Napata harufu ya matumizi ya Nyuklia Ukraine baada ya Kursk kuanguka

Napata harufu ya matumizi ya Nyuklia Ukraine baada ya Kursk kuanguka

Yaani zelensky ameamua kutoa vifaa vya kijashi, magari pamoja na wanajeshi wake sadaka ili tu apewe pesa!? Na kwa akilli zake za uchekeshaji alitegemea Urusi ataenda kichwa kichwa ili amtie hasara kimebuma.
 
Ukraine ana halalisha uvamizi wa Urusi katika mipaka yake.

Ukraine alipaswa kumfukuza Urusi katika mipaka yake na sio kuvamia mipaka ya Urusi kama Urusi alivyofanya kwake.

Sina hakika sana juu ya silaha hizo za maangamizi ila ninachoona ni Urusi kupata support zaidi ya kuingamiza Ukraine kupitia uvamizi huu.

Support ya ndani na ya nje kwa washirika wake na hata wasio washirika wake.

Urusi atasema najilinda dhidi ya uvamizi wa Ukraine atautumia udhaifu huu kuleta maafa sijajua ni kipi makamanda na majeshi ya Ukraine wanacho fikiri.
Yaani wewe jamaa bana

Urusi ana HAKI ya kuivamia Ukraine ila Ukraine haina HAKI ya kuivamia Russia?

Yaani yeye Ukraine kazi yake ni kukaa nchini mwake na kujitetea humo humo?

Yeye Russia ndio ana haki pekee yake ya kuvamia nchi za watu tu na kufanya atakalo ila hakuna nchi ina haki pia ya kuivamia Russia?

Wewe na Putin mna vichaa kabisa!
 
Hizi akili kwanini tunashindwa kuzitumia vyema? Kama Ukraine hawezi shikilia hilo eneo kwa mwaka mzima, ulitegemea Russia angekaa zaidi ya miaka miwili bila kuidondosha serikali ya sasa ya Ukraine?

Hii vita imetupa matokeo mengi tofauti na matarajio yetu. Sidhani kama Ukraine hajakaa chini na washirika wake kabla ya kuchukua uamuzi wa kuingia Russia.
Kwanza eneo la Kursk kwa asilimia kubwa ni pori na hata wakazi wake sio wengi. Pia inasemwa kwamba Russia iliondoa zana zake za kijeshi Kursk hasa meli vita wiki moja kabla ya Ukraine kuvuka mpaka kwahiyo imawezekana ni mpango wa Russia Ukraine ihamishie vikosi vyake Kursk bila upinzani kisha izibe njia za kuingia na kutoka na winter ikaanza na kazi nayo ianze.
 
Ukraine hana army ya kupiga russia kwa mda mrefu na kulinda maeneo anayo chukua na ku defend ndani kwenye maeneo yenye vita kwa wakati mmoja
unajuwa aina ngap za majeshi yanapigana upande wa Ukraine ? au unamuona Putin mjinga kuomba support Iran , North Korea na China
 
Ndio mnavyojidanganya watumie midude gani 😀

Unadhani kama ikitumiwa nyuklia pale ukraine utapatikana hata muda wa kuregesha majibu

Russia hawezi kutumia nyuklia sababu yeye sio mdhaifu kama marekani
kwahiyo Ukraine anapigana pekee yake ? unahisi kwann Putin hajafanya hivyo mpk sasa ?
 
Putin amepigiwa hesabu ya miaka 10 ijayo.

Kuna mwaka Putin atakuja kuondolewa na Warusi wenyewe sababu ya majnga yatakayo ikumba Rusia hasa uchumi
bila kusahau China anaombea kuwa na Urusi kama jirani ikiwa dhaifu na sio imara
 
kwan NATO imewai husika na huu mzozo ? au unahisi NATO ni Italy , Uk , Germany , France na USA ?
Mmeendelea kua wapiga ramli sasa au sio😀

Kwanini nato wasiende kumtoa mnabakia kua wapiga ramli poleni sana😀😀
 
kwahiyo Ukraine anapigana pekee yake ? unahisi kwann Putin hajafanya hivyo mpk sasa ?
Ukraine hapigani pekee hili kila mtu anajua

Russia atumie nyuklia kwanini wakati mambo yanamwendea vyema uwanja wa vita

Anaetumia nyuklia hua ni muoga na kama sio muoga hua kaona tishio mbele yake na hata Russia kasema hivyo akiona hili tishio mbele yake atatumia nyuklia

Marekani alitumia nyuklia kwasababu ya uoga wake
 
Putin aombe sana rafiki yake Trump ashinde uchaguzi wa Marekani, vinginevyo hii vita itazidi kumchachia.
kwenye mahojiano ya Trump na elon ,Trump alilidai alimshauri sana andunje kuhusu kuivamia ukraine,andunje akachukulia easly sasa hivi hajui atatokaje kwenye huu mtego.
 
Mmeendelea kua wapiga ramli sasa au sio😀

Kwanini nato wasiende kumtoa mnabakia kua wapiga ramli poleni sana😀😀
Dogo subiri hizi ni game za wakubwa zinapalaniwa kikubwa!

We uliwahi kuwaza kama ipo siku ndani ya ardhi ya Putin kutatokea mashambulizi toka Ukrain?

Mambo yanabadirika sana.
 
