Naombeni ushauri nimemfumania shemeji yangu

Mwanaume rafiki yake ni Mwanaume mwenzake, Huyo kiumbe unayemzungumzia ni Mungu pekee ndo anaweza kuishi nae
 
Wewe mwambie jamaa yako, au unataka siku umpelekee machungwa na matunda mengine ya kukuza afya akiathirika.....

Alafu vipi kama mke wake anampango wa kumuua jamaa yako akaishi na huyo mchepuko?

Vipi kama mke ampe watoto 5 jamaa wasio wakwake utajisikia vipi, wakati ukweli wote wa kumuokoa ulikuwa nao

au utajisilia vipi mke akimuiniza jamaa tena mkenge akasema anadaiwa mil 15++ akaenda mpa huyo mchepuko

Biblia inasema mwanamke msaliti hapaswi kuishi, tuishi humo
 
Hebu kwanza hizo videos tuzione
 
Kama unaushahidi..nunua flashi..rekodi..mtume mtu asiemjua..ampe..alafu kaa kimya. Akiona yeye..ataaamua lililo sahihi..na wewe hutakuwa na lawama. Na hapo untakuwa umeiweka huru nafsi yako kuliko uivyo sasa.
 
Tafuta namna ya kumwambia uokoe roho yake, uokoe mwili wake,uokoe maisha yake.
Maradhi ni mengi mno, ukimwi umetapakaa mno ni maumivu sana kusalitiwa, tafuta namna ya kumuokoa iwe tu indirect way hata direct way ikibidi, tulipofikia hakuna aliye salama ukimwi hauchagui.
Brother wangu aliambiwa sana mkewe anasaliti, hakuamini na akapuuza lakini leo hii na mke wote ni HIV+...inaumiza sana.
Sijaoa lakini huwa nawaambia rafiki zangu ikitokea umemuona mchumba yupo na mtu niambie, ili uokoe maisha yangu palipofikia tusioneane aibu[emoji846]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 

Achana na ushauri wa watanzania, eti, usimwambie, utaharibu ndoa. Sasa ndoa ikiharibika kuna shida gani? Mimi nakerwa sana na tabia hii ya watanzania. Unaweza usiseme leo, kesho akafahamu, na akaja kujua ulijua hukumwambia. Au akajua mwenyewe bila utaratibu akapaniki akambanika huyo dada. Kumbe ukitumia busara unaweza kuokoa yote haya.

Hapo cha msingi ni kutumia busara ya hali ya juu kumjuza jamaa yako. Kwanza, ni lazima uwe umejiridhisha na suala hili, pili hakikisha una ushahidi mujarab. Kuna namna nyingi ya kumfikishia taarifa, usikurupuke. Tumia viongozi wa dini, wenye busara, siyo hawa wanaokataa chanjo, eti, wameoteshwa. Kama ulivyosema kuwa mmeshibana na rafiki yako,basi pia huenda kuna watu wazima waliowazidi umri, watumie hao.

Hii usijali hata kama urafiki wenu utayumba. Utakuwa umewatendea haki hao wanandoa, watoto wao (kama wanao), familia yako na yao na jamii nzima ya watanzania. Kama haitoshi, hata peponi utakaa kiti cha mbele kabisa kama wale abiria VIP wa BM Coach.

Tujifunze kukabili ukweli hata kama unauma
 
Eti group la ndoa? Nonsense.

Litakuwa group la wazinzi tu.

Na wewe ukiwemo. So kausha acha wivu huko totoz hata wewe unamtaka.
 
Mwanamke msaliti sio wakumvungia mwambie jamaa ako ukweli.

Jamaaa anajibana alafu limwanamke linaenda kugawa na mapicha juu??
 

Najua upo kwenye mtihani mkubwa mno ndugu yangu. Linapokuja suala la kujihusisha na mahusiano ya watu huwa jambo zito sana.

Nakumbuka miaka mitatu iliyopita nilirudi nyumbani kutoka kwenye pirika zangu ikiwa yapata majira ya saa nne usiku. Bahati mbaya sikutoka na funguo ya geti hivyo ilinilazimu kumpigia mama simu anifungulie geti, simu iliita muda mrefu bila mafanikio. Nikiwa kwenye zoezi la kuendelea kumpigia mama simu alifungulie geti. Nilimuona mke wa bro wangu wa kitaa akiingizwa kwenye geti la jirani na shamba boy wa hiyo nyumba. Ukweli nilipigwa na bumbuwazi nisiamini nilichokiona huku nikijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu juu ya kitendo kile.
Ukweli nilimpigia simu bro nisamlimu kwa kuwa sikuonana naye kwa muda wa siku kadhaa. Alipokea simu tukasalimiana na kuniuliza kama nipo dukani kwa bwashee ambapo huwa mara nyingi tunakutana na kupiga story mbili tatu na kugonga mvinyo. Nilimwambia nipo hapa home nje nilikuwa nampigia simu mama anifungulie geti lakini simu yake inaita tu. Alichoniambia nilichoka, aliniambia anamsubiri mke wake arudi kutoka kununua maziwa ili aende dukani kwa bwashee akapige stori na jamaa.

Unaona sasa, “Mme anajua mke amefata maziwa dukani, na kumbe alienda kupewa cha fasta na shamba boi”. Ukweli sikuthubutu kumwambie bro kile nilichokiona kuhofia kusababisha migogoro baina yao. Na nikiwa nimesimama pale nje haikuchukua hata dakika 15 shemeji akatolewa mle ndani na kurudi kwake.

Hivyo kuna wakati unakuwa njia panda linapokuja suala la mahusiano ya watu.
 
Wazo zuri Sana. Nami nilifikiria hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…