Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Dalili ni hizi tatu miongoni mwa nyinginezo.
1. Speech ya Makamba kumjibu Lissu
Huyu mzee katoka mafichoni na kuja kujaribu kujibu hoja za Lissu!
Ni hivi: Mzee kaona jahazi linazama, kwahiyo akaona ni bora ajitokeze kuokoa jahazi ingawa kazi ya kujibu hoja za Lissu walipewa UVCCM kwa maagizo ya Bashiru, ila bila shaka mzee amegundua UVCCM pekee hawana uwezo wa kujibu hoja za Lissu hivyo kawataka na wazee wa chama wajitokeze kusaidia.
Kuna wanaoweza kudhani lengo la Makamba ni kumtafutia uteuzi mwanae, ila kwakweli Makamba ameshaona hali ni tete na waze wa chama sasa hawapaswi kukaa kimya.
2. Kauli ya Ndugai ya kumfananisha Lissu na mnyama
Kauli hii ukiichunguza, utagundua inatokana na chuki ambayo chanzo chake ni ushawishi na kukubalika kwa Lissu, jambo linalowafanya wamemjengee chuki Lissu na njia mojawapo ya kuonyesha chuki au kutoa hasira zao ni kutumia lugha kama aliyoitumia ambayo inaonyesha wazi chuki na hasira aliyonayo dhidi ya Lissu.
3. Matamshi ya Kheri James
Huyu nae ni kama Ndugai kwani inaonyesha amepaniki baada ya kuona jinsi Lissu anavyowafunika kwa hoja na sasa wamekosa hoja za kujibu na badala yake wanaibuka na lugha za vitisho na madai ya uongo eti Lissu anamtukana mgombea wa chama chao.
Kama kweli anamtukana,mwambieni ataje hayo matusi kama hajaisha kujikanyaga tu.
4. Mzee Baba kwenda mapumzikoni
Mapumziko haya ni matokeo ya kucheza mziki wa Lissu, na kwakuwa mziki wenye ni mnene, basi alilazimika kutumia nguvu za ziada ili kujaribu kwenda sambamba na beat, matokeo yake wamechoka/amechoka wakati beats zikiwa bado zinaendelea unless mapumziko hayo yamo kwenye ratiba ya kampeni zake.
Hata vitani huwa kuna kawaida ya kurudisha majeshi nyuma na kujipanga upya inapotokea mmepata kichapo kikali na kitakatifu huku mkiwa mnapoteana katika uwanja wa vita (battlefield), na hiki ndicho CCM wanakifanya kwa sasa kurudisha majeshi nyuma waangalie wanatoka vipi(wanatia huruma).
Kwahiyo, kutokana na watu hawa kuzidiwa kwa hoja huku wakiumizwa na mafuriko katika mikutano ya Lissu,mtarajie kuona na kusikia mengi ya kushangaza kutoka kwa watu hawa: vitisho, frustrations, hasira, jaziba, n.k.