Naombeni utaratibu wa kuwajibisha Precision Air Tanzania

Naombeni utaratibu wa kuwajibisha Precision Air Tanzania

doppla2

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2014
Posts
1,393
Reaction score
1,462
Karibu miezi miwili sasa nimekumbana na kazia mbovu ya huduma kwa wateja kutoka kampuni ya ndege ya Precision Air.

Tofauti na sera yao ya utaratibu wa kurejesha pesa kwa safari iliyohairishwa na kutolewa report ndani ya wakati ndani ya week 2, jitihada za kuwasiliana na huduma kwa wateja zinagonga mwamba na kuishiwa kupewa haadi wasizozitekeleza. Kila siku utajibiwa kwa maneno ama email suala lako linashughulikiwa na tutawasiliana nawe soon.

Kwa wenye uzoefu na taratibu za shirika hili au usimamizi wa mashirika ya ndege yanaposhindwa kutimiza huduma kwa wateja , ni hatua gani za kuchukua ili kudai uwajibikaji ? Njia za kuongea na customer care naona hazina matokeo inaonyesha mfumo wa mawasiliano ni sehemu ya kikwazo kwa utoaji wa haki kwa wakati.

Natanguliza shukrani nikipewa abc za kuwafikia wahusika . Kwa sasa Niko nje ya Dar .
 
Back
Top Bottom