Naona kuna kila dalili ya Prof Jay kutimkia CCM

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656


Wakati wakina Lema na Chadema wakishinda mitandaoni kusaini petition kadhaa wakitaka Diamond afungiwe, Profesa Jay yeye anapiga show na vijana waCCM (Nandy, Diamond , Weusi nk). Wasanii ambao kwa mujibu wa Chadema ni moja ya watu waliotumika kuingiza mamlakani utwala dharimu wa CCM.

Wakati makamu mwenyekiti anatuma kwenye magrupu ya whatsapp watu washare katiba mpya, prof anaweka pembeni hizo post kisha anapost kwanza show zake, na kudharau maamuzi ya chama ya kuhusu suala la katiba mpya. Huu ukosefu mkubwa wa nidhamu wa Prof kkwa chama bila shaka unaashiria profesa anataka kwenda CCM kusimamimsha uchumi kwanza maana katiba mpya inaweza kusubiri.

Mimi binafsi naona Profesa Jay ni moja ya mfano mkubwa wa kuigwa kwa vijana. Maisha ya Profesa yanatufundisha kuwekeza sehemu nyingine pale tunapokuwa na nyadhifa za kisiasa ili siku unapozipoteza maisha yaendelee, Leo hii tofauti na Msigwa na Heche yeye maisha yake yanaendelea kama kawaida.

Unapokuwa umewekeza nje ya siasa maisha yanaendelea hata unapokuwa nje ya mfumo, yaani unalipa bili zako bila shida.
Karibu sana nyumbani Jay
 

wewe unavomuona professor jay ana akili mbovu kam hicho chama? wacha aende sehem zenye akili
 
Wote wasioheshimu haki za msingi za wengine iwe ni kwasababu ya mamlaka ama sababu nyingine zozote,hawafai kuwa rafiki wa mtanzania na taifa letu.Dawa kuponya maradhi haya Katiba mpya.
 
Siasa ni ajira, ukiona kampuni iliyokuajiri haina maslahi unafunga contract na kampuni nyingine yenye maslahi kwako. Hivyo Prof. Jay akihamia chama kingine tofauti na ChaDeMa sawa tu akiona hilo lina maslahi kwake.

Lakini pia hakuna cha kumzuia yeye kama msanii hata kama ni wa chama pinzani kufanya kazi za sanaa na wasanii wa chama tawala.
 
J hawezi kukaa na wahuni wa chadema lazima aje ccm
 
Nani kasema kwamba kila aliye inadi CCM ni msaliti??

Wasaliti Ni wawili tu! Diamond na Zuchu.

Hawa walikuwa wanaunga mkono wakati jiwe anatema maneno ya makufuru na kutesa watu. Wakampa sifa lukuki eti "nyoronyoro" baba lao.
 
Kwani Heche alishawahi kuomba hata sabuni ya kuogea???Acha kudharau watu wewe ni nani uone mtu kunyang'anywa ubunge basi hawezi ishi??Huu ndio ushenzi anaoukemea Fatma Karume tena ni ushenzi wa kijinga haswaa.
 
Hata mdude nyagali atahamia ccm kisha atapewa ujumbe wa barozi wa nyumba kumi. Nisuala la mdaa tuuuu.
 
Prof Jay ni matunda ya sera nzuri za CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…