Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Amri ya tano, Waheshimu baba na mama upate miaka mingi na heri duniani.
Mbona me nawaheshimu sana tena sana kama kazi walizoniambia nifanye nafanya tena kwa moyo mmoja ila lipokuja suala la kufokewa na maza tena kwa sauti kubwa kwenye mambo madogo madogo kwangu mimi hili apana kwakweli nimevulimia sana ila naona imefika mwisho nahitaji kupata utulivu wa nafsi ndio maana nimeamua kuanza harakati za kutafuta chumba na niwaage kwa amani. Sasa hapo mkuu mimi kosa liko wapi au kuna sehemu gani mimi nimeonyesha zarau kwa wazazi
 
Habarini wakuu! Ni mimi kijana wenu humu jamiiforums nina miaka 21, kama mnavyojuwa umri huu bado nipo masomoni chuo flani hivi apa dar na bado nipo home.

Sasa tuludi kwenye mada, unajua nini hapa home sipaelewi sikuhizi nimekuwa nikichukiwa pasipo na sababu za msingi, hasa bi mkubwa amekuwa mtu wakunifokea fokea hadi majirani huwa wanasikia jinsi ninavyofokewa. Majuzi kati hapa niliambiwa sikuhizi hapo home sifanyi kazi na ninachelewa kurudi nyumbani, nikiwauliza wazazi wangu ni kazi gani wanataka mimi nizifanye hapa nyumbani naambiwa nioshe vyombo, mara nifyeke majani na mikazi mengine kibao.

Okay siku na kipingamizi kwasababu hawa ni wazazi wangu hivo ni wajibu kuwasikiliza na sio kwamba siku za nyuma nilikuwa sifanyikazi? Hapana ni kutokana na majukumu ya masomo huku chuoni yananibana sana hivo nakuwa mtu sio wakushinda nyumbani maana mda wote na huku chuoni huwa na baki mpaka saa 3 au nne usiku ndio narudi home. Nafanya hivi ili nikimbie majukumu ya nyumbani ila baadae nahisi wazazi wangu walinishukizia.

Anyway sasa kila nikifanya kazi za hapa nyumba bado maneno yanakuwa mengi mara uwambie urudie kuosha vyombo mara mbili wakati apo vyombo ushaosha na vinan'gaa bila shida , ukitoka hapo mara uwambiwe chooni unaachafua mara hausafishi mara unaingiza mchanga mara uwambiwe uliacha mavi leo asubuhi yaani maneno yanakuwa mengi halafu bimkubwa anaongea kwasauti kubwa hadi majirani wanasikia

Mimi hali hii sipendezwi nayo, naona wazazi wangu kama wameanza kunichoka, hapa nafanya mpango mwisho wa mwezi huu nichomoke hapa home najua mwanzo wa kujitegemea huwa mgumu ila potelea mbali siwezi kuendelea kukaa home huku nikidharirishwa na maneno ya bimkubwa.

Anyway natafuta chumba bei iwe 50k maeneo kuanzia ubungo kibo, kona mpaka kimara korogwe. Kama unaona au unasikia kuna chumba kinapangishwa maeneo hayo anipange sasa. Wakuu #natanguliza shukuran
kwa umri huo bado unastahili kufanya kazi za nyumbani japo sio kuosha vyombo,kufagia ndani au kudeki choo,labda kama unaishi wewe na wazazi tu nyumbani lkn km kuna watu wengine hapo nyumbani fagia uwanja,fyeka majani,punguza matawi ya miti km ipo ila kama hata hayo huwezi sawa hama lkn sio kuwakasirikia wazazi iyo ni mbaya sana...
 
Huu uzi japo ww mtoa mada unaumia mm huku nakufa mbavu..
Any way pole sana hata mimi nahisi nitakua mzazi mwenye ngenga(maneno maneno)
 
Sasa mkuu kama kula home nakula usiku tu nikirudi na kama kuwategemea wazazi basi ni sehemu ya kulala tu ila mengi najitahidi kujihudumia mwenyewe ila manyanyaso bado hayaishi.
Ni manyanyaso au kuhimizwa kuwajibika kama kijana uliyepo hapo nyumbani?
 
Malezi mazuri toka utotoni yanasaidia sana kupambana na changamoto ukubwani.
Nakumbuka Mother kipindi nasoma secondary school nilikuwa TV room naangalia lBonge la movie, mama aliponikuta naangalia TV mpaka usiku alizima na kuambiwa niende chumbani kulala, nilimind lakini hamna namna, sasa hawa vijana wetu wa sasa ukiwafanyia hivyo lazima aje kukuanzisha thread JF.
 
