Kama Harmonize na Wasafi wangekubaliana idadi ya nyimbo au albamu, wala wasingeingia kwenye mgogoro. Wangeachana salama. Kama kungekuwa na idadi ya nyimbo anadaiwa, Harmonize angeingia studio kumalizia. Miaka 20 au 10 ya nini? Saini idadi ya nyimbo, zikitimia, kama kuna haja, mnasaini tena.
Huyu jamaa mweupe sana kwenye tasnia ya burudani ingawaje mara kwa mara amekuwa akiandika!!!
Ukweli ni kwamba, HAKUNA MTAKABATA wa kutoa idadi ya nyimbo/album bila kutaja muda!!!
Mikataba inavyokuwa ni kwamba, mathalani utaambiwa "...5 Years Term" na ndani ya muda huo, Msanii atatakiwa awe ametoa idadi ya Album/Nyimbo X.
Na mara nyingi kama sio zote, nyimbo zinazozalishwa (known as Master Recordings) zinakuwa ni mali ya label unless otherwise stated. Kibongo bongo, rejeeni kesi ya Saida Carol na FM Studio (Mzee Mutta)!!
Sio Bongo tu, ni juzi tu hapa Taylor Swift aliandika:-
For years I asked, pleaded for a chance to own my work. Instead I was given an opportunity to sign back up to Big Machine Records and βearnβ one album back at a time, one for every new one I turned in. I walked away because I knew once I signed that contract, Scott Borchetta would sell the label, thereby selling me and my future. I had to make the excruciating choice to leave behind my past. Music I wrote on my bedroom floor and videos I dreamed up and paid for from the money I earned playing in bars, then clubs, then arenas, then stadiums.
Kwahiyo sentensi ya kwanza tu, unaona nyimbo alizokuwa anatengeneza Taylor zilikuwa ni mali ya Big Machine Records!!!!
Sasa ukitaka umiliki wa nyimbo urudi kwako msanii, hapo ndo pale unapopewa masharti! Kwa Taylor kwa mfano, yeye hata hiyo opportunity hakupewa lakini akaambiwa kama unataka, saini mkataba mpya na masharti yake itakuwa kila unapotoa album kwa ajili ya label, tutakupa fursa ya wewe kutoa albamu ya kwako!!
Na Taylor alifanya kazi na Big Machines kwa zaidi ya miaka 10, na ameondoka amesaini Universal mwaka jana tu hapa!!
Sasa tunaporudi kwa Harmonize, yeye alipewa fursa ya kutumia nyimbo zake alizotengeneza na Wasafi... atatumiaje, ndo hapo anavunja mkataba na kutakiwa kulipa 500M na hivyo kuwa na haki ya kutumia nyimbo zake!!!
Ni mwehu tu ndie anaweza kusema 500M ni pesa nyingi sana kwa level aliyofikia Harmonize na nyimbo alizotengeneza akiwa Wasafi! Pale alipo ana thamani ya zaidi 500M kama label mpya inaamua kumchukua!! Kwa maana nyingine, leo kwa mfano Sony wakisema wamchukue Harmonize, hawawezi kumpa chini 500M... NO WAY!!!