Naondoka na Slaa kampeni ya CHADEMA Asilia!

Naondoka na Slaa kampeni ya CHADEMA Asilia!

hahahahahaha It's too late nyie masisiemu..

Mnataka aanzishe ili agawe kura sio?? Subirini hiyo tarehe 8 siku EL anatangazwa, mtashangaa msiamini kitakachotokea..

Hapa mnachezeshwa mziki msiouelewa, mkija kujua dancing steps ngoma ni saa 11 disco lishaisha teh teh teh

Kaeni hapo...
 
dr slaa akiondoka maana yake hesabu hazikuzingatiwa kabla ya kumkaribisha lowasa..... Tumesisitiza kumuunga mkono lowasa kama viongozi wetu wakuu wote wamekubali kwa dhati hesabu zimezingatiwa....kinyume na hapo sitounga mkono maamuzi haya.....

nakubaliana na wewe, hesabu hazikufanyika kisawa sawa. Kwa nini lowasa akatae kumkaribisha lowasa?
 
hahahahahaha It's too late nyie masisiemu..

Mnataka aanzishe ili agawe kura sio?? Subirini hiyo tarehe 8 siku EL anatangazwa, mtashangaa msiamini kitakachotokea..

Hapa mnachezeshwa mziki msiouelewa, mkija kujua dancing steps ngoma ni saa 11 disco lishaisha teh teh teh

Kaeni hapo...
Tatizo hata hukusoma nimeandika nini. Nimesema aweza kuanzisha chama kipya baada ya uchaguzi mkuu.
 
Mkuu unataka tuwe na vyama kama vioski? Au vyama kama UPDP ya Dovutwa?
Uongozi wa Dr. Slaa ni wa principles. Chama atakachoanzisha kitafuata principles, siyo CHADEMA bila hata aibu wanakiuka principle yao kuu ya kupigana vita dhidi ya ufisadi.
 
Wachochezi tu nyie, hamna lolote, kama viongozi wa CHADEMA akiwemo Slaa wamekubaliana kumpokea LOWASSA nyie mna nini cha kuwaambia wananchi?
CHADEMA wamefanya kitendo cha ki - UNGU kumpokea LOWASSA aliyenyanyaswa vya kutosha na mfumo kandamizi, pia akapokwa haki yake na KITENGO ambacho hakiko kisheria! Sasa ukisema mambo ya kuondoka CHADEMA wakati huu ambapo neema imewazukia kila mtu anakuona wa ajabu! Tulieni LOWASSA achukue Nchi Kwanza!!!

user-online.png
Dr.W.Slaa

Today 06:20
#1
JF Senior Expert Member
verified.png
Array


Join Date : 1st July 2008
Posts : 681
Rep Power : 0
Likes Received1360
Likes Given282


[h=2]
icon1.png
Re: Dr. Slaa kuwasilisha leo mpango mkakati wa ushindi mbele ya Sekretarieti[/h]
Yericko,

Siasa ya unafiki sipendi. Nimenyamaza lakini naona mnazidi kunichokoza. Ni afadhali mngelikaa kimya kama nilivyonyamaza mimi. Uwongo wowote na upotoshwaji wowote sitauvumilia. Nitaukanusha hapo hapo. Hata kama una lengo lako ambalo silifahamu naomba sana usitumie jina langu. Nimefundishwa uwongo ni dhambi siko tayari kushiriki dhambi hiyo.

sina kikao chochote cha Secretariat sina mpango wowote ninaopanga kuwasilisha popote. Naomba watanzania wapuuze propaganda zote zinazofanyika kwa jina langu.

Ningehitaji kutuma taarifa yoyote kwa umma ningeliita Press Conference Mwenyewe au ningelitumia utaratibu wowote uliouliozoeleka.

Naomba kutoa onyo kwa mtu yeyote awaye, matumizi ya jina la Dr Slaa yakome.​


 
Wachochezi tu nyie, hamna lolote, kama viongozi wa CHADEMA akiwemo Slaa wamekubaliana kumpokea LOWASSA nyie mna nini cha kuwaambia wananchi?
CHADEMA wamefanya kitendo cha ki - UNGU kumpokea LOWASSA aliyenyanyaswa vya kutosha na mfumo kandamizi, pia akapokwa haki yake na KITENGO ambacho hakiko kisheria! Sasa ukisema mambo ya kuondoka CHADEMA wakati huu ambapo neema imewazukia kila mtu anakuona wa ajabu! Tulieni LOWASSA achukue Nchi Kwanza!!!

