Naombeni ushauri wa busara, amemfukuza mke wake kwa sababu yangu

kingkongtz

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2019
Posts
1,058
Reaction score
3,613
Wakuu kwema,

kama mada inavyojieleza, hapa nipo njia panda nakosa la kufanya,naamin ntapata maoni kupitia nyinyi.

Labda niwaeleze kisa na mkasa mpaka kufikia hatua ya kupandisha uzi usiku huu.

Nina rafiki ambaye tulitokea kuwa marafiki na kilichotukutanisha ni kazi tuliyokuwa tukifanya sehemu moja (kampuni moja), nadhan ni moja ya marafiki ambao tuliaminiana kwa mengi sana na tumekuwa tukishirikiana katika mambo kadha wa kadha (nampa big up sana hana roho mbaya) kiumri ananizidi mbali,yeye ana mke na mtoto.

Kadiri siku zilivyozidi kwenda alinitambulisha kwa mkewake so tukawa kama ndugu sasa huku mm nikimwita mkewake shemeji.

Wakati tukiendelea na kazi jamaa ilibidi amfanyie mchongo mkewake naye akapata kazi hapo hapo tukaendelea kusukuma gurudumu. tatzo lilianza mkewake alitengeneza mazoea ya ghafla na mm ,ule u-shem shem na kumisiwa kukawa kwingi, japokuw nilijitahid kumkwepa lkn alikaza mwishowe jamaa nafikir aliusoma mchezo mzima

Upesi upesi jamaa kapunguza ule ukaribu yaan yale mazoea hataki tena, sikutaka hata kuuliza mimi pia nikala kmya, sasa kwa upande wake akahisi ni kweli namchapia mkewe.

Sasa juzi mwamba hakufika kazini wala kakutoa taarifa yoyote, alikuja mkewake tu na wafanya kaz wengne kwa mbali nikawasikia waliokuw pembeni wakidai jamaa anaumwa,

Kumbuka wakati huo mi sina mazoea na shemej zaidi ya yeye kunichangamkia tu.

Muda wa kurudi home naona text

No ngeni "mamb"
Mimi safi habari
No ngen. nzur 2

Nikaipotezea, dakika chache simu inaita namba ileile akajitambulisha na akanipa habari za mumewe kuugua bas nikawapa pole yao na maongezi yakaishia hapo

Nafika nyumbani text tena inaingia

No ngeni (ile ile)
"ila shem huwa nakumic sana ni bas tu usinifikirie vibaya jamani"
Mimi."shem tulia na mme wako" yeye."hata kama ila mi nakupenda tambua hilo'

Sikujibu tena kwanza nilihisi wapo wote wananiigizia kwanza namba kaipata wap.

Ndugu zangu ile meseji kwanza ilitisha nikahisi ni mtego so nikaichunia nikaendelea na masuala mengne hata yy kakunichek tena

Sasa jana nimekaa zangu home naona mwamba huyu hapa na mkewake,aisee hata kabla sijawakaribisha mwamba kaniporomoshea matusi ya nguoni huku mwanamke analia.

Cha kushangaza zaidi akanambia "kwa kuwa mnapendana nimeamua kukuletea kabsa furahini sasa" kisha jamaa huyo akaondoka speed kwa mbaaali namsikia akimshukuru kwa kumzalia tu mtoto.

Huyu shemej akanipa mkasa sasa aisee kwanza nilihuzunika kumbe zile sms alifuta zikabak kwenye recycle bin (wazee wa Samsung) alijisahau na mme wake akazifuma kule kule

Sasa wazee nipo njia panda mwanamke kakimbilia kwa rafik yake ,kule jamaa nae sijui ananifikiria nn na mm natafuta njia ya kumuaminisha kuwa sikuwa wala sina mahusiano na mkewake,

Naombeni ushauri juu ya hili
 
Wanawake nao wanazingua sana. Kupenda huwa hakuishi ila ni namna ya kuridhika na kushinda majaribu
Wala usihangaike na chochote wala kumtext tena huyo mwanamke. Endelea na maisha yako, hii ndiyo mojawapo ya kudhihirisha kuwa hukuwa na mawasiliano naye.
 
