Watu wawili mkila mgahawani kuanzia asubuhi
Si nafuu kujipikia ndani
Nakukatalia mkuu,
Maybe inategemea na Mwanamke uliekua nae.
Ila kwangu ilkua tofauti sana miaka hiyo kabla hatujawa na familia kubwa.
Mfano:
Tulikua tuliishi wawili TU, Mimi na wife.
Tulikua na biashara ya vyombo vya ndani, Electronics ndogo ndogo (used&mtumba) , phone accesories, vipodozi , Saa na vikorokocho vingine vingi TU.
Hatukua na fremu wala nini,
Mzigo wa biashara ilkua juu ya meza ya mbao zile zinazowekwa barabarani maeneo ya K'koo opposite INA ilipo sahv jengo la CHINA PLAZA ile njia ya kwenda buguruni.
Ikifika jioni,Mzigo tulikua tunapakia kwenye tololi LA mbao na kufunika mpaka asubuhi
Mda wote nlkua nakomaa pamoja na wife.
Mchana tunakula mgahawani chakula cha 1500 kila mtu,Jumla 3000 MCHANA UNAPITA
Ikifika SAA 10 mchana wife anaenda home kuandaa cha jion.
Cha ajabu,
Ukimpa ile ile elfu 3 , anadai haitoshi.
Wakati mchana huo huo,
Imetosha kabisa Wali Nyama+ndizi mbivu tumekula na kushiba kabisa.
AISEE,
UGOMVI WA BAJETI YA CHAKULA ULKUA NI KILA MARA