Umemaliza kabisa,japo nilikuwa natofautiana na ww kwenye maeneo mengi huko nyuma,sasa mekusoma.
 
Koho koho koho koho koho koho.
Moshi wa siasa ni majanga majanga tu.
 
Wachochezi tu nyie, hamna lolote, kama viongozi wa CHADEMA akiwemo Slaa wamekubaliana kumpokea LOWASSA nyie mna nini cha kuwaambia wananchi?
CHADEMA wamefanya kitendo cha ki - UNGU kumpokea LOWASSA aliyenyanyaswa vya kutosha na mfumo kandamizi, pia akapokwa haki yake na KITENGO ambacho hakiko kisheria! Sasa ukisema mambo ya kuondoka CHADEMA wakati huu ambapo neema imewazukia kila mtu anakuona wa ajabu! Tulieni LOWASSA achukue Nchi Kwanza!!!

Hili bonge la mchumia tumbo. Hili jitu nikikumbuka post zake na wenzake Ritz naLizabon. Kumbe ni jitu la hovyo flani hivi.
 
Ukweli kuhusu Dr.Slaa
AN Chilongola (LLM)

Taharuki imetanda juu ya wapi alipo Katibu mkuu wa Chadema Dr.Wilbroad Slaa. kila mtu anazungumza lake kwa kadri anavyoelewa. wengine wakisema yupo kwenye maandalizi ya vikao vya kamati kuu na wengine wakisema amejificha kwa sababu hakubaliani na maamuzi ya kumleta EL kwenye chama.

Mimi kama kada wa chadema wa muda mrefu na mwanasheria mzoefu nimefanya utafiti na nimejiridhisha bila shaka yoyote kuwa hali si shwari ndani ya chadema licha ya juhudi mbalimbali zinazofanywa kuonesha kuwa hakuna tatizo.

Ukweli ni upi? Ukweli ni kuwa Dr.Wilbroad Slaa hakubaliani na maamuzi yaliyofanywa na kamati kuu ya Kumleta EL na kumpa nafasi ya kugombea Urais bila kufanya utafiti wa kutosha. Slaa anadai kuwa maamuzi haya ni ya haraka mno na chama kilitakiwa kijitafakari zaidi kabla ya kumpa ridhaa ya kugombea Urais.

Ikumbukwe siku ya jumapili tar.26 wakati UKAWA wamefanya kikao cha mwisho na EL Dr.Slaa alikuwepo na baada ya hapo akapotea kabisa na hajaonekana hadharani hadi leo.

Ukweli ni kwamba ndani ya kikao kile chs jumapili Slaa alionesha msimamo wake juu ya EL na kudai kuwa watanzania hawatatuelewa wakituona tukipita kumsafisha mtu yuleyule tuliyemchafua awali.

Hivyo Slaa akatoa masharti mawili makubwa. La kwanza ni EL aitishe Press na ajisafishe mwenyewe kabla hajatangaza kuja UKAWA. Aruhusu waandishi wamuulize maswali yote kuhusu Richmond na kashfa nyingine ikiwemo umiliki wa jengo la Ubalozi wa S.Africa na EL ajibu hoja zote kwa maelezo ya kueleweka. Sharti la pili la Slaa ni kuwa EL asupewe nafasi ya kugombea urais kwa sasa kwani ni ngumu kupima dhamir yake kama ni ya kweli. Slaa akapendekeza EL aje CHADEMA na aisaidie UKAWA kuchukua dola bila kugombea Urais.

Lakini Mbowe akampinga sana Slaa na akasema Katibu mkuu hawezi kuweka "ultimutum" ya EL kujiunga na chadema. Mbowe akapuuza mawazo ya Slaa na akaagiza mchakato wa kumpokea uanze mara moja na kesho yake Mbatia akaambiwa atoe tamko la kumkaribisha EL UKAWA.

