza kupata solution.
lakini never let this go undone!
muokoe msela inaonyesha ameshikwa maskio sana.
 
Kuna jamaa walikuwa wanajua ya kwamba shemeji yao anamegwa na njemba fulani kutokana na urafiki wao wakawa wanumia sana wakamwambia muhusika na wakandaa mtego, cku ya cku muhusika akapigiwa cm mkeo agawa uroda njoo ushuhudie huku jamaa akafika chap kwa haraka, wakamwambia subili hapa maana wameingia gest, wakasubili muda wakawaona wanatoka huku wamekumbatia basi kwa kuwa ilikuwa ucku jamaa akawa anawafuatilia kwa nyuma bila wao kujua, kufika mbele wakasimama wakiongea mwanamke akasema ngoja nimuwai huyu bwege atakuwa amesharudi jamaa kusikia vile uzalendo ukamshinda akamchoma kisu mwanamme na kufa pale pale, mwisho mwanamme amefunga mgoni amekufa mwanamke ameolewa tena hukoooooooooooooooooooooooooo, marafiki wanajuta kwa walichokifanya.
 
Screenshot picha na what sap messages halafu mtumie.Kisha omba muda umuelezee ishu nzima,mwanamke Malaya si wa kumfichia mambo yake ni hatari kwa rafiki yako.
 
aise vunga tu,kunguru hafugiki ipo siku rafiki yako atajionea mwenyewe,haiingii akilini kama tayari wana ndoa na bado anapostiwa kwenye group za wasap,kumwambia rafikio ni kuuweka urafiki wenu mashakani asilimia ya kuendelea kuwa marafiki endapo utamwambia ni 1 tu mapenzi ni zaidi ya ukichaa...wacha na wala usithubutu kumwambia kama bado unahitaji kuendeleza urafiki wenu...ipo siku atajua na usishangae wewe unaweza kumwambia kumbe mwenzako anajua siku nyingi ila ameamua kukubaliana na matokeo
 
Kama mwenye ndoa kashindwa kuiheshimu wewe Baki utaweza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…