Naombeni ushauri wakuu

Naombeni ushauri wakuu

Joined
Mar 21, 2024
Posts
30
Reaction score
135
Salaam wakuu.

Katika harakati za kutafuta kipi ni fanye baada ya masomo yangu ya ualimu hapo mwezi wa Saba, nimetoka Leo kuongea na Moja ya shule ya kanisa katoliki hapa jijini( niliwatumia letter of interest Leo wakaniita).

Wamenambia kuwa baada ya kumaliza chuo nifanye kazi nao kwa miezi sita(Bure), Kisha baada ya hapo watanipa mkataba, na Kwa kipindi hiko Cha kujitolea wamesema kuwa wa-tani accommodate chakula, malazi na matibabu.

Pia, wamesema kuwa taingia nao mkataba ambao utanipa assurance ya ajira baada ya Kipindi Cha miezi sita, ikiwa tatimiza mambo yafuatayo

1. Coverage ya topic ikiwa nzuri
2. Ufaulu wa wanafunzi kwa mitihani ambayo itakuwa inatugwa na department (kwenye somo langu)
3. Ushiriki wa kazi na usimamizi mzuri wa majukumu.
 
Unaweza ukapiga piga hapo huku ukiendelea kucheki michongo mingine boss.

Cha muhimu una pa kujishikiza Na hapo sio pa kutia kambi,
 
Actually Niipongeze Hio shule katoliki kwa kukupa fursa ya kuonesha uwezo wake.Nenda kafanye Nao kazi.Kwa ninavowajua Katoliki,Pesa Watakupa ili kwa sababu huwa wanatafuta aina fulani ya walimu basi Hicho Kipimo walichokupa ni Kizuri.Tatizo sasa umeleta JF ambapo napo kikatoliki inaonesha nidhamu yako ina walakini....
 
All the Best. Kubali tu hapo kama kuna uhakika wa ajira(kwa huo mkataba mtakaosaini) baada ya kujitolea
 
Actually Niipongeze Hio shule katoliki kwa kukupa fursa ya kuonesha uwezo wake.Nenda kafanye Nao kazi.Kwa ninavowajua Katoliki,Pesa Watakupa ili kwa sababu huwa wanatafuta aina fulani ya walimu basi Hicho Kipimo walichokupa ni Kizuri.Tatizo sasa umeleta JF ambapo napo kikatoliki inaonesha nidhamu yako ina walakini....
Dah ndugu umenipa moyo sana, acha nikaoneshe uwezo wangu, kama ni bahati yangu basi màmbo yanakuwa mazuri.
 
Back
Top Bottom