I think it's a game plan,

Vita inaelekea kwisha, wameona wawwachie kidogo ili wapate nafasi ya kukaa mezani.

If you remember, Russia alikuwa ameingia mpaka Kyiv mwanzoni mwa vita wakamwambia ili waanze mazungumzo atoke Kwanza then wakamgeuka.

Nadhan itakuwa vice versa ili wapate nguvu na justification kwa wananchi ya kukaa mezani
hapa sio kijiwe cha kahawa..Kuna documentary ya battle of Kiev.
Urusi aliondoka Kiev mwenyewe baada ya kuzidiwa.

Battle for Kyiv: Ukrainian valor, Russian blunders combined to save the capital.
 
Dogo subiri hizi ni game za wakubwa zinapalaniwa kikubwa!

We uliwahi kuwaza kama ipo siku ndani ya ardhi ya Putin kutatokea mashambulizi toka Ukrain?

Mambo yanabadirika sana.
Mashambulizi yametokea mpaka ndani ya ardhi ya Americant ambae kwenu super power

Seuze hapo mpakani Kwa Russia na kuhusiana na mashambulizi ndani ya russia ndio kwanza umeliona hili tokea 2022?
 
Wengi watakumbuka katika vita vya uvamizi vinavyoendelea huko Ukraine wakati vinaanza ilikuwa Ukraine akijibu mashambulizi kwa kushambulia eneo lolote ndani ya Russia au maeneo ya Ukraine yaliyotekwa na Urusi kama vile Crimea basi jeshi Urusi litajibu maradufu kwa kuvurumisha mvua ya makombora hadi ya supersonic kila mahali ndani ya Ukraine, Kyiv na miji mingine ilikuwa inashambuliwa sana kuanzia hospitali hadi shule za nursery za watoto.

Nimeshangaa kuona kuona kuna uvamizi au SMO ya wiki mbili sasa ndani ya mipaka ya Urusi katika eneo la Kursk majeshi ya Ukraine yakijivinjari ndani ya mipaka ya Urusi na kupelekea wakimbizi wa ndani wa Urusi zaidi ya 20,000 huku tukiwa hatujaona majibu ya majeshi ya Urusi mpaka sasa! Hii sio kawaida ya Putin kabisa ukizingatia mbele kidogo ya eneo hili kuna bomba la gesi linalopitisha 50% ya gesi kupeleka nje ya nchi.

Labda Putin ameisha amekuwa mdebwedo kabisa baada ya mipango yote ya uvamizi kuvurugika na kwenda mrama. Vinginevyo kuna uwezekano mkubwa anaandaa shambulizi "barbaric" la nuclear.
hapo yajayo yanafurahisha...NATO watapiga nduru mpk mbingu ya 7
 
kwenye mahojiano ya Trump na elon ,Trump alilidai alimshauri sana andunje kuhusu kuivamia ukraine,andunje akachukulia easly sasa hivi hajui atatokaje kwenye huu mtego.
Trump alishasema hatoruhusu kuona Ukraine ikimezwa na Russia, alizungumza haya kwenye mdahalo baina yake na Biden.
 
hapa sio kijiwe cha kahawa..Kuna documentary ya battle of Kiev.
Urusi aliondoka Kiev mwenyewe baada ya kuzidiwa.

Battle for Kyiv: Ukrainian valor, Russian blunders combined to save the capital.

Imetengenezwa na nani?

Una miaka mingapi?

Hujui influence ya media na why nations are fighting to controll or block media access?
 
Imetengenezwa na nani?

Una miaka mingapi?

Hujui influence ya media na why nations are fighting to controll or block media access?
1.
imetengenezwa/kuandika na walioshiriki kusimamisha majezi ya urusi Kiev.
2. nipo thirties.

3.let say hakuna media",Je,Urusi imeiteka Kiev?..
 
Trump alishasema hatoruhusu kuona Ukraine ikimezwa na Russia, alizungumza haya kwenye mdahalo baina yake na Biden.
Trump ni mtu wa kelele mingi ila vitendo zero.
Hata kipindi cha utawala wake alimkoromea vivyo hivyo China akisema hatoruhusu China iitawale Asia Pacific na South China sea ambako kuna baadhi ya visiwa vya Phillipines vilinyakuliwa na China.
Alipeleka battleships na Aircraft carrier kwa mbwembwe zoote.
China alipo deploy DONGFENG ballistic missiles tu zile ndege zote zilisimama kuruka kwake.
 
Ukraine ana halalisha uvamizi wa Urusi katika mipaka yake.

Ukraine alipaswa kumfukuza Urusi katika mipaka yake na sio kuvamia mipaka ya Urusi kama Urusi alivyofanya kwake.

Sina hakika sana juu ya silaha hizo za maangamizi ila ninachoona ni Urusi kupata support zaidi ya kuingamiza Ukraine kupitia uvamizi huu.

Support ya ndani na ya nje kwa washirika wake na hata wasio washirika wake.

Urusi atasema najilinda dhidi ya uvamizi wa Ukraine atautumia udhaifu huu kuleta maafa sijajua ni kipi makamanda na majeshi ya Ukraine wanacho fikiri.
Ukraine yuko sahihi, alivamiwa naye akavamia. Russia aliweka nguvu yote kuivamia nchi ya wenyewe akaiacha nchi yake uchi😃😃😃😃😃
 
Back
Top Bottom