Yani umeona swala lako wewe na familia yako tena WAZAZI wako ndio litapatiwa suluhisho humu,acha akili za kijinga kijana huo ujana usikupeleke pupa hivyo,Mzazi ana wajibu wa kukuambia chochote ikiwa hakileti madhara kwako na sijaona sababu ya wewe kulalama humu kisa tu kuambiwa ufanye MAJUKUMU ya HAPO NYUMBANI,kabla haujawa na miaka mpaka leo wamepambana,wamekupigania vya kutosha mpaka sasa hapo ulipo,huna haja ya kulalama mtandaoni humu hakuna msaada mkuu.

Rudi tena kwa Mama kapige magoti kamuombe msamaha huwezi jua kuna kitu ulifanya ama yeye anahisi kuna kitu mbele huko utafanya ambacho si kizuri.Kama waliweza kugundua wakati wewe bado ni mtoto mdogo hujui kuongea,wewe ni KUCHEKA na KULIA pindi ukipata maradhi hata ya tumbo basi Mzazi anajua hata kama huja muambia.

Heshima iwafikie WAZAZI WETU WOTE haijalishi wametulea katika mazingira Gani.

Tatizo la vijana wa sasa tunapenda sana USASA maisha ya TV na MTANDAONI {GLOBALIZATION} angalia WAZAZI WETU pindi walivyokuwa na umri kama wako walikuwa wanapewa majukumu gani kwao kwa WAZAZI WAO.

AHSANTE.

Sent from my V2204 using JamiiForums mobile app
Hamna bana kuna wazazi wengine wanyanyasaji kweli...bullying their own children etc...
 
Nakumbuka Mother kipindi nasoma secondary school nilikuwa TV room lilikuwa na Bonge la movie, mama aliponikuta naangalia TV mpaka usiku alizima na kuambiwa niende chumbani kulala, nilimind lakini hamna namna, sasa hawa vijana wetu wa sasa ukiwafanyia hivyo lazima aje kukuanzisha thread JF.
Sijui ni utandawazi au malezi,,Mimi nimeshindwa kabisa kumuelewa kijana eti hataki kugombezwa....Binafsi nimeshuhudia Wazazi wangu baba ,baba wadogo,na mashangazi zangu wakienda ndivyo sivyo Bibi yangu alikuwa anawakalisha chini na anampa mtu risala,,,,na wazee wanakuwa humble wanaenda kulalamika pembeni .Hiyo tumerithi hadi watoto pamoja na ukubwa wetu mzazi akikoroma unakuwa mtiifu.Ngoja kwanza akafundishwe na ulimwengu
 
Waefeso 6:1-3
Waefeso 6:1-3

Watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa maana kufanya hivyo ni vizuri. 2 “Waheshimu baba yako na mama yako,” hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, 3 “upate baraka na uishi siku nyingi duniani.”
 
Pole sana ndugu!!

Kuna brother Ake mshkaji wangu hivi, alitimuliwa kwao kipindi ako na 15 yrs.

Mshkaji kimalezi hapo kwao aseee wameteseka vibaya mnoo na MTU aliyewatesa ni dingi yao kabisa.

Na huyo brother Ake kwa sasa Mungu amemjaalia kajipata ako vyema na biashara zake, jamaa anasema hana hamu na huyo dingi yao.

Jamaa anasema dingi yao hapo NYUMA alikuwa na hela sana sasa akajafilisiwa na ndugu zake kwahiyo madhila ameyarudisha Kwa watoto wake.

Kuna watu wanateseka mnoo Kwa wazazi wao, kama hujawahi pitia hizi mambo asee mshukuru sana Mungu wako Kwa kukupa wazazi wema.

Mo jitahidi asee uondoke Kwa wema hapo home, pia upambane upate ramani za kujishkiza kipindi unasoma Ili life lisikupige chenga za Lionel Messi.

Chukua hiyo changamoto kama chachu ya kufanikiwa kwako kama Christiano Ronaldo, wengi walioteseka makwao Mungu amewabariki sana katika maisha wako vyema sana kama Napaku wa Arusha.
Tukiwambia watu Kuna wazazi wanateza watoto wao Wana kataha


Mm mwenyewe nilioyapitia kwa kaka angu siwezi sahaugi nakikumbuka nalia kbsa

Ila SAS nimetuliaa nimekuwa kma adui SAS Sina hamu nae
 
Tukiwambia watu Kuna wazazi wanateza watoto wao Wana kataha


Mm mwenyewe nilioyapitia kwa kaka angu siwezi sahaugi nakikumbuka nalia kbsa

Ila SAS nimetuliaa nimekuwa kma adui SAS Sina hamu nae
Umeandika kwa hasira mpk mwandiko umechanganywa
 
Waefeso 6:1-3

Watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa maana kufanya hivyo ni vizuri. 2 “Waheshimu baba yako na mama yako,” hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, 3 “upate baraka na uishi siku nyingi duniani.”
Kwani amesema awaheshimu ?au wao ndio Wana msakama kila siku na kumfanya ashundwe kujiamini Hadi anambiwa kak mudi kaoshe vyombeee na nk .....
Dr vip ....
 
Back
Top Bottom