Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Vyombo sio kwamba sioshi mkuu!! Vyombo naosha sema maza bado atakufokea mara huoshi vyombo vizuri mara vyombo utavivunja unavibamiza kwa nguvu yaani maneno ni mengi
Mmh huyu sasa kazidi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Una uhakika ni mama mzazi kweli???
 
tabia yako au tabia zenu watoto mliozaliwa kuanzia 1995 ni ovyoo sana wazazi wameisha kata tamaa na tabia zenu mnakaa kuiga wasanii mnaona ndio njia bora ya kuishi kumbe mzazi hapendezewi na tabia zenu mimi kama mzazi natamani muondoke mkaishi huko mnapojua nyinyi
 
Sasa pokea ushauri huu,sema na wazazi wako uwape ukweli wako wote,pia timiza wajibu wako vizuri tu na wazazi wako watakuheshimu tu
 
Wewe barehe inakusumbua na inaonekana una kiujinga Fulani hivi(sorry). wasikilize wazazi wako dogo utakuja kujuta, wewe unadhani kusoma ndo iwe sababu ya wewe kushindwa kusaidia kazi za nyumbani mpaka ulazimishwe?

Kwanza hapo kwenu hakuna kazi, yaani kuosha vyombo na kufyeka majani nayo kazi? Sisi wenzako tulikua tukitoka shule jioni tunapitiliza shambani kwenda kulima, na usijifanye eti Leo nimechelewa kutoka shule, utaikuta nafasi Yako ya kulima umeachiwa ipo inakusubili!!

Kwanza kazi nyingine sio mpaka uambiwe, kwa hiyo wewe unataka ukute chakula mezani tu unakula na kwenda kulala? Kazi hutaki? Njoo uishi kwangu uone kama hujatimka ndani ya siku mbili tu dadeq
 
Pole sana kuna wazazi na walezi wengine huchangia kuharibu watoto manyanyaso yanakuwa mengi mm nishawahi ishi maisha kama hayo nilivumilia mpaka muda ulipofika nikaondoka.
Mkuu usimjaze ujinga huyo dogo hataki kazi! Awe makini tu asije akawa choko. Mimi siku zote ninaamini mzazi hawezi kumnyanyasa wanae labda kama huyo mzazi ana matatizo ya akili.

Waswahili walishasema usie funzwa na ***** Dunia itamfunza.
 
Matoto ya siku hizi ndio maana mengi yanakua machoko, Mzazi ukiingia tu kwenye mtego wa kumlea mtoto anavyotaka basi ujue umesha mharibu mtoto. Yaani dogo analalamika eti kuosha vyombo? Kufyeka majani ya uwani? Kusafisha vyoo? Kusafisha uwanja?

Una miaka 20 alafu kazi kama hizo unataka mpaka mama akufokee ndo ukazifanye tena kishingo upande? Kweli? Wadau nao mna muunga mkono??
 
 
Mkuu, kwanza nisamehe kama tafsiri iliyokuja kwako ni kuwa nakutishia maisha.

Pili, naomba nikutakie heri katika huo uhamuzi wako.
Mpaka hapo sie tushajua kwa Nini mama yake anamfokea! Kiufupi dogo pasua kichwa, na siku akiondoka hapo home bibi mkubwa wake atachinja kuku na kujipongeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…