Naombeni ushauri ninunue flash gani nzuri kwenye maduka kati ya kioxera, toshoba, sandisk, n.k. ntajuaje ni feki?

gearbox

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2024
Posts
563
Reaction score
1,768
Habari zenu wakuu, nina uhitaji wa flash disk.

Wala sina mpango wa kuagiza nje ni emergency hivyo itabidi ninunue madukani, nipo mkoani brand zinazotamba ni Kioxera, Toshiba, Imation, Sandisk, n.k. ama unaweza kuongeza zako unazoziaona madukani






 
Sijajua hizo brand nyingine, lakini hiyo kioxera ni sawa na card reader. Ndani wameweka memory card ila inapiga kazi fresh tu
 
Kioxia ndio Toshiba, brand zote ulizo taja ni OG ila kuna asilimia 99% imetengenezwa China na ikabandikwa tu hio brand. Maduka yetu siku hizi yamejaa vitu feki tu.

Cha muhimu angalia speed ya flash husika, kama una file kubwa hamishia kwenye flash uone speed inasomaje, kama ni konokono 10mbps kushuka mchina kimeo, kama inapiga 20-40mbps kupanda angalau kidogo.

Ideal flash za kisasa ni usb 3 na zinahamisha mania ya mb kwa sekunde ila nadra kuzikuta huku kwetu.
 
Hua naona kwenye youtube flash zina speed ila kwa hizi flash zetu za bongo sijawai kuona inayofika 10 MB kwa sekunde, labda kwenye 5 hadi 7
 
Kuna flash inafikia 40mbps? Duh bc mm mshamba sana aisee
 
Mkuu chukua sandisk hawa wengine ni ngumu kupata Og yake japo hata sandisk lazima ujue kuangalia nazo zipo famba.. unapo nunu angalia kwa kuchungulia kwenye tobo la kuchomeka ukiona zile terminal zipo mundo wa round shape hiyo ni famba ila kama zipo square bebaa..
 
Kuna flash inafikia 40mbps? Duh bc mm mshamba sana aisee

Kuna flash inafikia 40mbps? Duh bc mm mshamba sana aisee
Mbona 40MBps ndogo sana zipo hadi za GBps, rahisi sana kuweka SSD ama related technology kwenye flash, ukiangalia masoko ya nje hizi flash zina speed mno na bei zake zipo chini, its just wafanyabiashara wetu Na wateja wanauza na kununua kwa mazoea huku.
 
Mkuu nyingi zipo sealed, utawezaje kutest?!
 
Hapo Kuna speed na size ya flash,
Wachina wanatweak flash ya GB 4 isome GB32++ kwahiyo itapokea files za GB 32 lakini GB zilizobaki ukijaza file zinacorrupt, ukinunua flash jaza file kulingana na flash then watch speed, kama sped ipo ok na files zote zinasoma you're ready to go.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…