Naongea na mwenye mbwa siongei na mbwa

Naongea na mwenye mbwa siongei na mbwa

Pamoja na hayo ndio amwite mwingine mbwa?
Mkuu sio Manji bwana ni Hans pope aliyesema hivyo kipindi Magu akiwa waziri wa ujenzi na miundo mbinu alipiga mkwara kuhusu malori na pope ana miliki malorry ndio akatoa kauli hiyo, mtoa thread amekosea au hajui au kakariri
 
Duh, kama mbwa kaweza kugeuka kuwa mwenye mbwa, basi badala ya kuwa na visasi angejitambua kuwa kumbe yawezekana pia kesho akageuka tena kuwa mbwa.
Tena sio mbwa atakayekuwa na mmiliki bali mbwa koko asiye na mwenyewe wa kumhifadhi bali wa kuzurura hovyo. Ndivyo dunia ilivyo, visasi huwa vikianza havina mwisho.
Hilo ni dua la kuku Mzee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu sio Manji bwana ni Hans pope aliyesema hivyo kipindi Magu akiwa waziri wa ujenzi na miundo mbinu alipiga mkwara kuhusu malori na pope ana miliki malorry ndio akatoa kauli hiyo, mtoa thread amekosea au hajui au kakariri
Ninalijua hilo
 
Nasikia alisha omba msamaha mapema kapiga mpaka magoti na masharti juu... Mzee anachotaka anapewa hata yale maujenzi ya fujo kwa mzee nasikia ni yeye..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yule aliekuwa mbwa sasa ndio kashika Nchi...

Funzo: Tujifunze kuwa na akiba ya maneno maana hatujui ya kesho....

Na lile ghorofa lako uliosimamisha pale iringa angalia lisije kwenda na maji pia...
 
T
Kuna mtu mmoja shombe shombe (chotara/zero point five), yeye ni mmoja wa watu wenye ushawishi ndani ya klabu ambayo zamani iliitwa Sunderland. Huyu mtu ni mmoja wa wadau muhimu wa sekta ya usafirishaji, ni mmoja wa wamiliki wa magari makubwa yanayopeleka mizigo katika nchi jirani.

Wakati wa awamu ya nne aliingia kwenye mzozo na aliyekuwa waziri wa barabara, akafikia hatua ya kuongea kwa dharau akisema kwamba yeye haongei na mbwa bali anaongea na mmiliki wa mbwa, ilibidi aliyekuwa waziri mkuu aingilie kati na kuutatua ugomvi ule.

Mungu si athumani siku za kuishi huwa zinakwenda kasi sana, leo hii yule aliyeitwa mbwa ndiye mwenye mbwa, na ana sauti ya juu kabisa na yenye mamlaka.

Shombe shombe yupo kwenye wakati mgumu, kwani huyu mwenye mbwa wa sasa, anafahamu fika dharau aliyokutana nayo wakati akiwa kazini katika wizara ya barabara.

Nyeti zinahabarisha kwamba mwenye mbwa yupo njiani kuandaa mapigo yatakayorudisha heshima aliyoipoteza baada ya kudharauliwa mpaka kufananishwa na dogi.

Somo muhimu kwa shombe shombe na wengine wote wenye kupenda kuropoka hovyo bila ya kuitazama kesho inafananaje, ni kwamba mdomo ulikiponza kichwa.
Tunamba hiyo video
 
Kuna vitu huwezi kuvisema lakini Hans Pope na JPM ni dhahili Hans Yupo mbali sana kwanzia siasa, biashara na Michezo!!.. Mungu amlaze Mzee Hans Pope sehemu salama Peponi!!
 
Back
Top Bottom