Si jambo la ajabu, ni dalili kuwa umri umeanza kukutupa mkono, lazima uyakubali mabadiliko, nadhani unayakumbuka matiti yako wakati unavovunja ungo jinsi yalivyokuwa yamesimama vyema na imara kama kifuu cha nazi, bila ya shaka hali hiyo haipo tena. Kwa ufupi hayo Ndio mabadiliko yanyoendana na umri, muda si mrefu utaona mabadiliko ktk maeneo yanayozunguka macho yako, usishangae bali yapokee tu.
Pendelea kula vyakula vinavyojenga mwili mara kwa mara ( matunda na mboga mboga) vitakusaidia kuimarisha ngozi yako isilegee sana. Pia fanya mazoezi ya kutembea kwa miguu angalau nusu saa kwa siku. Ukitembea 1hr itapendeza. Pia posheni yako ya chakula kila unapokula hakikisha inakuacha ukiwa bado unatamani kula ( iache tumbo wazi japo kidogo).
Jioni unapolala usile hadi kushiba. Unaweza kunywa maji na sambusa moja au mbili.