Napata ndoto za kutisha baada ya kwenda kwa mganga wa kienyeji

Napata ndoto za kutisha baada ya kwenda kwa mganga wa kienyeji

Kuota unakimbizwa ni ishara ya kufukuzwa kwenye mafanikio yako halisi na kupewa feki ambayo ndo unayaona sasa.

Lakini pia kuota nyoka anakutemea sumu ni ishara nyingine kwamba umeingia kwenye milki ya shetani (nyoka) na tayari amekupa sumu ambayo baada ya muda ndo itaanza kuonyesha makali yake.

Ulivyokuwa ukiomba na kukemea kwenye ndoto ni Mungu anasema na wewe kuwa bado mlango wa neema ya Kristu kupitia damu yake haujafungwa na anatamani uwe na nguvu za kiroho halisi kupitia Neno lake badala ya kutembea katika mafanikio hafifu na ya muda ya giza.

Jitafakari before ts too late. Umefanya jambo ambalo Mungu alitaka kuwaangamiza wana wa Israeli wote at once pale walipochanganya miungu (walitengeneza ndama) wakaiabudu.

Mungu akurehemu sana rafiki yangu. Moyoni wangu umepata huzuni kusoma andiko hili kama ni la kweli.

Be Blessed.

Wewe siyo wa kwanza kupitia Economic crisis Mkuu..

Tatizo hukupata ushauri sahihi matokeo yake ukashauriwa kuziendea njia za giza..
(kumsujudia Shetani)

Itakufaidi nini ukipata milki zote za Dunia halafu ukamkosa Mungu?

Kwa maana Shetani anao uwezo wa kukupa mali...lakini Mwisho wake ni Kifo tena cha Ghafla ili usipate Muda wa kutubu....

Na hiyo Dhambi utaona ni ndogo lakini...itakuandama wewe na uzao wako wote na ni machungu yasiyo na mfano...

Wewe unajiangalia binafsi yako lakini shetani analenga madhara yatakayokuandama vizazi vyako vyote...

Unajisikiaje unaendesha gari, una nyumba, na mali nyingi halafu moyoni mwako unajua wazi Mdhamini wako ni Shetani?

Hili jambo linaumiza nafsi za wengi wanaopata mali kwa njia za uganga na uchawi sema hawasemi...

SHETANI AKIKUKOPESHA UTALIPA, HATA KAMA UTACHELEWA KUDAIWA.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Mungu hafikiri km mwanadamu, ni mwingi wa rehema. Narudi kumalizia therapy ya kalmanzila, uzuri doctor hachanji wala hahitaji kafara hata ya njiwa hizo ndo connection hatari kwenye ulimwengu wa roho. Mambo yakiniendea vizuri narudi kwa God kikamilifu huku nikifurahia mafanikio niliyoyapata kwenye shirki. Hapo vipi kiongozi
 
Sasa kama unajua ulikuwa sahihi..ni kwa nini ukatuhadithia ndoto zako za kutisha ulizoota?

Mpaka Mungu akakuonesha kwa ndoto ina maana anakuonya...

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: ABJ
nifanyeje kiongozi, hawa watu waliweza kuona nyota yangu haijakaa sawa. Kwenye bible kuna vifungu na muongozo mzuri wa kusafisha kibali changu ili mambo yaniendee vizuri. kama ulishawahi pitia maisha ya kukaa mwezi bila kuingiza hata mia utaelewa. efforts zangu haziniletei matunda
Lia na chumvi ya mawe mkuu
Mshana Jr amekuwa akiimba Kila siku
 
Tubu mrudie mungu. Waganga wengi maisha yao ni ya chini, ya kimasikini. Kama wana uwezo wowote, kwanini wasijisaidie wenyewe kwanza!? Nafikiri wakati wako ulifika tuu, sio mganga. Ukiwa unasali, lazima utafute connection nzuri na uhangaike ku apply sehemu tofauti. Sala zina saidia lkn lazima ujishughulishe mwenyewe.
 
Mwisho wa maelezo yako umeonyesha kuniamini mganga.sasa hapo chagua mwenyewe utazika au utasafirisha?
 
Usiwe vuguvugu utatapikwa chagua moja ni heri ukatengeneza na muumba wako neema bado ipo...tubu Sasa umkabidhi Yesu maisha yako....soon Yesu anarudi kulichukua kanisa lake je upo tayari kwenda naye mwinguni...itakufaa nini uupate ulimwengu mzima na kuipoteza nafsi yako...tafakari chukua hatua ... maranatha [emoji2731]
 
KWENDA KWA MGANGA NI HATARI SANA. TENA SANA.

HUKO UNAWEZA KULIZOA LIROHO LA AJABU AU LIJINI LIKAANZA KUKUSULUBU MAISHANI NA KUKUTIA MARADHI NA MAUMIVU YA MWILI.

HII NINAYOKWAMBIA NI KITU HALISI.

ACHA.
 
Itafikia kipind utatakiwa uitoe sadaka familia
siwezi kufikia kote huko, zaidi ya ada ya buku mbili ninayotoa kupata therapy siwezi toa chochote
 
kwani kunaamri ya Mungu inayosema "USIROGE"
Ndiyo ipo mistari Mingi sana kwenye Biblia inayokataza Kuloga au kufanya uchawi

(Kumbukumbu la Torati 18:10-11)

1. Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,

2.wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Ndiyo ipo mistari Mingi sana kwenye Biblia inayokataza Kuloga au kufanya uchawi

(Kumbukumbu la Torati 18:10-11)

1. Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,

2.wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
ISAYA 8:19-20.

"Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?

Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi."

MAMBO YA WALAWI 19:28

"Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA."
 
Back
Top Bottom