Napata maumivu upande wa moyo, hizi ni dalili za ugonjwa gani?

Napata maumivu upande wa moyo, hizi ni dalili za ugonjwa gani?

Nina tatizo kama hilo, inakaribia mwezi sasa. Ninapata maumivu upande wa kushoto na moyo unauma km kuna kitu kinachoma, tumbo linakuwa linakaza sana, muda mwingine nasikia miungurumo kama ya gesi tumboni. Kuna muda mapigo ya moyo yanakwenda kasi na ninaanza kujisikia vibaya sana hasa usiku au nikiwa kwenye vyombo vya usafiri hadi inafikia hatua ninashuka na kutulia mahali then naendelea na safari, kama ni usiku nimelala nitaamka na kukaa kitandani yakitulia nitalala.

Nimeenda dispensary nikaambiwa ni gesi nikapewa dawa ila sioni badiliko lolote.! Sasa sijajua ni vidonda vya tumbo au ni shida ya moyo
 
ulipima wapi mkuu na gharama zikoje
Jina la polyclinic nimelisahau kidogo...ila ni pale MLIMANI TOWER ilipokuwepo zamani TCU...ni opposite na Mlimani city na ndani ya hilo ghorofa kuna HQ ya MCB BANK....

Jina la polyclinic linenitoka kidogo...Kama una bima itakuwa nafuu sana..

Mimi sijuwa na bima kwahiyo 'niliumia'. Kumuona specialist ilikuwa 30k...vipimo ilinicost 50k so jumla ni 80....Hapo ni nje ya dawa.

Kila la heri mkuu....Mungu akufanyie wepesi
 
Nikiwa chuoni kuelekea mwaka wa nne.. nilipata msiba mkubwa ghafla.. na being an introvert.. maumivu niliyaficha moyoni.. nilihuzunika na kuwaza na kuomboleza mwenyewe...

Niliporejea shule.. my life changed completely.. sikutaka kujiassociate na watu.. most of times nilitumia muda wangu mwenyewe...

Nikaanza kuexperience kuchoka haraka sana... Heightened heart rate.. dizziness.. head aches.. chest pain especially upande wa kushoto.. kuanzia upande wa mbele mpaka nyuma ya eneo la moyo.

Nilienda sana hospitali.. nikashindwa kuendelea kuwa active kwenye sports.. baadae ikaja kugundulika haikuwa shida ya moyo.. ila nilikuwa na GERD.. (A form of anxiety disorder) ni wasiwasi tu.

Nikaanza kujiongoza katika kubadili mtazamo na ilinisaidia.. I went back to sport activities in six months..na mpaka leo hurudi nyakati fulani fulani ninapokuwa stressed ila najua kupambana nayo kwa sasa.

Pole ndugu yangu.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Stress mara nyingi huleta hili tatizo yawezekana hata mtoa mada kuna kitu kilimkuta cha kumfanya awe na mawazo kila mara na kwa muda mrefu,na ukikaa vibaya unaweza waza hata kujitoa roho tu unajihisi kama dunia imekuangukia na hauna maana tena.
 
Mkuu kila mtu humutokea tokana na tatizo alilopata! Nakumbuka,mwaka 2018 nilikua na demu nilimpenda sana,akaja akapata kazi mkoa,nilipoenda kwake,nilikuta dalili flan hivi ambazo zikuzielewa! Usiku tumelala ikaingia text ya jamaa, kwa mpenzi wangu inasema ( Mpenzi wangu,ukitoka safari tu,nitakuja nikuto...m..b..e hadi this time ubebe mimba,na uache kuwa unatumia P2 after sex,nataka kuzaa na wewe!) Maana yake alimwambia yule jamaa,anasafiri ili hali yupo na mimi pale kwake! Asubuhi nikawa na ujasiri wa hali ya juu sana,nikauliza huyu nani, alijibu simple sana just a friend! Nilipombana akajibu kwani wewe umekuja kwetu officially?? Nina maamuzi yangu,naweza kua na wewe au kua na huyo aliyetuma sms!

