kaburungu
JF-Expert Member
- Mar 9, 2011
- 3,706
- 6,901
Pole sana mkuu, nimepitia kwenye dalili kama zako ila ni kama week tatu zilizopita vipimo umetaja ndio nilivyofanya na vyote havikuwa na shida. Kifua nilikua nacho tena kikali sana ila nilipewa dawa mapema kikatulia, nimehangaika na mafua makali sijapata umwa mafua kama yale.Upone haraka mkuuu, nashukuru kwa kuorodhesha hizo dalili.
Hivi karibuni nimekuwa nahisi vichomi kwenye kifua,joto la mwili liko juu,usingizi sipati,kichwa kinauma,mwili wote na mifupa kuuma na sometimes ucku nilitetemeka na uchovu wa hapa na pale japo sikohoi , Hali ambayo sijawahi experience kwa miaka mingi.
Nimelazimika kuingia jukwaa hili nione kama ntapata dalili kama zangu Ili nijue cha kufanya,nimepima vipimo vya kawaida kama typhoid,UTI,malaria na tumbo hakuna kitu.Hapa nawaza niendelee na vipimo au nitafute mkondo mwingine wa matibabu.
Siku nimeenda hospital kuchek afya walipima joto hakukuwa na shida ila Jana mchana hadi naandika sms hii joto liko juu Sana.Hapa Niko stuck nifanye uamzi upi japo tunatakiwa kutokuwa na hofu but lolote linaweza kutokea.Daa hatari sana may God helps me..
Kwa kawaida nikipata mafua kuna vidonge hua nameza ni ndani ya siku mbili tu habari imeisha, hayo niliyopata week tatu zilizopita yalikuwa makali sana, kukosa usingizi, joint kuuma, kichwa ndio usiseme joto la mwili kuwa juu yani tabu tupu, mimi ilikuwa ikifika usiku ni kama nakesha maana usingizi sipati.
Kwa muda wa siku kama tano nahangaika na mafua makali balaa.. hadi navyoandika muda huu nimepoteza ladha na harufu yani sinusi week ya tatu hii na sina mafua wala nini. Hali yako kwa sasa ikoje?
Note: sijaandika the whole story, kuna siku nadhani ya nne kuumwa mafua niliumwa sana usiku, yote tisa ilifika mahali mkojo ukawa hautoki maumivu makali sana chini kitovu upande wa kushoto ile siku nilishaanza kujiambia hii ndo kwisha habari ashukuriwe Mungu niliwahishwa hospitali kwa sasa nipo salama shida imebaki kwenye kunusa na ladha ya chakula, hatari hii [emoji23][emoji23]