Naombeni ushauri nipo njia panda

achieni wazazi wa pande mbili wayamalize kwa amani
 
1) Kwanza Kabisa hilo la ukabila futa kabisa,kwani kama asingekuwa appreciated kwako asingefunga Safari mpk huko kwenu kuja kutoa MAHARI.
2)Kutokana maelezo yako uliondoka mwenyewe bila kufukuzwa kwa TABIA ZAKO ZA KIBURI CHA KWENU huko UBENANI,.
3) Kwa maelezo inaonekana wewe ujafundwa kimaadili ya kuishi na mume,ss kama umepewa zaidi ya mtoto mzuri mlele vizuri asiwe na tabia kama zako,stp.
4)Unijui sikijui kama na kiburi chako, TAKE IT TO THE BANK,
 
@trudie
 
Dada kubali ushakuwa single mother. Mimi mama angu alikuwa single mother kwa wadogo zangu na naona walivyo walivyo hata kujiamini amini hawajiamini kama ni ndugu zetu. Yani hata likitokea tukio la kofamilia tukijumuika unaona wao wanajitenga tenga. Ni kama hawana confidence na sisi, ni kama hawampend baba na mashangazi. Yani maneno ya mama juu ya baba na mawifi zake (mashangazi) yamewajengea chuki watoto.

Huu ni upuuzi wa ma single mother. Stress zako unazimalizia kwa watoto. Matokeo yake nao wanakua na msongo wa mawazo kutoka kwako. Upompompo wako uliokufanya utemwe na mumeo hutakiwi kuubadili na kuwalisha wanao
 
Huyu anaonekana alidanganywa na wazazi wake ndo wanamdekeza.

Wazazi washamharibia bila yeye kujua. Nimegundua tatizo lilipo
 
Wabena awako hivyo mm nilumtolea mke wangu mahali nikaishi nae miaka 11 then mwaka wa 12 ndo nikamuoa ndoa ya kanisani tena hapo nishamzalisha watoto 6 kamili ukitolewa mahali ww ni mke wa mtu na mahali hairudishwi tulia....
 
Kwa kuwa ushatolewa mahari, na ikakubaliwa, wewe ushakuwa mke wa mtu.
Ndugu wanaweza kupinga ila ukiachwa utasemwa pia.
 
Dah baada ya kupita kule kwenye uzi wako mwingine.

Natamani sababu ya ninyi kuachana isiwe uliondoka ukamuacha huyu jamaa maana itakuwa haukuplay fair pia.
 
Hapo kinachowauma wazazi ni michango waliochangia kwenye harusi za majirani nao wanataka michango na zawadi +heshima ila Hadi hapo kama mahali imetolewa ww ni mke wa mtu bila kupepesa macho.tulia mpange maisha na namna ya kumlea mtoto wenu mpendwa a.k.a first born

Sent from my RMX2189 using JamiiForums mobile app
 
Inaonesha tayari ulikuwa na misimamo yako..bila shaka mlitengana
 
Vipi mrejesho mlishafunga ndoa?

Mahari sio ndoa,sheria haitambui hio
 
Aaah kwa upande wangu wazazi wako walikua sahihi. Ndoa tamu ni ile yenye heshima zote na sio ya kuogopa kubaki single mom na kutiahiana. Hope kwa wakati huu unaishi kwa amani
Hapana mkuu hatukufunga ndoa, baada ya muda kila mtu aliendelea na maisha yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…