Nikaona isiwe shida,nikabeba begi langu,nikasepa zangu kurudi kwangu,maana tungegawana majengo ya Serikali,basi niliumwa sana moyo, nikaenda hospital kumueleza Dr pale TMJ ,akanipima akakuta heart beats zinaenda kwa kasi sana,nikapewa dawa,za mwezi mzima,baada ya miezi miwili nilipona kabisa,nikarudi kufanya check up tena,mambo yalikua poa kabisa, halafu yule Dr siku hiyo baada ya check up si akaweka ule wimbo wa Ditto kazi ya moyo sukuma damu! Yaani ikabaki tunacheka tu wote pale! Nikamfutilia mbali yule demu,! Baada ya mda akaanza vi text mambo,kumbe kipindi hicho kazi imeisha na yule jamaa alikua mme wa mtu na ana familia yake! Na kama kuna kitu kinakutesa usikikumbatie! Ongea na mtu wako wa karibu,mshirikishe uweze kupata relief,hasa kuumizwa na mapenzi na kumpoteza mtu wako wa karibu,Mzazi au mlezi wako!
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
Kuna kitu hapo umekisema kinatutesa wengi sana,hicho cha kuweka limzigo rohoni unakua huna hata uwezo wa kumueleza mtu ndo chanzo kikuu cha tatizo hili maana wengi wanakua na Kitu kinawala ndani kwa ndani.
Na MAPENZI ndo huwa chanzo kwa asilimia kubwa.Japo ukiwah unaweza usitumie dawa za hospitali unapata tiba ya kisaikolojia unakua fit kabisa.
 
Nenda hospitali hili si suala la mitandaoni, hospitali kwanza kisha mitandaoni. Mitandaoni utakuja ambiwa huo ni moyo umedondoka stand yake imechakaa kuna mtu anayo mpya anaiuza.
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Habari za humu wataalam,

kwa muda mrefu ninasumbuliwa na maumivu eneo la moyo(kifuani upande wa kushoto) yakielekea upande wa nyuma kwenye bega.

Maumivu hayo sasahivi yanafika hadi shingoni.
Inaitwa Angina, kuna stable na unstable angina. Nenda muone daktari wa Moyo , mimi ilinisumbua sana na dawa zipo nyingi tuu
 
Mkuu kwa asilimia kubwa una gerd.
Gerd ni ugonjwa wa kuwa na asidi nyingi tumboni.kabla ya kuwa na chronic gerd unakuwa tayari na acid reflux.
dalili zake
1)kuhisi kiungulia
2)maumivu ya kifua sehemu za moyo yasiyoelezeka pamoja na mkono wa kushoto kuuma.
3)chakula huwa na hali ya kurudi nyuma hadi kwenye Koo na Koo huwa kama limeziba na kupelekea shingo,taya na kuzunguka mgongoni kuuma.
4)kupumua kwa shida hii ni kutokana asidi inayotoka tumboni hupanda hadi kooni na sometimes kuingia njia za hewa.
5)tumbo kuuma na kifua hasa wakati wa mazoezi ya kukimbia sana.

Kiukweli gerd imekuwa tishio saivi na tatizo bado watu hawaijui vizuri, nakushauri mkuu nenda hospital ila [emoji817] una gerd,na asilimia ndogo utakuwa na angina au matatizo ya moyo.
Ukigundulika na hiyo utaelekezwa matibabu yake hukohuko hospitali.ugua pole mkuu
Bro nimesoma habari yako kama imenigusa hivi Mimi naskia maumivu ya tumbo upande wa kushoto na sometime maumivu hupanda mpka juu maeneo ya chini ya Moyo ... Nisaidie nifanyeje ...!!?
 
Asante Sana lakini nina miaka minne na hili tatizo.
Ushauri
Nenda hospital kabla tatizo halija serious.
Note
Pendelea kutumia cocoa na kitunguu maji (chew) epuka vyakula vya zao la wanyama na ndege mf nyama, mayai, maziwa nk
 
Back
Top Bottom