thelostnuts
Member
- Jan 16, 2015
- 67
- 19
Wanajukwaa kama mada inavyojieleza hapo juu mimi ni mama wa makamo( miaka 35) nimejishangaa ghafla nimebadilika umbo langu bila kutegemea nilikuwa na umbo zuri kwa kweli sikuwa na tumbo kabisa pamoja na kwamba Nina Watoto wawili, mikono yangu ilikuwa midogo kuendana na mwili wangu huku ikiwa nyama zimekaza sasa tumbo limekuja na mikono imejaa,mbaya zaidi nyama za mikono na tumbo zimelegea.!
Siwafichi kwa hili linanikosesha confidence mbele ya watu, mume wangu naye amekuwa akiniambia kuwa siku hizi sipendezi kama ilivyokuwa zamani Kwa kweli inaniumiza.
Sijabadilisha mfumo wa maisha yangu ni ule ule wa siku zote, sijawahi kufanya mazoezi wala kufanya diet, sasa ninajiuliza ni kitu gani kimenibadilisha ghafla hivi.
Naombeni ushauri wenu ni nini nifanye niweze kurudisha umbo langu,na pia niweze kuwa na confidence kama zamani maana hata nguo naona hazinipendezi tena na pia nahisi nitakimbiwa na mume maana hana amani na hili liumbo utafikiri kalibeba yeye.