Naondoka na Slaa kampeni ya CHADEMA Asilia!

Naondoka na Slaa kampeni ya CHADEMA Asilia!

Nimepita maeneo ya mianzini jijini Arusha kuna kampeni ya chini kwa chini yenye kupeana hamasa kuwa wanachadema asilia waliojitolea kupigwa risasi na mabomu pale soweto kwa ushawishi wa Ufuasi wa Slaa.

Sasa wameweka nadhiri kuwa watahama na kumfuata kokote mpendwa wao Dr Willy Slaa ambaye ni baba wa vita dhidi ya ufisadi Tanzania.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA.

SHINDWA SHINDWA JINI WEWE HUTAFANIKIWA KUIGAWA CDM KWA CDM NI MOJA TU.

SHINDWA NA UKOME PEPO WEEWW!!!

ii
 
Lawezaje neno jema kiutoka nazareti?

Hebu fikiria kama vilabu vya mpira wa miguu visingeruhusiwa kusajiri wacheaji wapya hali ingekuwaje, na pili jiulize ni kwa nini vilabu vinaruhusiwa kusajiri wachezaji wapya tena kibaya zaidi hata wakutoka nje ya nchi ilihali vina wachezaji zaidi ya mmoja kwa kila nafasi. Nenda kawashauri Barcelona wasisajiri wachezaji wapya kwa sababu wao ndiyo timu bora duniani, watakutoa nduki karibu wakuue, kwa nini, hali hiyo hiyo lazima itazamiwe katika vyama vya siasa.
 
Dr Slaa akiondoka maana yake hesabu hazikuzingatiwa kabla ya kumkaribisha Lowasa..... tumesisitiza kumuunga mkono Lowasa kama viongozi wetu wakuu wote wamekubali kwa dhati hesabu zimezingatiwa....kinyume na hapo sitounga mkono maamuzi haya.....

Hesabu zilisha-fail tangu lowassa aingie CDM na kupewa fomu ya kugombea urais, maana yake ni kuwa hata Dr.slaa asipoondoka CDM ule ujasiri wa kujenga hoja kama ilivyokuwa mwembe yanga hatakuwa nao maana ni kula matapishi yake mwenyewe na kujipunguzia credibility kwa wananchi.

Yaani CDM/UKAWA walikuwa wanamkimbia fisi kwa kupanda mti bila kujua kuna nini juu, sasa wananing'inia juu ya mti ambao juu yake kuna nyoka .mkubwa hatari chini kukiwa na simba mwenye njaa akiwasubiri washuke awararue.
Kila uamuzi na jambo lolote watakalolifanya litakuwa na matokeo mabaya maana wakimtimua lowassa ni shida na akibaki ni shida pia. Slaa naye akibaki itakuwa ni shida na akiondoka itakuwa ni shida pia. Kwahiyo kama ni hesabu walizikosea muda mrefu muda wa kuanza kujipanga haupo tena.
 
NI sehemu gani hakuna wachagga????hizi ni namba nyingine ziacheni....kuanzia firstlady....
 
Hapo ni uelewa wa masuala ya hapa hapa au kuona picha kubwa.

Katika mapambano hayo ni kawaida kabisa .

Chris Hanni wa ANC - ndiye alipambana na umkonto we sizwe, lakini Mandela ndio alikuja kutawala Afrika Kusini.

Hatumchukii mtu au kumpenda mtu, yanatazamwa maslahi ya kudumu au picha kubwa.

Picha ndogo ni ipi, je tumuache fulani agombee ili kwamba tuonekane tumeangalia muda aliokaa katika chama ? Au tuangalie gari lipi linatufikisha pale tunapotaka kufika?

Picha kubwa au lengo kuu ni kuindoa CCM na mfumo kandamizi wake. Na ambaye kati ya wengi, atakaesaidi kufanya kazi hiyo si mwingine bali ni yule aliye katikati yao.

Kimkamkati ni muhimu kumpata huyu mchezaji aliyekuwa timu pinzani.. Kama kuna wachezaji na mashabiki na wanahisi ni vibaya, basi hawa wanahitaji kujifunza juu ya soka la kisasa ( au siasa) inavyochezwa.
 
Ww tembea naye tu yan kwa watu kama nyinyi IPO siku mtalia na kusaga meno na SKU zote mfa maji haishi kutapatapa polen sana
 
Nimepita maeneo ya mianzini jijini Arusha kuna kampeni ya chini kwa chini yenye kupeana hamasa kuwa wanachadema asilia waliojitolea kupigwa risasi na mabomu pale Soweto kwa ushawishi wa Ufuasi wa Slaa.

Sasa wameweka nadhiri kuwa watahama na kumfuata kokote mpendwa wao Dr Willy Slaa ambaye ni baba wa vita dhidi ya ufisadi Tanzania.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA.

Nitampigia kura Dk Slaa hata kama hatakuepo kwenye orodha ya wagombea urais
 
Hiyo taarifa si ya kubeza kuna viongozi wa CDM wanapanga kuuza majimbo na kata kwa madai hata mbowe kauza nafasi ya uraisi kwa Lowasa
 
mkuu umeshapokea buku 7 .chadema huwezi kuigawa kirahisi ila ni rahisi Sana kupenyeza sumu Kama hizo za kwako Ccm na ukafanikiwa chadema watu wake ni wamoja .hakuna uhusiano WA mabomu ya Soweto na Lowasa .
 
Una masaa 5 tu ujitokeze JF na unihakikishie kuwa hujajiuzulu nafasi yako. Kinyume na hivyo sina kingine cha kufanya zaidi ya kurudi CCM mimi na wadogo zangu na shemeji yangu.
 
Hahaha mtajichafua sana suluali lowasa rais kupitia ukawa
 
Kwanini ulimfuata Dr au ulifuata sera za chama?.
MAMLUKI NINI atakuwa huyu.
 
Sababu kuu ni hii, Slaa amejitahidi sana kukijenga CHADEMA, na sio siri CHADEMA imekuwa na nguvu sana baada ya ujio wa Slaa, kama lilivyo jina CHADEMA ni chama cha demokrasia, lakini demokrasi inaanza kutoka na ubabe unaingia.

Kulikuwa na wagombea walitakiwa kuchukua fomu za urais kisha kura za maoni zipigwe hilo limekufa, Lowassa kaja kabaka demokrasia kwa kusema anataka yeye tu apitishwe bila kupingwa, swali langu ni hili kama yeye Lowassa ana mvuto na wafuasi wengi anaogopa nini kupambana na wengine kwenye kura za maoni?

Kwa mtu mwenye uchungu wa nchi huwezi kuanza kumsafisha mtu ambaye hajajisafisha bado, kuna watu wanasema Lowassa katubu, kutubu nijuavyo mimi unakubali kosa kwamba ndio ulifanya kisha unaomba msamaha, lakini Lowassa hajafanya hilo ila amekana hahusiki na lolote analoulizwa, ikiwa hali ya kukana jambo ni kutubu mafisadi wote watakuwa wametubu maana wote wana tabia ya kukana,

Wabunge wengi wa
CHADEMA wamekuwa wakijitahidi kujenga hoja na kuongea na waandishi wa habari kwa lugha nzuri, misingi iliyowekwa na watu kama kina dr. Slaa, lakini leo anakuja Lowassa anaulizwa swali anasema "shut up", "keep quite" haya ni majibu ya hasira na kutisha watu ambayo hayakuwepo CHADEMA, lugha hii anaitumia kwa sababu yuko CHADEMA na watu wanashangili ila angesema maneno haya akiwa CCM angetamani ardhi ipasuke.

Hii inanikumbusha mchezo wa redio wa mzee Jangala na mwanae Mshamu, Mshamu anasema "dingi noma hivyo" kwa sababu Jangala hajui maneno ya kihuni anamsifia mtoto wake kwamba anaongea kiingereza kigumu.

CHADEMA wanasema system ya CCM ndio inawafanya watu wawe mafisadi na Lowassa katoka hiyo system na sasa atafuata system ya CHADEMA na UKAWA, lakini kabla hata ya wiki CHADEMA na UKAWA wanafuata system ya Lowassa kwa kuondoa wagombea wengine ili Lowassa apite bila kupingwa na hili ni sharti alilototoa Lowassa, system ikapindwa.
 
dr. slaa naomba kaa kimya tu achana na malumumba.
 
Back
Top Bottom