Hali hii ilimfanya Slaa kujihisi mnyonge na aliyepuuzwa. akahisi hathaminiki ndani ya chama licha ya mchango mkubwa alioutoa kukijenga chadema. jambo la ajabu Mbowe alipopelekewa taarifa hizo alijibu kwa kejeli kuwa liwalo na liwe. yani yuko tayari kumpoteza Slaa na kumkumbatia EL.

Haikujulikana wazi Mbowe ana maslahi gani katika hili la EL na kwanini aamue kuwa na msimamo mkali hivyo wa kumtetea EL.

Inadaiwa tangu jumapili Slaa alipoachana na viongozi wenzie wa UKAWA hadi sasa yupo ndani hajatoka na hakuna mgeni anayeruhusiwa kumuona. Anautumia muda huu kusali na kushauriana na marafiki zake kwa njia ya simu (wengi ni maaskofu) juu ya nini afanye katika kipindi hiki.

Wengi wamemshauri aachane na siasa na ajiuzulu nafasi yake ya SG ndani ya chadema wazo ambalo limeungwa mkono na mkewe Josephine na baadhi ya watu wenye misimamo mikali.

Baada ya ushauri huu mkewe wa Slaa ameonekana kufurahia na ameanza kuelezea kwenye mitandao ya kijamii. Jsna kupitia kundi la Nyakahoja la whatsapp Josephine alisema mumewe ameteseka sana na chama hiki na amekitoa mbali sana. Dr.Slaa alivunjika mkono na hadi sasa ana ulemavu wa kudumu kwa sababu ya kuitetea chadema. yeye mwenyewe alipigwa na kuharibiwa mimba mwaka 2011 kwa sababu ya chadema halafu leo wanapuuzwa kama vile si chochote ndani ya chama.

Anasema ni afadhali Mbowe angesikiliza ushauri wa Slaa wa EL kujisafisha kwanza kabla hajaja chadema maana kuja bila kujisafisha ni kuwaweka viongozi wote wa chadema kwenye mtego.

Madai ya Mbowe kupewa fedha na EL. Yapo madai kuwa Mbowe amehongwa sh. bil 12 ili kumpokea EL. Fedha hizi ameziweka kwenye akaunti yake binafsi na amewawia kidogo wale aliowaona wanaweza kumchallenge. baadhi ya watu waliopata mgao ni wajumbe wa kamati kuu ili kuwaziba mdomo. na si wajumbe wote bali wale wachache viherehere. baadhi yao ni Godbless Lema (anadaiwa kupokea milioni 120), Peter Msigwa (mil 135), Tundu Lissu (mil 180), Salum Mwalimu (Mil 180).

Pesa hizi ndizo zinazodaiwa kuwafumba macho kamati kuu na kuamua kumpitisha EL bila kufikiri mara mbili. Kitu cha ajabu kamati kuu imefunga dirisha la kuchukua fomu na kusema eti kamati kuu inamuunga mkono Lowassa tu.

Huu ni ujinga ambao hata CCM haiwezi kuufanya. Kamati kuu inatakiwa kuwa neutral. kamati kuu haitakiwi kuwa na mgombea. kamati kuu haitakiwi kuzuia watu kuchuku fomu. acha wachukue wengi kadri iwezekanavyo halafu wachujwe abaki mmoja.

Kama EL anajiamini yeye ni bora zaidi na ana nguvu zaidi kwanini anaitumia kamati kuu kuzuia watu wasichukue fomu? Siku chache zilizopita watu walilalamikia kamati kuu ya CCM kuwa ilikua na mgombea wake mbona hawaoni hili la kamati kuu ya chadema?

Ikiwa madai haya ya kuhongwa kamati kuu ni ya kweli basi chadema inaelekea ukingoni katika siasa za nchi hii. jambo la ajabu viongozi wanaodaiwa kuhongwa akiwemo Mbowe hawajakanusha habari hizi. halafu wanatuma ujumbe kw Slaa eti wakamsihi asiondoke. wajumbe wote waliotumwa wakaishia getini na hawakufunguliwa mlango. mlitegemea mfunguliwe mlango wakati kuna madai mmehongwa na hamjakanusha? kanusheni kwanza ndio muende kumuona Slaa. Au mnataka mkamhonge na yeye? Kama msipokanusha habari hizo mkienda mtafungiwa tena nje maana nyumbani kwa Slaa hakitaingia chochote kilicho kichafu.

Response ya Chadema. ni kama vile hawajali yanayoendelea. na bahati mbaya zaidi vijana wa chadema wameanzisha movement ya kumtukana Josephine kuwa yeye ndio anamponza mumewe. kwenye mtandao wa jamiiforums, facebook ma magroup ya whatsapp wanamtukana sana.

kwenye group moja la wabunge wa chadema wameanzisha movement iitwayo "Josephine Bring Back our Dr". wengine wanamwita mwanamke mpumbavu, wengine wanasema ana hasira ya kukosa ufirst lady, lakini wengine wamefika mbali na kudai anatumiwa na TISS na CCM.

Kimsingi madai yote hapo juu hayana mashiko. Josephine hatumiwi na TISS wala CCM. Hana uchungu wa kukosa ufirst lady wala nini. anachofanya ni kutetea haki ya mumewe. haki ya kuthaminiwa, haki ya kuheshimiwa, haki ya kutoa mawazo yake na kusikilizwa.

Hivi mumeo anapuuzwa kwenye vikao vikubwa vya maamuzi halafu unaambiwa waliompuuza wamehongwa fedha na hawajakanusha habari hizo, halafu ukimtetea mumeo unaambiwa unatumika na TISS. this is ridiculous.

Hakuna cha TISS wala CCM mchawi wa chadema ni chadema wenyewe na mchawi wa ukawa ni chadema. Hizi porojo za TISS ni mbinu inayotumika ili Slaa akiamua kutangaza msimamo wake ionekane anatumiwa na CCM. Chadema acheni siasa za kitoto. hivi Slaa aliyepigania chadema zaidi ya miaka 20 akitoa sadaka maisha yake kwenu ndio wa kutumika na TISS leo aache kutumika huyo EL aliyekuja jana? this is very interesting. chadema kitaingia katika rekodi za dunia za kuwa chama cha kwanza kumtilia shaka mwanachama wake wa miaka 20 na kumuamini mwanachama wa siku moja.

Nini kifanyike? Jambo linaloweza kufanyika na kusaidia kuiokoa chadema na UKAWA kwa ujumla ni mediation. zitafutwe mbinu nzuri za kukutana na Slaa na kuongea nae. aeleze yanayomhusu na chama kioneshe concern ya kuyatatua.

pia kwa kuwa Josephine anaonekana kuwa na nguvu kubwa sana kwa Slaa hivi sasa ni bora Watafutwe wanawake wenye heshima ndani ya chama wakaongee nae. kwa mfano Mama Regina Lowassa, mama Ntagazwa na mama Mbatia waende kumuona mwanamke mwenzao waongee nae. hii itasaidia kupunguza hasira za huyu mama maana tangu juzi anatukanwa mitandaoni akidaiwa ndiye anayemzuia Slaa.

Ni vizuri mambo haya yafanyike mapema maana taarifa zilizopo ni kuwa kufikia wiki ijayo kama chama kitakua hakijatoa msimamo kuhusu Slaa basi yeye atatangaza msimamo wake wa kujiuzulu wadhifa wake chadema na kuamua kuachana na siasa kabisa. kisa wataondoka nchini yeye na familia yake kwenda Italia ambapo ataishi huko kwa miaka mitano kabla ya kurudi nchini na kumalizia maisha yake Karatu. mipango ya Slaa kwenda kuishi Italia kwa miaka mitano inaratibiwa na shirika mija la kiroho la kanisa katoliki na maandalizi yanaendelea vizuri.

Hivyo basi ni vema kazi hii ikafanywa mapema na kwa umakini ili tusivuruge kazi yote ya kuijenga Ukawa na kuujenga upinzani nchini. ukweli ni kuwa Slaa akiamua kujiuzulu siasa za upinzani zitapoteza uelekeo na tutashindwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu kuanzia udiwani, ubunge hata urais. maana yake ni kuwa kazi yote iliyofanyika kuujenga upinzani inabomolewa siku moja na kuifanya CCM izidi kushamiri. na ikiwa Slaa ataondoka itachukua miska zaidi ya 100 kupata upinzani mwingine wenye nguvu kama huu. hivyo basi juhudi za haraka zinatakiwa.

