Mo mp5
Nikupe pole sana tena sana kwa mambo kadhaa.
Mosi kwa kufiwa na mdogo wako.
Pili, umepewa ushauri wa kila aina lkn hata sasa wewe mwenyewe hujui ushike upi uache upi?
Tatu, naona hujui kbs madhara ya ndoto za namna hii.
Kuna watu wamesema jambo zuri sana, wamesema omba. Lkn sijui kama unajua kuombea kesi za namna hii. Wewe mwenyewe unajionaje linapokuja swala la kuomba. Kuna tofauti ya kuomba na kuombewa.
Ok, tuingie darasani kidogo na Roho Mtakatifu anisaidie kukupa maarifa zaidi.
Mathayo 8:22
[22]Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao.
Unauona huo mstari.
Huyu ndugu alitaka kumfuata Yesu (nuru) lkn akatoa shariti, akamzike kwanza baba yake. Yesu akajibu kama unavyoweza kusoma hapo. Maana yake nini? Mtu anapokufa, hatuna ushirika nae tena, awe amemaliza wakati wake au bado, yaani akiishatoka kweny huu mwili ambao tunauona kwa macho, hatokaa aonane nawewe tena. Akiwa ndani ya mwili anaweza kuongea, akiisha toka hawezi tena, yaani hana viwezeshaji. Kuna maeneo mawili, aidha aende jehanamu au aende paradiso. Japokuwa kuna watu huchukuliwa mateka nakwenda kufanya kazi kuzimu, huku mnadhani amekufa na mkazika lkn kumbe yu hai ktk ulimwengu mwingine katulia tu anafanya kazi.
Kauli ya mdogo wako inasema, naenda lkn nitakuwa pamoja nawewe. Swali anaenda wapi?
Ngoja nikupe maarifa zaidi bro. Kuna bwana mmoja alikuwa tajiri sana, na mwenye roho mbaya sana. Alimtendea Lazaro vibaya sana. Muda ukafika Lazaro akafa akaenda kifuani kwa Ibrahim, huyu tajiri nae akafuata akaishia motoni. Akiwa anaivilia huko ndio akamuona Lazaro kifuani mwa Ibrahim. Akamsemeaha mzee akasema aise naomba huyo Lazaro achivye kidole ncha ya kidole.....ok nilitaka nikuonyeshe watu wanapokufa wanakwenda wapi. Hii story iko kweny biblia pia. Mtu hawezi kutoka huko kuzimu kuja duniani kukupa maarifa, au kukusaidia jambo. Hilo jambo halipo na halitakaa liwepo. Watu tumezika na kuzika lkn no more connection, why you?
Nakufafanulia kilichopo kati yako na marehemu.
Meneno uliyasikia vizuri ila sauti hukuijua ni ya nani? Narudia tena, unaweza kuelewa maneno ya mtu ila usielewe sauti. Sauti inakupa kusudi la hayo maneno. Sauti inakupa kujua mtoa maneno ni nani. Infact hakuwa mdogo wako, ni roho ya kuzimu ndio iliyokuwa inasema nawewe kwa kutumia kinywa cha mdogo wako. Unasema unamaanisha nini, namaanisha, maroho machafu yanaweza kutumia kinywa cha mtu yeyote hata baba yako kukusemesha. Mtu akikuambua wewe ni shoga wakati wewe si shoga si yeye aliyetamka ila kuna roho imemvaa ndio inayotafuta nafasi ya ushoga ndani yako. Sijui kama unanielewa. Sasa lilipo agano lzm na mauti iwepo. Ile roho imefanya agano nawewe na agano lenyewe ni kwamba itakuwa nawewe muda wote na ndio maana unapolala inakuita ktk roho mnajikuta mpo pamoja. Mauti iliyofanyika ni kifo cha mdogo wako.
Twende tu tutaelewana. Masomo mengine kama huelewi unaandika notisi utaelewa baadae sindio, ee twende mbele.
Kwahiyo sasa wewe unaushirika na roho ya mauti sio mdogo wako. Msaada itakaokupa hiyo roho iliyokatika sura ya mdogo wako ni kukuua tu, no more. Kuna watu nimeona wakisema itakusaidia mbeleni, anyway niseme nawao haelewi, kwahiyo kadiri mnavyoendelea ktk kukutana na kuongea inazidi kupandikiza uharibifu taratibu kbs bila ya wewe kujua. Na mbaya zaidi inatumia mazingira yaleyale mliokuwa na mdogo wako. Huo mzimu umetumia mbinu ngumu sana kwako bro,
Mimi ninayesema nawe nawewe nayajua haya mambo vizuri, na swala la ndoto ni sehemu Mungu amenipa kufasiri. Kwahiyo kama unahitaji msaada zaidi wa kimaombi na mafundisho ya Kristo basi karibu.
Hiyo roho imekuwekea hali fulani ya kumbukumbu isiyotoka ndani yako ili iendelee kukunasa. Kama umekuwa ukiota unakula nayo sasa hilo ni balaa jingine.
Good day