Naona kabisa ile kauli ya Mwl. Nyerere kuhusu CCM imeanza kuiva, angalia

Naona kabisa ile kauli ya Mwl. Nyerere kuhusu CCM imeanza kuiva, angalia

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Nadhani muda umefika siyo mbali CCM inakwenda kulala upande mmoja.

Mwl. Nyerere aliposema CCM si mama yake wala baba yake alikuwa na maana hasa.

Mwl. Nyerere aliposema mpinzani wa kweli atatokea ndani ya CCM basi si mbali.

Mwl. Nyerere aliposema CCM hakitakuwa na uwezo tena pale atakapotokea mjinga mmoja na kusema ...' sasa nani anabisha huyo mjinga hajasema?

Mapishi yapo jikoni, kuna hali ya kushangaza sana ambayo kuna waliopo ndani wanaona wapo salama na walio nje wanaona sawa tu ndiyo chama chetu hiki tutapita tu.

Ni kwa sababu ya mazoea kwamba kuna bao la mkono, ukiachana na bao la mkono pia kuna bao la jeshi la polisi, hawa nao kwa sasa hawajijui wapo wapi japo wanaelewa kazi yao ni nini.

Tunasuka na kunyoa na yetu ni macho na masikio, 2025 lolote linaenda kutokea.
 
Shida ni kutaka kuendesha nchi kama drugs cartel huku CCM ikiwa ndio engineer mwenyewe.

Kuna watu wanaona hii nchi ni mali yao na familia zao na wengine hawana mamlaka, matokeo yake wametumia muda mwingi kuwekeza kwenye inner circle yao kuliko kujenga mifumo imara itakayokuza vipaji vipya kwa faida ya Taifa na sio binafsi.

Matatizo yakutotengeneza mfumo imara na kuwa busy kutengeneza himaya binafsi ya familia na inner circle ndio yametufikisha hapa sasa kila mtu akiibuka huko nakusemasema hovyo Watanzania wanaona huyu anaweza kutusaidia kumbe naye Hana competence.

Kuibuka kwa watu jamii ya kina Makonda, Makamba, Mwigulu, Nape, nk ni dalili ya failure ya mifumo inayoweza kuruhusu watu wa namna hii kupitia connection zao kuingia na kujenga himaya zao ndani na nje, matokeo yake wanaonekana wana influence kumbe NI kwasababu ya wingi wa wajinga wenzao.

Leo kumeibuka wajinga ambao kupitia legacy ya JPM basi wanataka kuwaonyesha wananchi ambao wako stranded wao ni kama JPM kumbe nao ni bogus tu, Leo mtu kama Job au Konda boy nk wakipiga kelele zenye mlengo wa Kimagufuri basi tunaamini nao ni kama JPM kumbe wanataka kumtumia marehemu kama stepping stone tu.

Wazee wote wanaojielewa Jeshini na TISS ni wakati sasa wakufanya sehemu yenu kwa kuiokoa nchi kwenye Cartels na wimbi la wajinga waliopata nafasi yakupenyezwa kwenye mifumo nakujiona wao ni exception na nchi inachakuwalipa na sio wao kuilipa Tanzania.
Hawa wajinga ndio mpaka leo wametufikisha hapa, vijana hawana ajira, biashara za madawa kushamiri, wizi na ufisadi Serikali, kujaza incompetence Serikalin, rushwa, undugu, ukabila, udini, uchawa kushamili, umalaya, mfumo mbovu wa elimu, miundombinu mbovu, huduma mbovu za Afya nk.
 
Nadhani muda umefika siyo mbali CCM inakwenda kulala upande mmoja.

Mwl. Nyerere aliposema CCM si mama yake wala baba yake alikuwa na maana hasa.

Mwl. Nyerere aliposema mpinzani wa kweli atatokea ndani ya CCM basi si mbali.

Mwl. Nyerere aliposema CCM hakitakuwa na uwezo tena pale atakapotokea mjinga mmoja na kusema ...' sasa nani anabisha huyo mjinga hajasema?

Mapishi yapo jikoni, kuna hali ya kushangaza sana ambayo kuna waliopo ndani wanaona wapo salama na walio nje wanaona sawa tu ndiyo chama chetu hiki tutapita tu.

Ni kwa sababu ya mazoea kwamba kuna bao la mkono, ukiachana na bao la mkono pia kuna bao la jeshi la polisi, hawa nao kwa sasa hawajijui wapo wapi japo wanaelewa kazi yao ni nini.

Tunasuka na kunyoa na yetu ni macho na masikio, 2025 lolote linaenda kutokea.
Tuendako wote watanyoa vipara.
 
... Kuna watu wanaona hii nchi ni mali yao na familia zao na wengine hawana mamlaka, matokeo yake wametumia muda mwingi kuwekeza kwenye inner circle yao kuliko kujenga mifumo imara itakayokuza vipaji vipya kwa faida ya Taifa na sio binafsi ...
Hao ndiyo hawa wanalazimisha yeyote ajaye awe ndani yao na ikiwa ni nje yao basi wanahakikisha wanamsimamia everything.

Unaona mzee JPM alivyotaka kufanya mapinduzi mapya ya CCM mpya isiyo na hawa watu?, mwisho ndiyo wakampoteza.
 
Back
Top Bottom