AbuuMaryam
JF-Expert Member
- Dec 26, 2015
- 2,577
- 4,637
Na mimi swali langu liko hapo kwny electronic za mtumbaHahahaaaa hongereni sana
Familia iliyostruggle pamoja Mara nyingi huwa na furaha sana
Nje ya mada;hivi electronics za mtumba zinapatikana wapi?
Mgahawani huwa natumia 10k au 15k ni bora nipike tu hata mara moja kwa siku inapunguza gharama
elfu 60 kwa siku unalisha hekalu?Mke wangu kaenda kwao kujifungua,kabeba na watoto wakawaone ndugu zao upande wa mama yao,ni holiday season,napika kila siku na kazini naenda siyo kwamba nakwepa gharama la hasha kila nikila mghahawani huwa sipati radha ya chakula ninayoihitaji,najua kupika vizuri mama yangu alinifundisha since nikiwa darasa la tatu,lakini pia kusema gharama za kula gengeni zifanane na za kupika mwenyewe siyo kweli katika kupika mwenyewe huwezi kutumia elfu 60 kila siku Mimi nanunua nyanya na vitunguu vya wiki nzima kwa TSH 5000/=(nyanya 3500 na vitunguu vya 1500)
Mafuta lita tano utasahau kabisa,mchele kg 50,utasahau kabisa,gesi na gunia la mkaa utasahau kabisa hivyo vyote vitagharimu kama (130,000/=)kwa maisha nilipo.Ukiwa na hivyo vyote unaweza ukapitia mbogamboga za majani za mia tano ukala mlo wako safi kabisa.Naomba tu niishie hapo.
Wakuu,
Moja ya changamoto kubwa ninayokumbana nayo ni suala la kupika.
Baada ya Kula Mgahawani kwa muda mrefu, nikaona nianze mchakato wa kupika. Lakini nimegundua kuwa, Kupika chakula cha mtu mmoja ni Gharama kubwa kuliko kula mghahawani.
Mimi bajeti ya chakula cha mchana ni 3000 na jion hivyohivyo, hivyo jumla kuwa 6000 kwa siku.
Lkn nilipo anza kupika nikaona gharama ni zilezile mchanganuo ni kama ifuatavyo,
1. Mchele nusu 1000
2. Mboga za majani 500
3. Mafuta 500
4. Nyanya na vitunguu, hoho 1000
5. Nyama robo 1500
6. Nishati 500
Jumla inakua 5000
Najua wengine watasema vitu unanunua kwa jumla, lkn nimefanya hivyo na ukichukua hesabu zake ni kama hivyo tu.
Sasa hapo hujaweka usumbufu wa kupika, kuosha viombo, kumwagamwaga maji, na muda pia.
Pili kupika kunahitaji ufuatiliaji, mana nishaunguza sana tu.
Je nyie ambao ni mabachela mnaweza save vipi gharama kwa kupika na kuepuka kula mghahawani?
Labda mnaweza nishawishi tena nirudi jikoni mana nilipika wiki mbili nikaacha mpk vitu vikakaribia kuharibika ikabidi nivigawe tu.
Mkuu,Heri yako unayekula 3000, mimi lunch yangu inarange 7000 hadi 10000, diner the same, niwekee huo mchanganuo tuone kipi afadhali
Ndio, yaani ukipita karibu na kwa mama ntilie ubwabwa maharage tu utasikia unanukia hadi mtaa wa tatu na unaanza kuhisi njaa wakati ulikuwa umeshiba
Hyo saccoss wanapika chakula?Mkuu,
Nilikuwa na matumizi makubwa sana, kwa siku nilikuwa napindua 20k kwenye misos tu, hujaweka mafuta..
Nikaona hii balaa, nikaamua kujiunga na Saccos moja ya serikali, ili wawe wananikata kiasi fulan kila mwezi,
Kiukweli baada ya kuweka limit, nikaweza kujishape kwa 12k kwa siku na ninampango wa kufika 10k.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha kwa hiyo ww kila siku unakula nguna na dagaa mchele tu??Kibachela buku tu inatosha.
Hua nazungusha kiugali changu unga robo 200. Napika kwa kerosine stove (jiko la mchina). Mafuta koroboi 2 150 jumla 300. Yanatosha kuivisha ugali.
Mboga: Nachukua na dagaa mchele wa kulumagia. Japo fungu ni buku niliingia MoU na Mama Chuki awe ananiuzia nusu fungu yaani 500 na kila siku nanunua kwake tu
Sipakui ugali nakula kwenye sufuria tu na dagaa nakula kwenye gazeti lake. Kwahyo kazi yangu ni kuosha sufuria na mwiko tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo mkuu, hua nabadili diet nikiwa nje na home kwenye mishemishe.Hahahaha kwa hiyo ww kila siku unakula nguna na dagaa mchele tu??
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye maisha ya ubachela wanasema kupika sio kazi kuosha vyombo. Endelea kula magengeni au vuta jiko mkuu
Kwenye maisha ya ubachela wanasema kupika sio kazi kuosha vyombo. Endelea kula magengeni au vuta jiko mkuu
Acha kuendekeza umasikin, mwili haujengwi kwa matofali utazeeka siku siyo zako ipende afya yakoBachela nataka kuwa bachela sababu maisha ya kisela sometimes yananipa raha
Mkuu
Watu tunatumiaga hiyo 1000 kwa siku na tunadunda mtaani
Nunua mkate au maskonzi weka ndani kazi ni kuhakikisha chupa inachai muda wote
Maisha yanaenda mungu siku moja atafanya maisha yawe mepesi usijali mkuu