Naombeni ushauri wakulima wenzangu.

Naombeni ushauri wakulima wenzangu.

Asante sana kwa muongozo, bado nina maswali kwako usinichoke tafadhali. Nimefurahi kuwa wewe mwenyewe ni mkulima wa kilimo husika cha nyanya vipi kuhusu mkoa ama sehemu inayo kubali kwa kilimo cha nyanya na msimu mzuri wa kulima nyanya ni upi? Asante
Kwa upande wa mkoa upi unafanya vzr zaidi sijui Mimi sijawahi Lima mkoa tofauti na Geita&mwanza.
Japo nimetembea kama morogoro,Arusha,pwani nk kote huko nyanya nilikuwa naona inastawi.
Uchaguzi wa mbegu Bora ndo solution mkuu. Mimi sio mtaalamu wa shuleni ila ni mkulima mzoefu wa zao hili.
Duh! Ina maana 5M kwa heka 3 hiyo hela ni kidogo sana! Asante kwa taarifa
Ndio huu ni ukweli huwezi Lima heka3 Kwa mtaji wa m5 huwezi mkuu.
Mbegu bora pekee ya kutosha heka 1 itenge laki7-8 Hivi.
Bado madawa na mbolea vibarua,kamba na miti ya kufungia nyanya Yako. Binafsi Hadi Sasa Hivi navuna Nina heka imetumia m3 na 457k Kuna zingine nilikuwa siandiki kama pesa za sabuni,mboga nk za wafanyakazi wangu.

Katika shamba hili sijakodi
Samadi sijanunua ipo home tu.

Niishie hapa mkuu
 
Ndio maana nimekuja kwenu kuomba ushauri, naomba taarifa sahihi mzee.
Tanzania kusema mazao ya biashara ni kama vile Pamba, Kahawa, chai, tumbaku na Pareto! Sasa sema labda unataka kulima kitaalam zao la mpunga au mahindi ambayo ni mazao ya chakula!
 
Ushauri mzuri sana huu, nyanya inatumia gharama kubwa sana mpaka hatua ya mwisho. Ila ni zao ambalo linaweza kutoa mara kumi ya kile umetumia. Ngoja niweke mambo sawa msimu ujao nije tuungane huko.
Kwa upande wa mkoa upi unafanya vzr zaidi sijui Mimi sijawahi Lima mkoa tofauti na Geita&mwanza.
Japo nimetembea kama morogoro,Arusha,pwani nk kote huko nyanya nilikuwa naona inastawi.
Uchaguzi wa mbegu Bora ndo solution mkuu. Mimi sio mtaalamu wa shuleni ila ni mkulima mzoefu wa zao hili.

Ndio huu ni ukweli huwezi Lima heka3 Kwa mtaji wa m5 huwezi mkuu.
Mbegu bora pekee ya kutosha heka 1 itenge laki7-8 Hivi.
Bado madawa na mbolea vibarua,kamba na miti ya kufungia nyanya Yako. Binafsi Hadi Sasa Hivi navuna Nina heka imetumia m3 na 457k Kuna zingine nilikuwa siandiki kama pesa za sabuni,mboga nk za wafanyakazi wangu.

Katika shamba hili sijakodi
Samadi sijanunua ipo home tu.

Niishie hapa mkuu
 
Sikushauri uache kulima mahindi uende kwenye ufuta, mahindi mavuno yana uhakika zaidi kuliko ufuta.
Huo ufuta tulilima tukiwa wadogo aisee ili ujaze gunia inabidi ujipinde hasa.
Nakumbuka tulikuwa tunapiga mzigo huo ila matokeo yake hata ndoo kujaa ni mtihani.
Ila soya nitalima Tena maana nililima miaka kama 5 iliyopita
 
Umeona. Nimeshalima ufuta ekari 40 skufikisha hata milioni kumi.
Mahindi nyanda za juu kusini ukilima kitaalamu mavuno ni uhakika sababu mvua zipo.
 
Habari zenu wapambanaji

Leo niko mbele yenu kutaka ushauri wa kimawazo kutoka kwenu ndugu zangu. Niko kwenye mpango wa kuingia kwenye kilimo kwa kumanisha hasa. Nina bajeti ya kiasi cha Tsh. 5M, hivyo kutokana na hicho kiasi niko mbele yenu kutaka ushauri wa mawazo kwa haya yafuatayo.

