Naombeni ushauri nimemfumania shemeji yangu

Nimeaoma huu uzi ila nimeshindwa tambua wewe ni mwanaume au mwanamke
 
nakazia tu fuata hii maneno
 
Tafuta admin au mtu yoyote amuunganishe katika Hilo kundi la whatsaap then wewe nitoe kwa siku chache kama mbili Tatu hivi halafu hizo picha azione basi hapo jamaa atajua kila kitu na baadae atolewe na wewe urudi. Hatajua kama wewe ni mhusika ila atajua yote na ushahidi. Mke hapo atajua afanye nini
good idear fanya hivyo boss
 
Achana na wazo la kumuambia maana utasababisha ndoa kuvunjika kitu ambacho si kizuri. Kama hizo picha kwenye group unazo unaweza kutafuta njia jamaa azione hata kwa kumtumia kwa namba ambayo si yako ili ajue bila wewe kujulikana

Ogopa sana kuwa chanzo cha migigoro katika ndoa za watu maana wakisameheana utashindwa kuwaangalia usoni na wakiachana pia utashindwa kuwaangalia usoni
 
Mpe Mkanda Mzima, A to Z.

Kama unaona inaweza kuvunja urafiki wenu, basi tafuta namna ya kumfikishia ujumbe pasipo yeye kujua kuwa umetoka kwako.

Otherwise unamwita unamwambia kile unachofahamu, na inawezekana ukamwambia na asimwache mkewe, akamkanya tu kisha wakaendelea na ndoa yao, sio uwe teyare kupokea hilo.
 
J

Je, ingekuwa wewe mwanaume unayafanya hayo, mkeo aelezwe ili ukamatwe?
Aelezwe tu mkuu. Mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu mchungu. Sisi tumeshawahi kumshusha mchepuko wa mjomba tukiwa safarini. Tulikuwa tunaenda kwenye msiba, uncle alipewa gari na ofisi kwa ajili ya kubeba ndugu na jamaa njiani tukagundua mmoja kati ya marafiki zake waliopanda ni mchepuko wake. Aisee, hawatasahau ile siku. Walisemwa mno na binti akashushwa kwenye moja ya miji tuliyopita njiani.

Kuna familia zinathamini na kuheshimu sana ndoa, ikisikika unafanya upuuzi utatamani uhame ukoo. Haijajilishi una status gani hiyo ndo nidhamu tuliyojiwekea
 

Hata mie hapo sitii neno, mambo ya watu wanaojifunika shuka moja mazito sana, sio ya kuyaendea pupa.

Unaweza kutema nyongo, kesho unawakuta wako wote wanaendelea na maisha yao, unajificha wapi hapo?

Wayamalize wenyewe tu! Kwanza siku hizi watu wanauana na matukio kibao.
 
Hamna ugumu wowote tena hayakuhusu tena usitake kuharibu urafiki wenu, kama mwanaume anaakili timamu basi angeshastuka yaani mtu alouza kiwanja kuclear mkopo wa mpenzi,?,,,unahangaika naye wa nini
Narudia hayakuhusu,utakuja kunishukuru badae
 
Mkuu si usajili line kwa jina tofauti umwambie Huo jamaa yako hatajua
kama ni wewe utajifanya ni msamaria mwema then unamtumia na hiyo evidence ya picha,maana Huyo jamaa yako soon atalea ukimwi ama watoto Wa jamaa mwingine atalea.

Roho itakusuta maana ukweli unaujua na humwambii,Malaya sio Wa kulea.
 
Nduuu

Hayakuhusu

Maana inategemea na akili ya rafiki yako


La sivyo achana na kuongeza idadi ya maadui duniani
 
Hapa no kona kona,chap chap mchane jamaa,mambo yenu haya ya kuanza kuhofia hofia mtu anapelekewa magonjwa unaona,ndoa saivi hazina tena uzito ule😀,mwambie fasta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…