Mwandishi wa makala haya ni ndugu A.N Chilongola, mwanachama wa chadema na mkurugenzi wa kampuni ya uwakili ya Chilongola &Advocates iliyopo Mabibo Dar.[truncated by WhatsApp]
 
Msipuuze mawazo ya watu bali mawazo hayo yawasaidie kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kifikra,kimtazamo,kimaamuzi,kujenga hoja na kukataa au kukubali jambo fulani.
 
Wachochezi tu nyie, hamna lolote, kama viongozi wa CHADEMA akiwemo Slaa wamekubaliana kumpokea LOWASSA nyie mna nini cha kuwaambia wananchi?
CHADEMA wamefanya kitendo cha ki - UNGU kumpokea LOWASSA aliyenyanyaswa vya kutosha na mfumo kandamizi, pia akapokwa haki yake na KITENGO ambacho hakiko kisheria! Sasa ukisema mambo ya kuondoka CHADEMA wakati huu ambapo neema imewazukia kila mtu anakuona wa ajabu! Tulieni LOWASSA achukue Nchi Kwanza!!!

Ukiwasikiliza hawa wanafiki wa ccm na wafuata bendera wasiojitambua hutafikia malengo na mategemeo hata siku moja. Siku zote siasa ina hesabu zake na sayansi yake. Na sio kila mchango wa wachangiaji una nia nzuri kwa ukawa kwa mafanikio yake. Wala sio kila mmoja ana uwezo wa kufanya siasa.Wengi wamesahau uamuzi wa kumteua Lowassa kupeperusha bendera ya uraisi kupitia ukawa ni uamuzi wa viongozi wa vyama vyote vinavyounda ukawa baada ya kupata ridhaa ya kamati kuu za vyama hivyo.

Baada ya maridhiano ya vyama vyote hivyo na kwa idhini ya kamati kuu zao wakakubaliana chadema watoe mgombea uraisi na ni lazima mgombea mwenza kwa katiba ya nchi atoke visiwani tena awe wa chama kinachomsimamisha mgombea uraisi ambao ni chadema. Kwa kuwa chadema hawawezi kumpata mgombea mwenza huko c.u.f. watamteua na atajiunga chadema kukidhi masharti ya sheria. Lowassa kwa sasa ni mwanachama wa chadema. Halimashauri kuu ya chama hicho ikihudhuriwa na wajumbe wahusika wote akiwepo na katibu mkuu Wilbrod Slaa katika kumtafuta mgombea uraisi kwa nafasi waliyopewa na ukawa walikubaliana kumsimamisha Edward Lowassa.

Katika kufikia uamuzi huo walirejea adhma na malengo yaliyounda ukawa kuwa ni kuitoa ccm madarakani na mfumo wao kwanza mengine yatafuata. Pia waliuona mtaji watu wengi watakaomfuata Lowassa ambao zote hizo ni kura kwa chadema na ukawa. Rejea hotuba ya m/kiti wa chama akimtambulisha Lowassa. Hivyo kwa pamoja na kwa hoja hizo wote walikubaliana kumsimamisha Lowassa kama mgombea uraisi. Sasa yeyote alieshiriki maamuzi hayo akirudi nyuma au kususa makubaliano hayo atakuwa na yake na wote mnalijua jina la mtu wa hivyo. Ukitaka kuelewa upenzi wa Lowassa kwa watu amepata udhamini wa zaidi ya watu 1600 wakiwa na kadi zao za kupigia kura wakati waliotakiwa ni 200 tu. Naomba katika hili tuwe wamoja na kutokuweka maslahi binafsi mbele.
 
Jaman niulize kiswali kwan chadema ni chama cha wachaga au maana wengi ninaowaona ni wachaga tukiwapa wachaga c ndo kila seckita ngazi za juu watakuwa wachaga tuuuu

Wapige vita kivyengine sio kwa njia hii ni hatari sana mkuu (ukabi.......) utatuweka tusikokutarajia.
 
Mleta mada wewe ni ccm, usijifanye leo ndo unampenda slaa. Toka pepo!
 
Back
Top Bottom