Assalamualaikum,
Naombeni ushauri ninunue friza la kampuni gani kwa ajili ya biashara ya soft drinks na maji kwenye duka la rejareja.
BEKO: Zimekuwa designed kula umeme mdogo sana na kutunza baridi muda mrefu sana baada ya kuzima hasa usipofungua fungua. Downside halifanyi kazi vizuri kipindi cha joto kali pia kwa freezers zinakuja bila compressor fan, kipindi cha joto unaweza kufunga kuongeza ufanisi, kipindi cha hali ya hewa nzuriutalipenda sana na bei yake ya kawaida.
West Point: Zuri sana kwa ufanyaji kazi na energy saving, bei zake zimechangamka kidogo. Nadhani kwa freezers ndio zuri zaidi kwa haya yanayokuja kwa wingi nchini.
Delta: Sikushauri, umeme unaenda na ufanisi sio mzuri sana.
Hisense: Classic na bei imechangamka, unaweza kukuta appliance ni kubwa lakini ikachukua umeme kidogo na ufanisi mzuri. Mara nyingi fridge/freezer ujazo ukiwa mkubwa huchukua muda kugandisha.
Bosch: Hayapatikani sana nchini, ni bora kuliko yote kwenye list hii. Ukilipata hata la mtumba beba, alianza kutumia energy saving zamani. Bei imechangamka.
Mo electric: Sijui kafanyaje lakini ameweza, bei ya mtanzania.
Bruhm: Kwa freezer ukiweka vitu vingi vipya visivyo na ubaridi, compressor inafeli. Unasort kwa kuweka extra compressor fan pia usiliweke sehemu palipojibana sana, compressor inahitaji sana hewa.
Von: Yuko vizuri sana