Naombeni ushauri Wenu ni Muhimu nimechanganyikiwa

Naombeni ushauri Wenu ni Muhimu nimechanganyikiwa

N
Ndio nina ujuzi huo mkuu nafanya software kama uko interested njoo PM
Mkuu emu toa maelezo software siku hizo zimerahisishwa kiasi kwamba kuna madogo hawana hata ujuzi wa computer ila wanatengeneza software, kazi umeacha au umefukuzwa?
 
Kabla hujafanya chochote jipe mda kwanza wa kutafakari usifanye mambo kwa kukurupuka hata km kilichotokea kimekupa jeraha kiasi gani kwa hio hio million yako na points usiitumie ihifadhi sehemu salama huku ukiwa unatafakari nini cha kufanya, na ukitaka upate ushauri mzuri juu ya nini cha kufanya tafuta watu wanaofanya waombe ushauri watakushauri vizuri, yangu ni hayo tu mkuu
 
Daah nimepoteza kazi.. akiba nina 1.3 million kodi nimeshalipa miezi sita naishi na ndugu zangu wawili mimi ni mjuzi wa Computer software.. Nssf nina 22million wameniambia nikae miezi 18 ndo watanipa hela tangu yote kwa sasa wanipa asilimia 33% ya mshara wangu kigezo kuwa nina Elimu naweza kupata tena kazi na mimi mpango wa kuajiriwa sina tena na wala sitaki..

Naombeni ushauri wenu nifanye biashara gani na hyo 1.3million nawaza kwenda Arusha nikajitafute upya kwa sasa Naishi Dar
FIC ukiweka 1.3M kila siku unadownload not less than 100k per day
 
Nimepunguzwa kazini
Mkuu, wazazi ndo kila kitu kwako, waambie ukweli angalia mwenye moyo mgumu ambaye hata panic haraka umwambie ukweli kisha yeye ndo ataangalia namna ya kumwambia mwenzake

Kama Baba ndo jasiri basi mwambie yeye kisha yeye ndo atamfikishia mama hili ni muhimu usipuuze

Pili dili na mtu wa NSSF tafuta mmoja ambaye anaonekana ndo mkubwa angalia namna ya kukutana naye private umwambie huna mpakgo wa kuajiriwa afanye mpango upate chako kisha utampoza

Nim3penda msimamo wako hutaki kuajiriwa

Hiyo 1.3m kama tayari una computer angalia namna ya kujiboresha (kodi hata fremu kisha weka tangazo la huduma unazotoa ukiweka bango utaamgalia namna ya kuwalipa manispaa waweza kufungua hata stationary uchwara)
 
Mimi mwenyewe nitakwambia anzisha biashara ya duka la rejareja a.k.a mangi. Angalia wewe mwenyewe sehemu gani nikiiweka itakuwa inazunguka kila siku inakupa faida. Tumia hivyo 33% katika mahitaji yako ya kila siku, lakini hakikisha unahifadhi hiyo 33% walau nusu ukishindwa walau robo uwe unaipeleka dukani ili duka likuwe kwa haraka. Ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom