Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wachochezi tu nyie, hamna lolote, kama viongozi wa CHADEMA akiwemo Slaa wamekubaliana kumpokea LOWASSA nyie mna nini cha kuwaambia wananchi?
CHADEMA wamefanya kitendo cha ki - UNGU kumpokea LOWASSA aliyenyanyaswa vya kutosha na mfumo kandamizi, pia akapokwa haki yake na KITENGO ambacho hakiko kisheria! Sasa ukisema mambo ya kuondoka CHADEMA wakati huu ambapo neema imewazukia kila mtu anakuona wa ajabu! Tulieni LOWASSA achukue Nchi Kwanza!!!
Kabla ya Slaa kuhamia Chadema ilikuwa na majimbo mangapi?leo hii ina majimbo mangapi?Kwa taarifa tu,Dr Slaa nae alihamia toka CCM kama hivi na nyakati hizi.Zaidi Dr Slaa siyo Chadema asilia,amekikuta kikiwa ni chama sio fukuto
Yuko kamili gado.vipi mgombea wako makufuri anaendeleaje?
Slaa hawezi ng`olewa na fisadi yeyote.Wakijaribu ana wanachama wanaompenda wengi watatumia ile nguvu ya umma ya wanachama kumrudisha.Ule msemo wa PEOPLE`S POWER sasa unairudia CHADEMA yenyewe.Wanachama watahakikisha wanalikimbiza fisadi mchana kweupe na kumuweka Slaa madarakani.
Taarifa za karibu zinasema kuna fisadi baada ya kuona mambo magumu Ukawa anataka kutimukia ACT kwa ZITTO kabwe CHAMA ambacho hakiko muungano wa UKAWA na Zitto kakubali kuwa akiona magumu aende tu watampokea chap chap awahi muda wa tume kuchukua fomu.
Toka lini ukawa msemaji wa CDM
Hatogopi tena ufisadi kwani chama kilicho madarakani ndicho kiwanda cha kutengeneza mafisadi. Bora tusiangamize aliyetuonyesha kiwanda cha kufyatulia mafisadi bali tusaidiane naye kukiangamiza kiwanda hicho mkuu ili tuokoe vizazi vijavyo.Mabadiliko ya kurasimisha ufisadi
Mmemtelekeza kabisa, mimi nawapongeza kwa jinsi mnavyotupiga shavu kupromoti CHADEMA&UKAWA na kumzika kabisa tingatinga.Yuko kamili gado.
Hatogopi tena ufisadi kwani chama kilicho madarakani ndicho kiwanda cha kutengeneza mafisadi. Bora tusiangamize aliyetuonyesha kiwanda cha kufyatulia mafisadi bali tusaidiane naye kukiangamiza kiwanda hicho mkuu ili tuokoe vizazi vijavyo.
Nimepita maeneo ya mianzini jijini Arusha kuna kampeni ya chini kwa chini yenye kupeana hamasa kuwa wanachadema asilia waliojitolea kupigwa risasi na mabomu pale Soweto kwa ushawishi wa Ufuasi wa Slaa.
Sasa wameweka nadhiri kuwa watahama na kumfuata kokote mpendwa wao Dr Willy Slaa ambaye ni baba wa vita dhidi ya ufisadi Tanzania.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA.