Naona si sawa Kwa Wananchi kulalamika posho za watumishi na Viongozi Gavoo

Naona si sawa Kwa Wananchi kulalamika posho za watumishi na Viongozi Gavoo

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,850
Reaction score
6,030
Kwanini wananchi Huwa tunaumia bila sababu pale watumishi wa Serikali pamoja na baadhi ya viongozi wakiwa wanalipa posho.

Mimi naona asilimia kubwa ya watanzania ni wakulima na wafanyabiashara , na wateja wengi wa biashara zetu ni watumishi, mkisema wasipewe posho hayo maduka , na biashara mlizofungua nani atawaungisha.

Nafikiri jambo baya ni ufisadi na uwizi, lakini posho na kipato Cha mfanyakazi kunasaidia kukuza uchumi. Akipata kaposho ataenda nunua suruali, kanyama ka kakuku, Sasa akiishi Kwa bajeti biashara zutakufa na Kodi hamtalipa, Hawa watumishi halaf ni masikini wa kutupa, Huwa hata huwezo wa kuweka akiba ni mdogo au hawana.

Jiulize kwanini biashara nyingi wanauza sana mwisho wa mwezi, kama tunaamua pesa zisiende Kwa watumishi wazirudishe mtaani, basi serikali ikajengee Barbara halaf biashara zetu zife
 
Kwanini wananchi Huwa tunaumia bila sababu pale watumishi wa Serikali pamoja na baadhi ya viongozi wakiwa wanalipa posho.
Mimi naona asilimia kubwa ya watanzania ni wakulima na wafanyabiashara , na wateja wengi wa biashara zetu ni watumishi, mkisema wasipewe posho hayo maduka , na biashara mlizofungua nani atawaungisha.

Nafikiri jambo baya ni ufisadi na uwizi, lakini posho na kipato Cha mfanyakazi kunasaidia kukuza uchumi. Akipata kaposho ataenda nunua suruali, kanyama ka kakuku, Sasa akiishi Kwa bajeti biashara zutakufa na Kodi hamtalipa, Hawa watumishi halaf ni masikini wa kutupa, Huwa hata huwezo wa kuweka akiba ni mdogo au hawana.
Jiulize kwanini biashara nyingi wanauza sana mwisho wa mwezi, kama tunaamua pesa zisiende Kwa watumishi wazirudishe mtaani, basi serikali ikajengee Barbara halaf biashara zetu
 
Sidhani kama watu wanalalamika watumishi kulipwa posho za halali, watu wanalalamika wizi wa pesa za uma na ufisadi.

Posho zinaweza geuka wizi pale zinapotolewa kwa utaratibu usiofaa, mfano idara inabuni project feki watu wajichotee posho.,huo ni wizi wa pesa za wanaolalamika.
 
Yani Mimi Nina bar, nauza sana watumishi wakilipwa maposho, Tena kama kapata safari ya kikazi, wanakunywa Hennessy tu
 
Ni kweli lakini hii inasaidia kwa kiwango kidogo sana.
Wananchi ni wengi kuliko watumishi. Kwahiyo wananchi wakisema wategemee posho za watumishi haiwezekani.
Nadhani serikari hizo posho wangetumia kuwa wezesha wananchi kiuchumi.
Mfano, kujenga barabara maeneo ambayo hayana barabara bora, hii itasaidia wananchi kufanya shughuli za kiuchumi, kama kupata fursa, kujiajiri n.k
 
Back
Top Bottom