Naondoka mkoa X baada ya Mkuu wa Mkoa mpya kuwa kilaza na alikuwa classmate wangu

Tajiri wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2022
Posts
1,079
Reaction score
2,947
Hivi itakuwaje mtu ambaye alikuwa kilaza na mshika mkia darasani kwenu akuongoze wewe? Hiki ndicho kilichotokea baada ya mkuu wa mkoa hapa mkoani kwetu kuchaguliwa au kuteuliwa wakati yeye alikuwa kilaza wa kufa mtu darasani kwetu na yeye alikuwa anatokea mostly kumi mbaya za mwisho kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa.

Siwezi kuvumilia kuongozwa na kilaza mie na baada ya kuona kwamba huyu kilaza anakuja mkoani hapa nilimwandikia meseji ya kwamba mimi naondoka hapa mkoani kwasababu yako haiwezrkani kilaza wewe uje uniongoze nikamaliza.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Huo ni ujinga tu. Unatakiwa kufahamu kuwa hakuna uhusiano wa moja Kwa moja kati ya kufanikiwa darasani na kufanikiwa kwenye maisha halisi.
 
Sio Tu Hekima ya Uongozi na Hekima ya maisha kiujumla,,,Kusoma na Hekima ni Vitu viwili tofauti,,Hekima haikupi usomi,,na Usomi Haukupi Hekima na haimaanishi pia ukiwa umesoma ndio una hekima,,au ukiwa hujasoma ndio huna Hekima,,,unaweza ukawa na vyote,,ukakosa vyote,,au ukijaaliwa kimojawapo Kati ya hivyo,,Maisha kuna wakati yanahitaji Hekima,,, Maisha kuna wakati yanahitaji Usomi,,kuna wakati yanahitaji vyote viwili,,na kuna wakati pia hayahitaji vyote viwili!!Mtoa Mada badala amtumie klasimeti waunde comb ya Hekima na Usomi ili maisha yapate kwenda yeye analeta Chuki,, Wivu,,,dharau za kipuuzi,,kisirani na roho mbaya ambayo kimsingi hazileti ugali mezani wala pesa mfukoni nk
 
Hauko sahihi hata kidogo Mkuu, mh.Mkuu wa Mkoa sio mtu mdogo na kumbuka raisi wa nchi hii amemuamini na hizi joking zako hazita kufikisha kokote,ukibaki huo Mkoa ur will enjoy mema ya nchi Kanisa.
All the best huko unakokeenda na mwache Mh.mkuu wa Mkoa aje kufanga kazi Ili alete maendeleo kwa wananchi.
 
Mkuuu usiwe na hasira kihivyo, bakia tu hapo hapo ukiendesha maisha yako. Hivi ulikuwa hujuwi vilaza wengi ndiyo wanaongoza jamii hapa Afrika na wanaaminiwa sana na jamii. Vilaza mashuhuri ni manabii wa kisasa, wachungaji, maustadh, masheikh. Hawa maisha yamewashinda wamejikita kwenye dini kutafuta ulaji toka kwa kondoo wao.
 
[emoji23][emoji23]
Atakufuata huko huko uliko hamia, na gharama za kuhama sio zake wewe unahama kwa gharama zako
 
Kwanini ww usiwe zaidi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…