Naona Trump anaigeuza Marekani kuwa kama Ujerumani enzi za Hitler

def_xcode

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
2,551
Reaction score
6,837
1758181242318.png

Siasa za Marekani zimegeuka na kuwa kama za Afrika ndani ya muda mfupi. Bw. Trump kila ambaye anapingana naye basi anakuwa mbaya na waliomzunguka sharti kumsifia tu kama machawa. Siasa zimekuwa ni kuwatuhumu Demos ambao wengi wanakuwa referred kama the lefts na kila baya anawatuhumu wao

Zamani ilikuwa inasemekana kwamba Marekani unaweza kusema chochote ni freedom of speech, ila sasa serikali imewataka waajiri kwa mfano kuwafukuza watu walioonekana kushangilia kifo cha Charlie Kirk. Imetengenezwa tovuti ambapo yanawekwa majina ya watu walioongekana kufurahia kifo chake

Leo nimeona katangaza kuwa wako kwenye mpango wa kulabel wale wanaopinga Fascists kuwa nikundi cha kikagaidi jambo ambalo ni shambulio la moja kwa moja kwa Demos

Nimeona mkuu wa FBI ambavyo alikuwa anajibu hovyo na kuwakejeli members wa Congress. Yani mambo yanayoendelea ni kama sasa hivi Marekani hakuna tena checks and balance

Trump alianza kuwa haruhusu vyombo vya habari ambavyo vinamwandika vibaya kuingia kwenye press zake kitu ambacho kingefanywa na rais mwingine kama Obama kelele zingekuwa nyingi.
Ametishia kuwa New York kama wakimchagua mayor yule Mwislamu, hatapeleka pesa huko. Shambulio la demokrasia hili

Jana niliona mwandishi mmoja wa Australia anamuuliza vipi kuhusu tuhuma za yeye kufanya biashara ikulu, akamuuliza wewe unatoka wapi? Jamaa akamjibu Australia. Akamwambia unajua kiongoozi wako anakuja kuniona, unapaswa kuhakikisha mko vizuri na mimi, nitamwambia kiongozi wako kuhusu wewe.
Ingelikuwa zamani hii ingekuwa bonge la topic ila kwa trumo ni kama kila chombo kimepigwa ganzi.
Inavyoonekana kuna mpasuko mkubwa sana, hadi watu wanatangaziana vita mtandaoni kati ya lefts and right na wanatishiana hadi kuuana
 
So unaona ni jambo sahihi mfano kwa hapa Tanzania itokee kiongozi mfano wa CHADEMA,CUF au ACT amepatwa matatizo au kafariki halafu kiongozi wa serikalini aandike post mtandaoni kuwa anafurahia kifo cha huyo mtu na anaonyesha kutaka wafe au wauliwe wengine zaidi?

Hiyo kwako omekaa sawa,ni sehemu ya freedom of speech kuandika mambo ya kufedhehesha familia ya marehemu kwa kuwatusi na kuwakebehi kwa kunajisi jina la mpendwa wao ambae kauwawa kikatili bila hatia yoyote tena hadharani?🤔

Nadhani ifike muda tuanze kutumia akili badala ya hisia kwenye mambo ya msingi.

Mimi naunga mkono wanaharakati na serikali ya Trump kuwafukuza kazi na kuwaadhibu wote wanaofanya kebehi na dhihaka kwa kifo cha Charlie Kirk ambae hakuwa ni mtu mbaya kisheria ni vile tu maoni yake yake yalikinzana na upande wa Left wing Democrats ambao wanaendekeza mambo mengi ya kipuuzi kama ushoga, ubakaji, uhamiaji haramu, kutukuza na kuchekea wageni wanapodharau utamaduni wa Marekani, kupromote ngono kwa watoto na kupigia kampeni uhalali wa mafataki kulala na watoto wadogo wa kuanzia miezi hadi miaka 16.

Washenzi sana democrats.
 
Shida ni double standards, kuna kiongozi wa demo aliuawa na wao akina trump walikuwa wanashangilia tu na yeye trump anajifanya hamjui.
Na hao watu wengi ambao wanadai walishangilia, ukweli ni kwamba walikuwa wanashangilia kwa kupost yale mabaya aliyoyasema. Yani walikuwa wanaweka clip za vipande vya video ya yale aliyokuwa akiyasema.
Trump mimi namkubali kwa mambo mengine, ila siasa zake zinavunja mambo mengi ambayo kwa miaka mingi US ilikuwa ikiyasimamia.
Kwa mfano, walikuwa wanadhani aliyemuua Charlie atakuwa Demo, labda mwafrika au mwaarabu, wakawa wanasema apewe adhabu ya kifo, ajabu wakaja kukuta anatokea familia moja ya upande wao na hapo tone ikabadilika. Ikawa inapaswa kuombewa maana Charlie angependa hivyo japo bado wanajaribu kuonyesha kuwa jamaa ni left.
Siasa za US kwa sasa zimekuwa za kuligawa taifa kwa kiasi kikubwa sana. Nao wanafanana sisi. Siasa now zinakuwa uadui si tu wa kupigana kwa hoja, bali hata katika maisha ya kawaida. Na hii si kwamba wameanzisha republicans tu, niliona baada ya kamala kushindwa, lefts walikuwa wanajipost wakisema, nimeacha kuongea na ndugu zangu kwa kumchagua trump, mara nimeacha kuongea na rafiki zangu kwa kumchagua trump.
Kuna clips kibao za Obama alikuwa anakuwa challenged na maswali chokonozi lakini hakuwa anawafukuza waandishi, alikuwa anayaddress kitu ambacho kwa bwana Trump hawezi kukivumilia.
 
