Naona Kula Mgahawani ni nafuu kuliko kupika kwa mtu mmoja

Kupika simple sana na napenda sana sana Ila baada ya kupika na kula vyombo naosha baada ya wiki 3 mpaka mwez na mpaka nione kutu Labda ndo nashtuka au mpaka nzi wasuse na hujikuta nambulia kuvitupa nankununua tena

Karibu buan ndo maisha yetu
 
Sure mkuu ila migahawani wanatulisha sana mauchafu, mara maji ya mchele waoshee qu.mer na maujinga ujinga kibao tu ila kwa issue ya gharama ni nafuu sana kwa walio single kuliko kupika mwenyewe.
 
Asee kupika chakula cha mtuu mmoja inahitaji moyo. Though kuna changamoto lakini ni bora kujipikia mwenyewe kuliko kula kwenye mgahawa. Vyakula vya mgahawa havishibishi na havna flavor..kama umezoea kula nyumbani utapata tabu na vyakula vya mgahawa.
 
Changamoto nayopata ni kuosha vyombo...inafika mahali natamani vuta jiko. Pia naeza enda gengeni 3 times...kwan naeza fika gheto..mara nimesahau...karoti...sijui hoho...tangawizi...daah kazi kweli..
Hii pia ilinikumba mimi
 
Kula mgahawani ni nafuu mno kwa bachelor kama mimi..unaokoa muda pamoja na gharama pamoja na mausumbufu mengine ya ajabu ajabu yanayo husiana na kupika
 
Kusevu gharama ni pamoja na kula vitu usivyopenda kama ugali na misumari (dagaa). Ila kama utataka kula pilau ni aheri ule kibandani tu.
 
Kwenye maisha ya ubachela wanasema kupika sio kazi kuosha vyombo. Endelea kula magengeni au vuta jiko mkuu
Hio ndio biashara ambayo inanifanya nishindwe kupika yani. Kupika ni raha sana ila ingekuwa kuna namna ukishashiba vyombo vinajiosha ingekuwa raha sana. Mchina atufyatulie mashine hio tafadhali. Kupika sio kazi, ishu kuosha vyombo yani ndio balaa!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…