Kwah
Wakuu kwema,

kama mada inavyojieleza, hapa nipo njia panda nakosa la kufanya,naamin ntapata maoni kupitia nyinyi.

Labda niwaeleze kisa na mkasa mpaka kufikia hatua ya kupandisha uzi usiku huu.

Nina rafiki ambaye tulitokea kuwa marafiki na kilichotukutanisha ni kazi tuliyokuwa tukifanya sehemu moja (kampuni moja), nadhan ni moja ya marafiki ambao tuliaminiana kwa mengi sana na tumekuwa tukishirikiana katika mambo kadha wa kadha (nampa big up sana hana roho mbaya) kiumri ananizidi mbali,yeye ana mke na mtoto.

Kadiri siku zilivyozidi kwenda alinitambulisha kwa mkewake so tukawa kama ndugu sasa huku mm nikimwita mkewake shemeji.

Wakati tukiendelea na kazi jamaa ilibidi amfanyie mchongo mkewake naye akapata kazi hapo hapo tukaendelea kusukuma gurudumu. tatzo lilianza mkewake alitengeneza mazoea ya ghafla na mm ,ule u-shem shem na kumisiwa kukawa kwingi, japokuw nilijitahid kumkwepa lkn alikaza mwishowe jamaa nafikir aliusoma mchezo mzima

Upesi upesi jamaa kapunguza ule ukaribu yaan yale mazoea hataki tena, sikutaka hata kuuliza mimi pia nikala kmya, sasa kwa upande wake akahisi ni kweli namchapia mkewe.

Sasa juzi mwamba hakufika kazini wala kakutoa taarifa yoyote, alikuja mkewake tu na wafanya kaz wengne kwa mbali nikawasikia waliokuw pembeni wakidai jamaa anaumwa,

Kumbuka wakati huo mi sina mazoea na shemej zaidi ya yeye kunichangamkia tu.

Muda wa kurudi home naona text

No ngeni "mamb"
Mimi safi habari
No ngen. nzur 2

Nikaipotezea, dakika chache simu inaita namba ileile akajitambulisha na akanipa habari za mumewe kuugua bas nikawapa pole yao na maongezi yakaishia hapo

Nafika nyumbani text tena inaingia

No ngeni (ile ile)
"ila shem huwa nakumic sana ni bas tu usinifikirie vibaya jamani"
Mimi."shem tulia na mme wako" yeye."hata kama ila mi nakupenda tambua hilo'

Sikujibu tena kwanza nilihisi wapo wote wananiigizia kwanza namba kaipata wap.

Ndugu zangu ile meseji kwanza ilitisha nikahisi ni mtego so nikaichunia nikaendelea na masuala mengne hata yy kakunichek tena

Sasa jana nimekaa zangu home naona mwamba huyu hapa na mkewake,aisee hata kabla sijawakaribisha mwamba kaniporomoshea matusi ya nguoni huku mwanamke analia.

Cha kushangaza zaidi akanambia "kwa kuwa mnapendana nimeamua kukuletea kabsa furahini sasa" kisha jamaa huyo akaondoka speed kwa mbaaali namsikia akimshukuru kwa kumzalia tu mtoto.

Huyu shemej akanipa mkasa sasa aisee kwanza nilihuzunika kumbe zile sms alifuta zikabak kwenye recycle bin (wazee wa Samsung) alijisahau na mme wake akazifuma kule kule

Sasa wazee nipo njia panda mwanamke kakimbilia kwa rafik yake ,kule jamaa nae sijui ananifikiria nn na mm natafuta njia ya kumuaminisha kuwa sikuwa wala sina mahusiano na mkewake,

Naombeni ushauri juu ya
Kwahiyo mke wake upo naye muda huu wa usiku wa sasa saba???
 
