Napata maumivu ya kichwa yasiyopona kwa takriban mwezi sasa

Napata maumivu ya kichwa yasiyopona kwa takriban mwezi sasa

Natumai nyote mu wazima wa afya.

Nimekuwa nikisumbuliwa na maumivu ya kichwa yasiyopona kwa takriban mwezi sasa. Kila siku, ikifika muda fulani, kichwa huuma sana na kunikosesha raha.

Nimetumia dawa nyingi bila mafanikio.

Je, huu ni wakati muafaka wa kupima macho ili kuona kama tatizo linaweza kuwa macho yangu?

Huenda nikapata afueni.
Una damu nyingi nenda kapime wingi wa damu kama ni nyingi nenda kachangie damu
 
Wingi wa damu
Kutembea/kufanya kaz juani
Over working
Muda mchache wa kulala
Dhalili ya homa
Mawazo
Tatzo la macho

Hizo ni baadhi ya sababu za kichwa kuuma
 
Ulishawahi kupata ajali , kupigwa na kitu kizito kichwani au sudden fall? ukapigiza kichwa
 
Hilo tatizo wanaita ni kipanda uso asee mimi wife nimehangaika nae mwaka wa kumi sasa mara nyingi kichwa huuma jion mpka asbh mchana unaweza kupata unafuu na ni kwenye paji la uso au upande karb na sikio.
Kwa sasa wife ana siku zake akikarbia siku zake au baada ya sik zake lazima kiume asee magonjwa mengine yasikie tu.
Tumeangaika kila akipimwa mara damu labda nying lakn wap mara homoni labda zinashida akapewa dawa za kurekebisha lakn wapi
Akapimwa macho lkn wapi.

Wataalam wanasema kipanda uso n mpka madawa ya miti shamba nd unaweza kupona
 
Angalia pia vyakula na vinywaji unavyotumia caffein ikizidi huleta maumiv ya kichwa
 
Mda mwemgine kinauma apa mbele kwenye komo,mda mwengine upande wa kulia na mda mwengine upande wa kushoto
Either macho, sinus, migraine au pressure zaidi low pressure.
Kapime macho, pressure, wingi wa damu.
Pia angalia hormones km zipo sawa.
Lifestyle pia inaweza kuwa sabb. Jee unapumzika vya kutosha? Kazi unafanya kwa kiasi zaidi za kutumia akili na computer? Jee huna vitu vinokufanya uwe tensed?
Au kuna kitu una uraibu nacho kwa sasa umekiwacha, kama chai au kahawa n k? Mana saivi kipindi cha mfungo pengine unafunga na mwili haujakubaliana na hio hali. Kiufupi nenda kafanye vipimo na usikubali kuondolewa njiani hakikisha unajua tatizo ni nini na unapata matibabu. Mana madaktari wetu kwa labda,labda hawajambo.
Pia tumia mafuta ya kupaka yanasaidia sn. Km vicks, lkn isiwe vicks kali
20240425_062818.jpg
20240425_062756.jpg
 
Back
Top Bottom