Napata maumivu upande wa moyo, hizi ni dalili za ugonjwa gani?

Nina tatizo kama hilo, inakaribia mwezi sasa. Ninapata maumivu upande wa kushoto na moyo unauma km kuna kitu kinachoma, tumbo linakuwa linakaza sana, muda mwingine nasikia miungurumo kama ya gesi tumboni. Kuna muda mapigo ya moyo yanakwenda kasi na ninaanza kujisikia vibaya sana hasa usiku au nikiwa kwenye vyombo vya usafiri hadi inafikia hatua ninashuka na kutulia mahali then naendelea na safari, kama ni usiku nimelala nitaamka na kukaa kitandani yakitulia nitalala.

Nimeenda dispensary nikaambiwa ni gesi nikapewa dawa ila sioni badiliko lolote.! Sasa sijajua ni vidonda vya tumbo au ni shida ya moyo
 
ulipima wapi mkuu na gharama zikoje
Jina la polyclinic nimelisahau kidogo...ila ni pale MLIMANI TOWER ilipokuwepo zamani TCU...ni opposite na Mlimani city na ndani ya hilo ghorofa kuna HQ ya MCB BANK....

Jina la polyclinic linenitoka kidogo...Kama una bima itakuwa nafuu sana..

Mimi sijuwa na bima kwahiyo 'niliumia'. Kumuona specialist ilikuwa 30k...vipimo ilinicost 50k so jumla ni 80....Hapo ni nje ya dawa.

Kila la heri mkuu....Mungu akufanyie wepesi
 
Stress mara nyingi huleta hili tatizo yawezekana hata mtoa mada kuna kitu kilimkuta cha kumfanya awe na mawazo kila mara na kwa muda mrefu,na ukikaa vibaya unaweza waza hata kujitoa roho tu unajihisi kama dunia imekuangukia na hauna maana tena.
 
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
Kuna kitu hapo umekisema kinatutesa wengi sana,hicho cha kuweka limzigo rohoni unakua huna hata uwezo wa kumueleza mtu ndo chanzo kikuu cha tatizo hili maana wengi wanakua na Kitu kinawala ndani kwa ndani.
Na MAPENZI ndo huwa chanzo kwa asilimia kubwa.Japo ukiwah unaweza usitumie dawa za hospitali unapata tiba ya kisaikolojia unakua fit kabisa.
 
Nenda hospitali hili si suala la mitandaoni, hospitali kwanza kisha mitandaoni. Mitandaoni utakuja ambiwa huo ni moyo umedondoka stand yake imechakaa kuna mtu anayo mpya anaiuza.
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Habari za humu wataalam,

kwa muda mrefu ninasumbuliwa na maumivu eneo la moyo(kifuani upande wa kushoto) yakielekea upande wa nyuma kwenye bega.

Maumivu hayo sasahivi yanafika hadi shingoni.
Inaitwa Angina, kuna stable na unstable angina. Nenda muone daktari wa Moyo , mimi ilinisumbua sana na dawa zipo nyingi tuu
 
Bro nimesoma habari yako kama imenigusa hivi Mimi naskia maumivu ya tumbo upande wa kushoto na sometime maumivu hupanda mpka juu maeneo ya chini ya Moyo ... Nisaidie nifanyeje ...!!?
 
Asante Sana lakini nina miaka minne na hili tatizo.
Ushauri
Nenda hospital kabla tatizo halija serious.
Note
Pendelea kutumia cocoa na kitunguu maji (chew) epuka vyakula vya zao la wanyama na ndege mf nyama, mayai, maziwa nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…