Ninachokulekeza ni jinsi ya kushinda vya kiroho ikiwa umelala.
Kitu Cha kwanza kabisa uombe Toba, kwaajili yako, family, ukoo, mahali unapolala (ardhi) mtaa. Na chochote kile ambacho kimefungua mlango
Shetan hapiti kama hana uhalali, hivyo Toba itakusaidia kumpa Mungu nafasi ya kukutetea. Kasome Daniel 9: 4-19( kaombe toba kupitia hii mistari, tumia damu ya Yesu inene rehema juu yako)
2
Utu wako wa ndani lazima uwe na nguvu ya kupigana vita, cz ukilala hutakiwi kulala usngiz utu wako wa ndani lazima uwe Macho
“lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. ”
— Mathayo 13:25
Kulala usingiz wa mwilini ni sawa ila ndani uwe na nguvu Ili usipandikiziwe vitu visivyo sahihi.
Unapataje nguvu Kwa utu wako wa ndani Kwa kumuomba Mungu
“awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, #kufanywa imara# kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake #katika utu wa ndani. ”#
— Waefeso 3:16
3
Mungu akufundishe mikono yako vita ili uweze kupambana ktk vitu vya rohoni(Daudi alipewa)
“Ananifundisha mikono yangu vita; Hata mikono yangu yaupinda upinde wa shaba. ”
— 2 Samweli 22:35
“Na ahimidiwe Bwana, mwamba wangu, Anifundishaye mikono yangu vita, Vidole vyangu kupigana. ”
— Zaburi 144:1
👆anayefundisha kupigana ni Mungu, hivyo jiombee.
4. Achilia damu ya Yesu ( nyunyiza katika kila kitu) Kwa Imani, Kwa kutamka,
Mfano ardhi, mwili wangu, nafsi yangu, na chochote kile ili vipigane upande wangu.
Waebrania 12:24
Paka damu ya Yesu ya pasaka ktk malango ya ndoto na muda malango ya nyumba yako,( Kwa kutamka kuwa napaka damu ya Yesu ya pasaka
Kutoka 12
¹² Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana.
¹³ Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri.
👆Akiiona damu(Yesu) hatoruhusu pigo Wala yule anaye haribu aingie ktk majumba yenu./ktk chochote unachotaka kilindwe
4
Mungu akusaidie kushinda vita vya kiroho hata uwapo ktk njozi
“Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa njozi, Ukasema, nimempa aliye hodari msaada; Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu. ”
— Zaburi 89:19
Omba hiyo.
#yeyote mwenye shida ya njozi na akiota hawezi kupigana, aombe hiyo# jiombee Mara Kwa Mara na usome Neno la Mungu ( bible) Kwa msaada wa Roho Mtakatifu
Ukiomba kwa Imani na mara nyingi, utajikuta unaweza kuomba vizuri kabisa, ukiwa umelala usingizi, na unashinda hukohuko ktk ndoto
NB hakikisha unatengeneza na Mungu