Nahitaji kufanya kilimo biashara na pia nahitaji ku dili na mazao ya biashara, hivyo naomba ushauri ni fanye hasa kilimo cha zao/mazao gani? Swali langu kuu ni hilo, nataka ushauri kutokana na nchi yetu Tanzania ni mazao gani ya biashara ambayo nikifanya ni hot cake. Nafahamu watu wanafanya kilimo cha Mahindi, Mpunga, Maharage, Nyanya nakadhalika. Binafsi nilihitaji ni komae na zao moja la biashara hivyo naomba ushauri wenu kwenye hilo.

Pia napenda kufahamu ni wapi ndani ya Tanzania hii zao husika linakubali kutokana na hali ya hewa, mfano ukiniambia fanya kilimo cha mpunga ningependa kujua ni wapi zao hilo niende kufanya ambapo unaona linakubali zaidi. Kutokana na kiasi changu napenda kuanza na heka tatu, nimedhamilia kuingia kwenye kilimo kwa msimu huu.

Natanguliza shukrani za dhati kwenu nyote, niko hapa nasubiri ushauri wenu. Ushauri wenu nitauzingatia kwa kina, asanteni sana.

Karibu.
Jikite katika kilimo cha vitunguu maji Singida au Iringa (Ruaha Mbuyuni).
 
Asante sana kwa ushauri wako, kwa hiyo pesa naweza anza na heka ngapi mpaka navuna bila presha, nilime mwezi wa ngapi ili kuangukia kwenye soko zuri mpaka wakati wa kuvuna?
Jikite katika kilimo cha vitunguu maji Singida au Iringa (Ruaha Mbuyuni).
 
Wataalamu wa hesabu wakiwa wengi hata kilimo kitakuwa na tija maana mtaani tutakuwa na watu wenye kufikir sana. Read and vote here

Asante sana, ni aina ipi ya maharage ambayo sokoni yana soko, vipi kuhusu mkoa mpaka kijiji ni wapi nikaweke kambi? Kwa huo mtaji unadhani naweza lima heka ngapi, msimu mzuri ni kuanzia mwezi wa ngapi kwa kilimo hicho?
Pesa mara nyingi haitoshi ila ukiamua hiyo pesa ninyingi mkuu
Kilimo nisehem sahihi kwangu nashauri ulime maharage
Ukiyazingatia vizuri kwahyo pesa unaweza pata mwanga zaidi
 
Soya inakubali hasa mikoa ipi na wakati mzuri wa kulimwa ni upi?
Huo ufuta tulilima tukiwa wadogo aisee ili ujaze gunia inabidi ujipinde hasa.
Nakumbuka tulikuwa tunapiga mzigo huo ila matokeo yake hata ndoo kujaa ni mtihani.
Ila soya nitalima Tena maana nililima miaka kama 5 iliyopita
 
Sahihi kabisa, kuna jamaa alipiga magunia ya kutosha huko Mpanda.
Umeona. Nimeshalima ufuta ekari 40 skufikisha hata milioni kumi.
Mahindi nyanda za juu kusini ukilima kitaalamu mavuno ni uhakika sababu mvua zipo.
 
Kabisa
Wataalamu wa hesabu wakiwa wengi hata kilimo kitakuwa na tija maana mtaani tutakuwa na watu wenye kufikir sana. Read and vote here

Asante sana, ni aina ipi ya maharage ambayo sokoni yana soko, vipi kuhusu mkoa mpaka kijiji ni wapi nikaweke kambi? Kwa huo mtaji unadhani naweza lima heka ngapi, msimu mzuri ni kuanzia mwezi wa ngapi kwa kilimo hicho?
Maharage yanjano(yale yasiyotambaa
Mkoa wa Ruvuma,
Vijiji vya Songea +mbinga + namtumbo madaba
kuna vijiji kama Mputa, Mbwambwasi, peramiho vijijini na baadhi yamaeneo kuelekea madada bado ardhi ipo

..kwa hiyo pesa unaweza Lima hata hekari tano mpka 7 nachenji ikabaki
Kutokana namvua msimu mzuri nimwezi wapili mpka watatu kufikia tareh 15 uwe ushapanda mwez wa sita unavuna
Kwamwezi wa12 yanakubali tatizo lipo yakianza kauka hivyo itakupasa uwe nabanda lakuweza kuanikia nakuhfadhi maharage yako
Maeneo kama mbwambasi navijiji vyakaribu kama Muhukuru kuna ardhi yakutosha nawatu bado hawajastuka hivyo unaweza wahi kwabei rahisi mpaka 90 mpka 100 elfu kwa hekari

Nikilimo chamiezi miwil mpka mitatu
 
Back
Top Bottom