Kosa ulifanya tangu siku ya kwanza ulipo ona analeta mazoea ukakaa kimya, fasta sana ulitakiwa kumjulisha jamaa na vile umekiri ni marafiki mlioshibana hata haya yasingefika huko, tatizo vijana mnajiona vijogoo mkishobokewa, mtakuja kupigwa shoka la kichwa.
 
Huyu rafiki yako hajiamini au wewe hujatueleza yote, hizo message km kumtuhumu zote zinamshitaki mwanamke na sio wewe, unless alizifuma messages zako ukimjibu huyo mwanamke km unampenda. Otherwise kama uli mute kama unavyosema huyo rafiki yako asingesema amewaacha kwa kuwa mnapendana na kuwasusa wote mana messages zinamshtumu mkewe zaidi. Sema usaidiwe kijana...
 
ulikosea kukaa kimya kwenye meseji alipokuambia anakupenda, kimya kinaleta makadirio kwamba hujastushwa tayari mpo kwenye mahusiano ama mlihamishia mawasiliano kwenye simu za siri.

ilibidi umjibu kumkataa kabisa huku ukishinikiza yeye ni mke wa rafiki yako na umesikitishwa kwa usaliti anaotaka kumfanyia rafiki yako pamoja na kuweka urafiki wenu hatarini.
 
Hujaeleza story yote inaonekana, ila unaonekana na wewe uliendekeza mazoea na mke wa jamaa, kama ni jamaa yako na unajali urafiki wenu, jaribu kumuita mkae chini umueleze ukweli na umuhakikishie hakuna kitu anachofikiria na unamuheshimu sana, akikataa nawa mikono and move on
 
Kuna kitu unaficha kwenye hiyo convo, weka wazi haiwezekani kwa hizo sms 4 tu iwe hivyo mkuu na kama ni hivyo basi huyo jamaa yako ni kisusio, anajua kususa sana.

Katika kitu huwa sitaki ni mazoea na mashemeji zangu, huwa siruhusu ukaribu wa aina yeyote ule. Na huwa nawaambia kabisa jamaa zangu tusitiane majaribuni.
 
H
Huyu rafiki yako hajiamini au wewe hujatueleza yote, hizo message km kumtuhumu zote zinamshitaki mwanamke na sio wewe, unless alizifuma messages zako ukimjibu huyo mwanamke km unampenda. Otherwise kama uli mute kama unavyosema huyo rafiki yako asingesema amewaacha kwa kuwa mnapendana na kuwasusa wote mana messages zinamshtumu mkewe zaidi. Sema usaidiwe kijana...
Hii habari iko nusu.. jMaa hataki kuonyesha yeye amechocheaje maamuzi ya kususiwa mke. Sms one tu ususiwe mke, kweli? Lamomy hii inaingia akilin kweli?
 
Hayo ni Yao Wala yasikusumbue matatizo mengine ni kufanya kama huyaoni mda utaamua
Usitafute kuonesha huhusiki we ignore endelea na maisha ila note this isije siku Moja kwamba hawajarudiana kabisa basi ukamla huyo mwanamke kwa kusema hawako tena pamoja hapo utakuwa umeharibu kabisa
 
Kijana acha mazoea na wake za watu,huwa mimi sina, mazoea na wake za watu hadi wake wa kaka zangu,kipindi nipo mkoa niliozaliwa nikienda nyumbani kwa kaka yangu yeoyote yule,shem ananishangaa anajua huyu jamaa kaja leo home basi kuna kitu kaagizwa na kweli ntaenda nikiagizwa kitu. Kwenye nyumba za kupanga ndio kabisa sitaki mazoea. Ila ulikosea kukaa kimya ulikuwa unatunza bomu linalotaka kulipuka ingawa kuna midume mingine ukiiambia ukweli haiamini unakimbilia kumwambia mkewe. Kuna jamaa niliwahi kumwambia kuwa mkeo ananichukia sikutaka kumficha
 
Back
Top Bottom