jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 36,197
- 29,717
Nimepita maeneo ya mianzini jijini Arusha kuna kampeni ya chini kwa chini yenye kupeana hamasa kuwa wanachadema asilia waliojitolea kupigwa risasi na mabomu pale Soweto kwa ushawishi wa Ufuasi wa Slaa.
Sasa wameweka nadhiri kuwa watahama na kumfuata kokote mpendwa wao Dr Willy Slaa ambaye ni baba wa vita dhidi ya ufisadi Tanzania.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA.
Sasa wameweka nadhiri kuwa watahama na kumfuata kokote mpendwa wao Dr Willy Slaa ambaye ni baba wa vita dhidi ya ufisadi Tanzania.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA.
Sababu kuu ni hii, Slaa amejitahidi sana kukijenga CHADEMA, na sio siri CHADEMA imekuwa na nguvu sana baada ya ujio wa Slaa, kama lilivyo jina CHADEMA ni chama cha demokrasia, lakini demokrasi inaanza kutoka na ubabe unaingia.
Kulikuwa na wagombea walitakiwa kuchukua fomu za urais kisha kura za maoni zipigwe hilo limekufa, Lowassa kaja kabaka demokrasia kwa kusema anataka yeye tu apitishwe bila kupingwa, swali langu ni hili kama yeye Lowassa ana mvuto na wafuasi wengi anaogopa nini kupambana na wengine kwenye kura za maoni?
Kwa mtu mwenye uchungu wa nchi huwezi kuanza kumsafisha mtu ambaye hajajisafisha bado, kuna watu wanasema Lowassa katubu, kutubu nijuavyo mimi unakubali kosa kwamba ndio ulifanya kisha unaomba msamaha, lakini Lowassa hajafanya hilo ila amekana hahusiki na lolote analoulizwa, ikiwa hali ya kukana jambo ni kutubu mafisadi wote watakuwa wametubu maana wote wana tabia ya kukana,
Wabunge wengi wa CHADEMA wamekuwa wakijitahidi kujenga hoja na kuongea na waandishi wa habari kwa lugha nzuri, misingi iliyowekwa na watu kama kina dr. Slaa, lakini leo anakuja Lowassa anaulizwa swali anasema "shut up", "keep quite" haya ni majibu ya hasira na kutisha watu ambayo hayakuwepo CHADEMA, lugha hii anaitumia kwa sababu yuko CHADEMA na watu wanashangili ila angesema maneno haya akiwa CCM angetamani ardhi ipasuke.
Hii inanikumbusha mchezo wa redio wa mzee Jangala na mwanae Mshamu, Mshamu anasema "dingi noma hivyo" kwa sababu Jangala hajui maneno ya kihuni anamsifia mtoto wake kwamba anaongea kiingereza kigumu.
CHADEMA wanasema system ya CCM ndio inawafanya watu wawe mafisadi na Lowassa katoka hiyo system na sasa atafuata system ya CHADEMA na UKAWA, lakini kabla hata ya wiki CHADEMA na UKAWA wanafuata system ya Lowassa kwa kuondoa wagombea wengine ili Lowassa apite bila kupingwa na hili ni sharti alilototoa Lowassa, system ikapindwa.
Dr. Slaa, tunakuomba uwatendee haki wananchi kwa kuanzisha chama kipya cha siasa. Sioni chama chochote cha siasa ambacho Dr. Slaa anaweza kujiunga nacho. Siyo CHADEMA ambao wameamua kumsaliti Dr. Slaa ambaye alihatarisha maisha yake na familia yake na wengine kukipa CHADEMA heshima iliyopata kabla ya ujio wa Lowassa. Dr. Slaa pia hatakiwi kujiunga na CCM, wala ACT, wala CUF, wala NCCR mageuzi wala chama chochote cha siasa.
Kitu pekee anachoweza kufanya Dr. Slaa ili kuwatendea haki wananchi watanzania ambao wanadhamira ya kweli ya kupigana na ufisadi kwa dhati kabisa ni kuanzisha chama kipya cha siasa. Hata kama Dr. Slaa ataanzisha chama chake baada ya uchaguzi mkuu itakuwa ni vizuri mno. Ukweli ni kuwa uongozi wa Dr. Slaa akiwa na chama chake cha siasa unahitajika sana ili wananchi waliopondeka moyo kwa unafiki wa CHDEMA na UKAWA wapate pa kujisitili.
Madonda na makovu ambayo CHADEMA kwa kughilibiwa na UKAWA wameyacha kwa wananchi wapenda haki ni makubwa mno. Njia ya pekee ni kwa Slaa kuanzia chama kipya cha siasa. Kiukweli CHADEMA wamemfanyia Dr. Slaa na wapenda haki wote kitu kibaya mno. Binafsi nimesononeshwa sana.