Naombeni ushauri wa busara, amemfukuza mke wake kwa sababu yangu

Dogo tatizo lako ni kumu entertain Mke wa rafiki yako... Mbaya zaidi jamaa alijisogeza nyuma wewe ulivyo fala ndio ukazidisha ukaribu na shemeji yako.. Jamaa alikuwa ana wa zoom from a distance. Aliona mengi bila shaka... Hilo ni kosa la kwanza.

Kosa la pili wewe ni muongo muongo... Hapa unatuomba ushauri ila bado unasema uongo. Huyo shemeji yako ulikuwa una chat nae zaidi ya unavyosema hapa.... Na hadi ukawa unajua jamaa hamjali Mke wake maana yake uliweka ukaribu ili wewe ndio uonekane unajua kujali.. Simping

Kosa la tatu siku jamaa kaja na Mke wake kwako na kutoa tuhumu wewe ulibaki ukicheka cheka tu kama zuzu.. Pale ungekaza hata umchape makofi jamaa na Mke wake kwa kukuvunjia heshima. Wewe ukatulia Mke wa mtu kaachwa ndani kwako mume akaondoka wewe ukabaki nae tu.. Na bado mkaendeleza stories ndio baadae akaondoka..

Mumewe alishakutuhumu... Kamleta kwako na wewe ukatulia.. Kama jamaa aliondoka hatua chache anageuka nyuma anashangaa Mke yupo ndani kwako tuu.. Dakika kadhaa... Hapo huyo jamaa ndio anachorea mstari majibu yake.

Sasa, wote bahati mbaya mnafanya kazi ofisi moja. Hili jambo likifika ofisini ni lazima hatua zitachukuliwa. Na ni obvious alieingilia ndoa ya watu ndio atakae shughulikiwa.
 
Chema chajiuza na kibaya chajitembeza

Kama ni mwanamke mwema na hawana ndoa, mwambie tu afuate vitu vyake muoane

Kwani shilingi ngapi, ye si kasusa
 
Aisee
 
Kwa ufupi wewe ndiye uliyesababisha matatizo yote hayo,
Kama ungesimama as a Gentleman,wala huyo mke wa rafiki yako asingekua na ujasiri wa kukutamkia kua anakupenda,ila alikuona unaingilika kwa jinsi ulivyokua unadeal nae,

Jiandae kutafuta kazi sehemu nyingine tu.
 
Weka wazi kwanza ndio tuingie front kukupa maujanja. Tunajua hapo there is something fishy. Kiukweli kabisa picha iko wazi unamla,unapita nae,huyo shemeji. ??.

Hapa sio mahakamani,hapa ni sehemu ya wazi unasaidiwa unapita kushoto. Sasa ukifunga code kama hivyo,hata misaada inakuwa kwenye code hivyo hivyo.

Kwa hiyo Uzi unaweza ukatembea sana kwa hiyo mpaka mwisho unaweza usijue umesaidiwa ama ndio umejiongezea misamiati ktk tatizo lako. Kumbe chanzo kimeanzia kwako kupiga pin baadhi ya mavitu
 
Nawe pia jiandaeee
Mwenzio akinyolewa wewe tia majii
 
Rule 1. Usiwe na mazoea na mke wa Rafiki yako
 
Pole dogo.!ulifanya kosa kukaa kimya ila imesha tokea huna budi kutafuta suruhuu.aah..!umesema unafanya kazi kampuni moja,yaani rafiki yako,mke wake na wewe si ndio?ushauri wangu .“NENDA KWA MTU WAMAKAMO AMBAE YEYE ANA MUHESHIMU MUELEZEE KWA UKWELI NA UWAZI,KISHA AMUITE RAFIKI YAKO NA MKE WAKE MJADILI.KISHA JISHUSHE UMUOMBE MSAMAHA KWA KUTO MJULISHA MAPEMA.naami kufanya hivyo yata isha kwani KWENYE UKWELI UONGO UJITENGA.
(muhenga aishiwi busara karibu kijana)
 
Madogo tushawaambia acheni mazoea na wake za watu hata kuchat nae tu ni kosa acha kabisa
 
Kuna mambo umeficha ili uonekana hauna hatia....mtu hawezi kumuacha mke aliyezaa nae watoto kizembe hivyo.
 
Umiwahi kuitazama movie ya Andhaa Kanoon(kama wewe wa kitambo kile) kama umewahi fanya kama vile Amitha akifanya..kama hujaiona hiyo movie itafute uitazame utapata majibu.
 
Umiwahi kuitazama movie ya Andhaa Kanoom(kama wewe wa kitambo kile) kama umewahi fanya kama vile Amitha akifanya..kama hujaiona hiyo movie itafute uitazame utapata majibu.
aliambiwa kaua na hajaua akafungwa alivotoka akamuona yule jamaa alofungwa kwajil yake,,akamuua kwel mbele ya watu wazito😆😆kama sijakosea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…