Naona kama mkosi Mkubwa kwangu kuzaliwa jamii ya watu weusi

Naona kama mkosi Mkubwa kwangu kuzaliwa jamii ya watu weusi

Huyu katoka kwemye familia ziizokuwa advanced ya umaskini. Huko ukinya chalet ukijamba nchale ukikaa nchale ukiinama nchale. Hakuna koneksheni wala mipango ya maendeleo. Ukienda mjini huagi, ukitaka kununua kitu cha maana usiseme.
 
Mkuu ni kweli kuna mambo ya ajabu na binadamu wa ajabu ajabu sana Africa na hata duniani kwa ujumla ila lazima ujue jinsi ya kwenda nao sawa tu maana hakuna namna umeshakuja duniani tena bongo.
 
Binafsi kuzaliwa mtu wa jamii ya watu mweusi kumegeuka mkosi na sio tu kuzaliwa katika jamii ya mtu mweusi pia kuzaliwa Afrika& muafrika na pia sio tu kuzaliwa muafrika pia kuzaliwa Tanzania na Mtanzania.

Ni mambo ambayo kabla ya kuzaliwa kwangu kama ningepewa machaguzi hakika nisinge fikiri mara mbili ninge yakataa haraka sana bila hata kujiuliza mara mbili mbili.

Katika safari ya maisha yangu sijawahi kabisa kufurahia maana ya maisha na sababu yake naifahamu na inanitesa sana.

Sina uwezo wa kuikataa asili yangu na jamii yangu na hata kama nikifanya hivyo nitakuwa najiongopea tu lakini ukweli halisi utabaki ndani ya moyo wangu ukinitesa sana.

Binafsi nimekuwa ni mtu wa kuwaza sana tena sana hali ambayo mara kadhaa imekuwa ikinipelekea mpaka mwili wangu kutokuwa sawa kiafya.

Nimejaribu mara nyingi kuya puuzia, kujiepusha na kutoya fuatilia mambo yanayo tokea katika jamii yangu angalau nilinde afya ya mwili wangu kwa kujiepusha kuwaza sana lakini nimeshindwa ni kama hayo mambo yana nilazimisha niyawaze hata nikijaribu kujiongopea kwa kutokuyafuatilia lakini changamoto bado ipo.

Inahitaji moyo wa kipekee sana kuwa mtu mwenye furaha katika hii jamii yetu.

Jamii yetu kwa haraka unawezasema ni kama imerogwa au imelaanika huko kale au sijui ndivyo ilivyo ? Kwa kweli sifahamu labda wenzangu mnafahamu.

Huu mkosi wa mimi kuzaliwa katika hii jamii sitapenda wala sitahitaji kizazi changu kije kirithi hii hali maana inahitaji uvumilivu wa kiwango cha juu sana pasipo kuchukua maamuzi magumu.

Katika jambo nililo jiapizia ni mimi kutokuja kuleta kiumbe katika mkosi huu kama huu mkosi acha unipate mimi tu na nife nao lakini sio kiumbe changu kuja kurithi hii laana ambae mimi Baba yake nimeiona na kuishi katika jamii yangu.

Imefika muda unaishi tu ili umalize safari ya maisha yako hapa duniani ufe.

Nimekuwa ni mtu wa huzuni nyingi sana mara nyingi na pia ni mtu wa kufikiri sana kupita kiasi, wenda kuzunguka kwangu maeneo mengi katika jamii yangu kuna nitesa sana na kupelekea yote haya.

Na hakika niliyo shuhudia yana hitaji moyo mgumu sana na wa uvumilivu kufikiri sisi hatuja laaniwa au hatuna mikosi.

Mitandao kidogo inasaidia kunipunguzia huzuni na wakati mwingine nayo inachangia kuniongezea huzuni ni sawa na 50/50.

Inahitaji moyo mgumu sana kuyavumilia haya ya jamii yangu maana ni mateso makali na ukiwa na akili timamu hakika mateso makali lazima yatese mwili wako mpaka siku ya kifo chako.

Kama kweli kuna maisha ya pili baada ya kifo na nikapata machaguzi ya kuzaliwa wapi hakika sitaweza kuchagua asili yangu na jamii yangu niliyo nayo.

Kwa sasa sina uwezo wa kukimbia kivuli changu(asili yangu ) lakini acha nikipieshe kizazi changu juu ya hii laana iliyopo katika jamii yangu.

Unahitaji moyo wa kipekee sana tena sana kutokuchukizwa kwa yanayo endelea.
Tafuta kitu ufocus kukifanya jitahidi uwaze hicho kitu baada ya muda utakuwa normal achana na nyumbu ambazo hazielewi nini haswa unapitia
 
Tazama ramani utaona nchi nzuriiii
Yenye mito na mabonde mengi yana.......

Taaaanzaniaaa tanzaniaaaaaa
Nakupenda kwa moyo woteeee....

Mungu ibariki tanzaniaaaaaa
Wabariko viongozi wakeeeee

Mungu ibariki Africaaaaaa ......
 
Huyu akienda Ulaya harudi!

Africa kuna makelele ya watu, radio, magari nk, kuna kufuatiliana kijinga jinga , kuna majungu, kuna uchawi, kuna vumbi, ajali, njaa, magonjwa, ujinga, ufisadi, ndoa ndoano nk
 
Hii ndio jobless depression nayoijua mimi. Mkuu fanya kitu kama yule maarab wa Tunisia aliyejimwagia petrol na kujichoma moto live.
 
Acha kufuru,
Kuna watu wsmezaliwa Gaza na Sudan.
Usifikiri kuwa wakaazi wote wa Gaza na Sudan wanafurahi kuzaliwa huko.

Namna ya kufikiri na kutazama mambo tunatofautiana kati ya mtu na mtu.
 
Mkuu ni kweli kuna mambo ya ajabu na binadamu wa ajabu ajabu sana Africa na hata duniani kwa ujumla ila lazima ujue jinsi ya kwenda nao sawa tu maana hakuna namna umeshakuja duniani tena bongo.
Ni kweli hakuna namna maana tayari imekwisha tokea siwezi zuia hilo ni kusubiri kifo tu, lakini kama kungekuwa na machaguzi hakika nisinge chagua kikombe hiki.
 
Tafuta kitu ufocus kukifanya jitahidi uwaze hicho kitu baada ya muda utakuwa normal achana na nyumbu ambazo hazielewi nini haswa unapitia
Nje ya kazi nilijaribu hicho unacho zungumza lakini ni kama nilikuwa najirisha upepo tu.

Nilikuwa najiongopea kutokuyafuatilia baadhi ya mambo lakini kichwa changu kilikataa mpaka sasa kimekataa.

Umewahi kufikiri mpaka kuumwa kwa zaidi ya siku mbili ?
 
Nje ya kazi nilijaribu hicho unacho zungumza lakini ni kama nilikuwa najirisha upepo tu.

Nilikuwa najiongopea kutokuyafuatilia baadhi ya mambo lakini kichwa changu kilikataa mpaka sasa kimekataa.

Umewahi kufikiri mpaka kuumwa kwa zaidi ya siku mbili ?
Kumbe mie nilikuwa na hali nzuri nilijibu kupitia namna hii na itakuwa vyema kama ukimwona daktari kwA matibabu zaidi
 
FB_IMG_1717598792712.jpg
 
Back
Top Bottom