Tiwe w

Siasa za Marekani zimegeuka na kuwa kama za Afrika ndani ya muda mfupi. Bw. Trump kila ambaye anapingana naye basi anakuwa mbaya na waliomzunguka sharti kumsifia tu kama machawa. Siasa zimekuwa ni kuwatuhumu Demos ambao wengi wanakuwa referred kama the lefts na kila baya anawatuhumu wao

Zamani ilikuwa inasemekana kwamba Marekani unaweza kusema chochote ni freedom of speech, ila sasa serikali imewataka waajiri kwa mfano kuwafukuza watu walioonekana kushangilia kifo cha Charlie Kirk. Imetengenezwa tovuti ambapo yanawekwa majina ya watu walioongekana kufurahia kifo chake

Leo nimeona katangaza kuwa wako kwenye mpango wa kulabel wale wanaopinga Fascists kuwa nikundi cha kikagaidi jambo ambalo ni shambulio la moja kwa moja kwa Demos

Nimeona mkuu wa FBI ambavyo alikuwa anajibu hovyo na kuwakejeli members wa Congress. Yani mambo yanayoendelea ni kama sasa hivi Marekani hakuna tena checks and balance

Trump alianza kuwa haruhusu vyombo vya habari ambavyo vinamwandika vibaya kuingia kwenye press zake kitu ambacho kingefanywa na rais mwingine kama Obama kelele zingekuwa nyingi.
Ametishia kuwa New York kama wakimchagua mayor yule Mwislamu, hatapeleka pesa huko. Shambulio la demokrasia hili

Jana niliona mwandishi mmoja wa Australia anamuuliza vipi kuhusu tuhuma za yeye kufanya biashara ikulu, akamuuliza wewe unatoka wapi? Jamaa akamjibu Australia. Akamwambia unajua kiongoozi wako anakuja kuniona, unapaswa kuhakikisha mko vizuri na mimi, nitamwambia kiongozi wako kuhusu wewe.
Ingelikuwa zamani hii ingekuwa bonge la topic ila kwa trumo ni kama kila chombo kimepigwa ganzi.
Inavyoonekana kuna mpasuko mkubwa sana, hadi watu wanatangaziana vita mtandaoni kati ya lefts and right na wanatishiana hadi kuuana
Kwa kweli, Trump pamoja na ubabe wake, hajafikia tawala dhalimu kama za huku kwetu.

Utawala wa Trump haujawahi kuteka na kuua watu au kuwapoteza kama unavyofanya utawala wa mama. Wala haujawahi kumbambikia kesi kama unavyofanya utawala wa mama dhidi ya Lisu.

Trump ni mbabe wa maneno tu, na hiyo ndiyo siasa yenyewe, watu wanabishama kwa hoja.

Hilo kundi lililomwua Kirk, hata likiitwa la kigaidi ni sawa tu. Maana ya ugaidi, ni kufanya vitu vya mauaji ili kuwatisha watu fulani. Washindani wake walistahili kushindana naye kwa hoja, na siyo kumwua.
 
Hajauwawa na kundi la kigaidi, ni mtu mmoja.
20250918_130651.jpg
 
Tiwe w

Kwa kweli, Trump pamoja na ubabe wake, hajafikia tawala dhalimu kama za huku kwetu.

Utawala wa Trump haujawahi kuteka na kuua watu au kuwapoteza kama unavyofanya utawala wa mama. Wala haujawahi kumbambikia kesi kama unavyofanya utawala wa mama dhidi ya Lisu.

Trump ni mbabe wa maneno tu, na hiyo ndiyo siasa yenyewe, watu wanabishama kwa hoja.

Hilo kundi lililomwua Kirk, hata likiitwa la kigaidi ni sawa tu. Maana ya ugaidi, ni kufanya vitu vya mauaji ili kuwatisha watu fulani. Washindani wake walistahili kushindana naye kwa hoja, na siyo kumwua.
Mkuu si mbabe wa maneno tu, anawashughulikia, wanafutwa kazi, wanakamatwa. Sasa hivi katika utawala wa trump unaweeza kuwa una green card ikawa cancelled kwa post yako tu. Watu wamepoteza uhalali wa kuishi Marekani kwa post zao za kuonyesha wako upande mwingine.
Kila suala huanza taratibu na hajafikisha mwaka ofisini ila siaisa za US zimechukua sura mpya. Na si ndani ya US tu hata nje. Ni kama siasa za duania zimebadilika ghafla. Kule NATO nao wamegeuka machawa mwenyekiti anamwita dady.
Trump siasa zake ni kama za afrika. Wafanyabiashara wakiwa against naye wala hajifichi anawatisha hadharani. Uliona Musk alipompinga alisema nninaweza kuifanya Dodge ichunguze mikataba yake. Aliporudi umeona kwani kachunguzwa?
CEO mpya wa intel uliona alimtish, jamaa kaenda akazungumza naye na kumsifu lile tishio alilosema jamaa kuwa CEO wa intel ni national security akalifuta na kumwita ni mtu safi kabisa.
Yani siiasa zake ni kwamba ama unaniunga mkono ama ninakukanyaga. Unaona hadi ana kwenda after judges wanaotoa maamuzi ambayo hayapendi. Anafuata hadi vyombo vya kutoa statistics kama haziendani naye anasema ni takwimu za uongo anazignore, anaweka watu wake au anakuja na za kwake na watu wake ndizo zinakuwa takwimu rasmi.
Hizo ni siasa zetu huku Afrika.
 
Back
Top Bottom