Naombeni ushauri wenu jamani kwenye hii biashara ya kusaga mahindi

Naombeni ushauri wenu jamani kwenye hii biashara ya kusaga mahindi

EveningStar

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2018
Posts
262
Reaction score
162
Habari yenu wakuu,

Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 29, elimu yangu ni shahada ya kwanza.

Ni hivi baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kutafuta kazi bila mafanikio yoyote, hivi karibuni nimekutana na jamaa mmoja, yeye ni muajiriwa serikalini na anataka kuanzisha biashara yake ya kusaga mahindi, kupack unga na kusambaza kwa wateja.

Sasa huyu jamaa changamoto aliyokua nayo ni kwamba hana muda wa kutosha kusimamia biashara atakayoianzisha, hivo kutokana na mimi sina kazi hivi sasa, ameniomba niwe msimamizi wa biashara yake na faida itakayopatikana atanipatia asilimia 30.

Na huyu jamaa anataka kununua mashine zake mwenyewe za kusaga mahindi.

Hivyo naombeni ushauri wenu jamani wazoefu wa hii biashara au wenye uelewa wa hii biashara katika mambo yafuatayo,

1.)Upatikanaji wa malighafi yaani mahindi mazuri.

2.) Soko lake lipoje?

3.) Upatikanaji wa vifungashio upoje?

4.) Ushindani katika soko upoje?

5.) Utaratibu wa kufanya hii biashara kisheria upoje? namaanisha utaratibu wa kusajili na kupata vibali katoka mamlaka husika.

6.) Kodi ipoje?

7.) Upatikanaji wa mashine na gharama zake zipoje?

8.) Ipi sehemu nzuri ya kufanyia hii biashara? Jamaa na mimi tupo DSM

9.) Changamoto ya hii biashara ipoje?

10.) Wapi yanapatikana mahindi mazuri?

11.) Vipi kuhusu usimamizi wake upoje?

12.) Changamoto zake zipoje?

13.) Faida yake ipoje?

Ni hayo tu ndugu zangu, naombeni msaada wenu kuyajua ili niweze kuilewa hii biashara angalau nipate pa kuanzia kama msimamizi.

Ahsanteni sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nakuadvise tu aangalie industry nyingine hii ya food products iko crowded sana, faida mtapata lakini ndogo kutokana na ushindani mkubwa.

Kwa nini msijaribu industry ambayo kidogo ushindani wake sio mkubwa mfano mimi naweza kuku suggestia waste management upande wa households , viwandani na taasis tayar kuna makampuni makubwa .
 
Hio biashara inachangamoto za ushindani, ! Hebu check na mshauriane biashara nyingine! ..

Pia nakushauri Kama inawezekana mtoke huko Dar kwenu mtembee huku mikoani ili kuangalia fursa mbalimbali , sio kukaa dar tuu! Kumbuka kukaa sehemu moja ndio linapelekea kuanza kukopi biashara za wengine!

Mfano, huku mikoani Kuna fursa ya viwanda vya mafuta ya kula! (Alizeti) .. kwenye Alizeti utauza mafuta, utauza Mashudu, utauza 'ugido'..etc.. na soko la mafuta ya Alizeti la ndani ni kubwaa na huwezi kulimaliza .

BTW hongera kwa kupata ajira mkuu?!! Sisi bado tunachoma mahindi ya pilipili na limao,[emoji2][emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ajira iko wapi mkuu?, si mpaka faida ipatikane, jamaa anaipenda hiyo biashara, sasa kama ina changamoto ya kiushindani hamna namna ya kuikabili hiyo changamoto mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hio biashara inachangamoto za ushindani, ! Hebu check na mshauriane biashara nyingine! ..

Pia nakushauri Kama inawezekana mtoke huko Dar kwenu mtembee huku mikoani ili kuangalia fursa mbalimbali , sio kukaa dar tuu! Kumbuka kukaa sehemu moja ndio linapelekea kuanza kukopi biashara za wengine!

Mfano, huku mikoani Kuna fursa ya viwanda vya mafuta ya kula! (Alizeti) .. kwenye Alizeti utauza mafuta, utauza Mashudu, utauza 'ugido'..etc.. na soko la mafuta ya Alizeti la ndani ni kubwaa na huwezi kulimaliza .

BTW hongera kwa kupata ajira mkuu?!! Sisi bado tunachoma mahindi ya pilipili na limao,[emoji2][emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
Namna ya kuikabili hiyo changamoto mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
papaa ingieni tuu shamba kunalipa kuliko hio, miezi mitatu tuu unaanza kuona mwelekeo ,hio hadi miezi 6 hadi 7,utengneze jina,utashangaa mnakuja kuuza mashine bei ya skrepa,

upande wa pili ni kwamba hio ni biashara nzuri ukipata soko,pia mnaweza mkaanza kuuza pumba,kusaga kwa wakazi wa eneo ili kupunguza gharama za uendeshaji,pia mkawa na shamba lenu wenyewe ,biashara sio yakuingia na miguu miwili,ni hayo tuu mkuu,wisioajiriwa wako wengi usikate tamaa,io kofia ya degree ivue
 
Biashara hiyo inaweza kukulipa au isikulipe unategemea na wewe ulivyo amua kuindesha :
Mt mtaji, unacho zalisha,mbinu za kushindana kwenye soko nk
Zitatoa majibu ya swali lako
 
Back
Top Bottom